Nauliza swali: Hivi tunaacha kuangalia bunge kwa sababu ya hoja za wapinzani au uongozi wa Makinda?

Ndakilawe

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
4,815
2,814
Leo spika Makinda aliwapatia wabunge wa upinzani nafasi ya kuomba miongozo, halafu akaikataa miongozo yote, then akasema nimewapa nafasi hawa wenzetu waongee, ili kuuonyesha umma kuwa wao ndio wanaofanya wananchi wasiangalie bunge. Pia waandishi wa wahabari waache kuripoti kinazi, na kuponda uongozi wa spika na naibu wake, pamoja na wenyeviti;

Je ni kweli kuwa tunaacha kuangali bunge kwa sababu ya hoja za wapinzani ni mfu, au ukandamizaji unaofanywa na hao viongozi wa bunge wanaotoka CCM?

Naombeni mnisaidie..........
 
Sababu ni udhaifu wa spika na baadhi ya wabunge kuongelea masilai ya chama badala ya wananchi walio wapeleka mjengoni
 
Huyo bibi akikalia kiti hamu ya kuangalia bunge huwa inanitoka ana kiherere kama house girl anaporudi kijijini akitokea mjini kufanya kazi.kaniuzi sana alipokataa mwongozo wa wenje alipotaka kujua mikoa ambayo haina hospital za jeshi watu wake wakatibiwe wapi
 
Aaaaaaaaa, huyu mama kweli ni kichefuchefu yaani alivyo na sura yake ndo hata katika maamuzi yake. Amekuwa dikteta mno. Bunge linapunguza uhuru wake na wabunge wanashindwa kujadili hoja mbalimbali kwa uhuru kisingizio cha kanuni kutumiwa vibaya. Mfano Mh. Mnyika ameomba mwongozo pasipo kumsikiliza anachotaka kukisema kwa kuwa alianza kwa kutoa background ya hilo jambo akamnyamazisha je kitendo hicho ndo kulinda kanuni?
 
Hivi ni wapi naweza kupata anwani ya makinda nimtumie angalau barua ajue ni jinsi gani nimechoshwa na uongozi wake DHAIFU?
 
yote yana mwisho wake time will tell...... siku zilizopita wana ccm walikuwa hawatukani lakini siku hizi wote kazi yao matusi kwa chadema na wananchi mniambie ni kiongozi gani ccm ambae hatukani cdm?
 
Leo spika Makinda aliwapatia wabunge wa upinzani nafasi ya kuomba miongozo, halafu akaikataa miongozo yote, then akasema nimewapa nafasi hawa wenzetu waongee, ili kuuonyesha umma kuwa wao ndio wanaofanya wananchi wasiangalie bunge. Pia waandishi wa wahabari waache kuripoti kinazi, na kuponda uongozi wa spika na naibu wake, pamoja na wenyeviti;

Je ni kweli kuwa tunaacha kuangali bunge kwa sababu ya hoja za wapinzani ni mfu, au ukandamizaji unaofanywa na hao viongozi wa bunge wanaotoka CCM?

Naombeni mnisaidie..........

Nilijaribu siku ya kwanza kuangalia bunge nikasema labda ilikuwa siku mbaya kwa wabunge(kwa mambo ya kitoto na ujinga nilokuwa nasikia na kuona). Nikahama chaneli ingine kuangaliza muziki.

Siku kata tamaa nikajaribu tena siku nyingine. Ilikuwa ndio mbaya zaidi (maana sasa mpaka matusi yakawa yanatolewa), nikadhani labda nimefungua chaneli ingine kimakosa.

Nimeamua kuwaachia wengine nao wajaribu. Nikipata atayenipa habari ya mabadiliko ntajaribu tena kuangalia bunge la Tanzania
 
Back
Top Bottom