Amba Samedi
Senior Member
- Apr 5, 2024
- 193
- 326
Habari wanajamvi,
Natumaini Jumatatu yako imeanza vyema. Nami pia niko salama. Nimejibanza kwenye kona moja hapa patlivuuu kuandika maneno haya.
Katika pitapita zangu, nlikutana na DukaPro (DukaPro Business Software (Accounting & Point-of-Sale Software)), na nahisi ni programu nzuri kwa usimamizi wa maduka na shule. Hata hivyo, ninatafuta program/software kama hii inaotoa vipengele kadhaa ambavyo DukaPro haina—hasa API kwa ajili ya kutumia na software zingine ambazo nnazo.
Hiki ndicho ninachotafuta kwa sasa:

- Programu inayofaa katika matumizi ya duka na shule (kama DukaPro). Nna wateja kadhaa wamejipanga, lakini siwezi kuscale vya kutosha kwa timu ndogo nliyo nayo.
- Uwezo wa kuibrand – Ili niendeshe biashara chini ya jina la kampuni yangu.
- Bei ya kudumu (lifetime) – Ningependa gharama ya moja kwa moja badala ya malipo ya kila mwezi. Hii ni kutokana na aina ya wateja nnaowahudumia kwa sasa.
- Support – Kipengele hichi ni muhimu sana kwangu. Nlitaka software ambayo nikipata shida, msaada upo, wa kawaida na wa kitaalam.