Natumai Urusi imecheza karata nzuri

Natumai Urusi imecheza karata nzuri

Ghosryder

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
10,707
Reaction score
4,578
Baada ya kuwekewa vikwazo na nchi za magharibi, imeamua kufungua ushirikiano na nchi za umoja wa africa huku ikilaani machafuko yanayoendelea mashariki ya kati, ikidai yamechochewa na NATO baada ya kusambaratisha tawala za Ghadafi na zile tawala zilizokuwa na nguvu,licha ya onyo lake kupinga uvamizi wa kijeshi Libya. Amesaini makubaliano ya ushirikiano na AU mbele ya Mwenyekiti wa AU Bi Dlamini Zuma. Naona ni nafasi nzuri ya Africa kupiga hatua na kuepukana na kiburi cha watu wa Magharibi wanaotulazimisha hadi tuwe mashoga ndio watusaidie.
 
All are thieves. Russia invaded Crimea. Unclean hand tries to shake hand with African.Putin is trying to return Cold war era. Russia is not as rich as westerners. Russia would embrace all African dictators for him to fit in.
 
kwani putin naye na viongozi wa kiafrika wanatofatiana nini? kwenye mambo ya demokrasia? yeye akihisi tu labda unasaidia mtu aliye tishioa kwake, au mwanaharakati utaishia jela tu.Sioni hata jipya ambalo anaweza kuisaidia afrika labda kwenye upande wa kukandamiza democrasia tu na c kingine.Ni misaada kiasi gani ambayo huwa anasidia africa kulinganisha na hao anaowaita wanyonyaji? Bora shetani unaye mjua kuliko maraika usiomjua.
 
Back
Top Bottom