Nauli pendekezwa na wakala wa DART

Nauli pendekezwa na wakala wa DART

SNAP J

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
7,117
Reaction score
8,096
Wakala wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam ( DART ) ambao watatoa huduma ya usafiri wa umma katika njia na miundombinu ya DART katika kipindi cha mpito wamependekeza viwango vipya vya nauli kama ifuatavyo;

Kabla ya kufikia uamuzi wa kuridhia viwango hivyo vipya vya nauli, SUMATRA imeandaa mkutano ili kupokea maoni toka kwa wadau mbalimbali utakaofanyika September 15, ukumbi wa Karimjee, DSM kuanzia saa 3 asubuhi.

Wote mnakaribishwa.
 

Attachments

  • 1441787181727.jpg
    1441787181727.jpg
    42.1 KB · Views: 1,311
Karibuni tujadili japo naona ni kubwa sana hii.
 
Naomba kujua njia za pembezoni za Dart ndo zipi hizo ama wanahusika na zile zisizo za mwendo kasi pia?.
 
wasitake makubwa hata huduma haijaanza wanatanganza naulu kubwa kwa kugezo gani? waanze na zilizopo baadaye watu wakizoea waombe mjadara wa bei baada ya kufurahia huduma
 
Hii nauli ni kubwa kuzingatia hali ya maisha ya Mtanzania na viwango vya mishahara! Bora wangeacha nauli ibaki km ikivyokuwa awali!
 
nadhani watu wote watakaofika hawatapata nafasi ya kuongea bali baadhi, sasa ni busara kuanza mjadala huu huku nje ili wale wanaokwenda pale waende na hoja za msingi.

kwangu mimi nadhani ni lazima tuangalie kiasi hiki cha nauli kinatoka wapi?

kwa msingi huo nakumbuka kuwa mabasi haya yamesamehewa kodi na kama hili limefanyika tunategemea liwe na impact kwenye bei atakayopata mtumiaji na sio kwenda kwa mmiriki kumuongezea faida.

nikirudi kwenye aina ya usafiri wenyewe naona kama usafiri huu unatakiwa kuwa wa bei nafuu kutokana na abiria kwenda wamesimama na hivyo kutoa nafasi ya gari kubeba watu wengi zaidi. sina data lakini kwa logic ya kawaida ninaona magari haya yatakuwa yanaendeshwa kwa faida kuliko daladala za sasa ambazo zinabeba watu wamekaa hivyo viwango vya bei sitegemei viwe tofauti na bei za sasa labda kama ni kushuka.

lakini tuangalie impact ya bei hizi kwa wananchi.

mfumo huu haujasambaa vya kutosha ku cover maeneo yote hivyo wananchi wengi watalazima kupanda mabasi yao ya sasa mpaka maeneo yenye mitandao hii ya huduma hizi ambazo pengine ndizo zinazoruhusiwa kuingia mijini na kujikuta wakitumia gharama kubwa sana kwa usafiri.

tunategemea mifumo hii kama imewekwa bila madaraja kwa maana mtu aliyekuwa akitumia gari lake kulipa gharama kubwa lakini ambayo kwa kulinganisha na matumizi yake ya gari ni kidogo sio tatizo isimuongozee mwananchi wa chini ukali wa maisha.

mifumo hii tunaiweka ili kuleta unafuu na sio kutengeneza mifumo ya kuwaumiza masikini na kuwanufaisha matajiri na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaongeza gepu kati ya masikini na tajiri.

haiwezekani kuwalazimisha waendeshaji kutoza gharama ambayo ni ya hasara kwao lakini tunategemea serikali ndiye mtetezi wa wanyonge hawa hivyo atawabana hawa na kukubaliana kiwango cha bei ambacho hakimuumizi yeyote kati ya watumiaji na wamiriki.
 
Si wangemalizia iwe buku tu kuliko kubakia na chenchi ya mia
 
Wakala wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam ( DART ) ambao watatoa huduma ya usafiri wa umma katika njia na miundombinu ya DART katika kipindi cha mpito wamependekeza viwango vipya vya nauli kama ifuatavyo;

Kabla ya kufikia uamuzi wa kurudhia viwango hivyo vipya vya nauli, SUMATRA imeandaa mkutano ili kupokea maoni toka kwa wadau mbalimbali utakaofanyika September 15 , ukumbi wa Karimjee, DSM kuanzia saa 3 asubuhi. Wote mnakaribishwa.
Hebu angalia hawa jamaa wameshatutoa kwenye hoja ya msingi na sasa wanatusahaulisha kwa kutuletea hizi hoja zisizo na mashiko kama ya nauli.
Mbona walipokuja kuwagawia UDA kuendesha huu mradi uliojengwa kwa jasho la Watanzania kwa 100% hawakutuuliza wala kutangaza tender!?
 
kwa style hiyo...wafanye yooote ila watuachie daladala zetu kama kawaida... maana hizo gari zao za mwendokasi wanataka kuzifanya anasa sasa
 
Nauli ghali hafu lazima watu kupanda magari Mara mbili kituoni. Wakati mwanzo ulikuwa unaweza kupanda gari moja hadi posta kwa nauli moja. Sasa hizi nauli si ndo kuongeza ugumu wa maisha
 
Hii nauli ni kubwa kuzingatia hali ya maisha ya Mtanzania na viwango vya mishahara! Bora wangeacha nauli ibaki km ikivyokuwa awali!

Acha kulia lia mmeshaambiwa mchague moja kuendelea kulala wanne pale hosp, kula mlo mmoja kwa siku, kulala kwenye nyumba za tembe au kufanya mabadiliko kutaka maisha bora uamuzi ni wako kusuka au kunyoa Mungu akunyime vyooote akupe akili na maarifa vinginevyo dunia itabaki kuwa mzigo.
 
Chagua sisiem chagua maisha magumu. daladala tunapanda mia sita na lina piga ruti chavhe kwasababu ya foleni. sasa iweje wasio na foleni waongezewe nauli ?????
Bora daladala mara mia.
 
Back
Top Bottom