Natoa onyo kwa wale wote wanaotoa pesa kwa hawa watoto wanaoomba pesa kwa gia ya shikamoo

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,385
Reaction score
2,587
Ni siku ya ijumaa alasiri naelekea kituo cha mabasi ya usafiri kwa raia ndani ya jiji la dar es salaam, hii ni ijumaa tulivu jua lishaanza mapumziko yake, rangi yake maridadi ya kahawia iliyochanganyikana na yangi ya machungwa imetanda angani, hakika ni siku tulivu ndege wanaruka na kuimba kwa shangwe, miti nayo inayumba yumba na upepo mwanana wa kutoka baharini ukipuliza taratibu.

Nikiwa nikijongea kituoni nikiongozana na wanafunzi wenye furaha wakicheza michezo yao barabarani pasipo wasi wa wasi wa bodaboda, kwa mda mfupi nikakumbuka jinsi gani nilivyokuwa na furaha utotoni mwangu kipindi kile kila kitu ni mchezo hata mauwa yalipendeza Zaidi, vyakula vilikuwa vitamu muno hasa hasa pipi, katika mawazo yangu ghafla nikashtukia SHIKAMORE kwa kukurupuka nikajibu marahaba.

Katika kujibu kwangu nikaangalia ni mtoto yupi mwenye adabu na uungwana wa kusalimia wakubwa zake, nikageuza shingo na kichwa kuelekea chini ndipo nikamwona mtoto mzuri mdomo wake mdogo unaoshindwa kufunika meno yake makubwa mapya meupe kama theluji yanamweka mweka, ngozi yake ya usoni laini ikiwa imerembwa na mistari ya vumbi kwenye mashavu kutokana na michezo aliyocheza na wenzake, macho sasa meupe hayana doa yanamatarajio makubwa sana ata kwenye gizaa yatakuwa yanangaa, hakika wanajamii wenzangu yatupasa kuwajali sana watoto hawa kwani wanastaili mengii mema sana kutoka kwetu.

Basi nikiwa nimejawa na furaha tele ghafla mtoto yule nilimsikia akisema naomba pesa ya nauli, ndipo nikajua nature yake kumbe adabu yote ni kwa sababu ya kutaka pesa, daah jamani kumbe hadi watoto ni matapeli wa hisia yaani kumbe kunisalimia kote kwa sababu anataka pesa, hii tabia yapaswa kupigwa kwa nguvu zote.

Kuwa na adabu ni jambo ambalo haliitaji kulipwa, ujumbe kwa wanaoleaa watoto kwamba kuna mambo ya msingi ambayo yanasimama yenyewe kama yenyewe kama utu, heshima, uhuru hizi ni idea ambazo zinasimama zenyewe hutakiwi kumpa mtoto pesa ili aonyeshe adabu au heshima bali mtoto aonyeshe heshima kwa sababu heshima ni kitu kilichopewa thamani na jamii na mtoto atazawadiwa kuitwa mtoto mwenye heshima na jamii full stop nothing more.

Natoa onyo kwa wale wote wanaotoa pesa kwa hawa watoto wanaoomba pesa kwa gia ya shikamore, na kwa wazazi wanaofundisha maadili kwa njia ya kuhonga MSITISHE mara moja tabia hio kwani madhara yake ni exponential katika generation za huko mbele kama huyo mtoto ambaye hajajua thamani ya kweli ya heshima, watoto wake wana asilimia kubwa ya kutokujua pia. Jamani tusingangane sana kuelekeza nguvu zetu zote katika kupata utajiri wa mali kwani kuna utajiri pia wa jamii ya watu wastarabu ambayo dhamani yake haiwezi ikalinganishwa na mkusanyo wowote wa mali za kidunia.
 
We wa hao watoto wanaishi na bibi,single mama,au baba ni mlevi sana anasahau majukumu yake ya kuhudumia familia,mama anampa darasa mtoto jinsi ya kuomba pesa barabarani
 
Ulimpa milioni ngapi ??? ,nimekuelewa kwa machalii kama hao in the years to come they would act as beggars in suits and nice skirts
 
Kalikuwa ni kasichana mbona kama umekaoa sifa kama zote
 
Vilaza utawajua tu yeye....alidhani anaonesha ana uwezo. Kumbe anaonesha kilaza sana.anaandika andika upuuzi mwingi wakati point ilikuqa fupi tu.

Yani hii story ungeandika maneno kumi tu ingeeleweka
 
Vilaza utawajua tu yeye....alidhani anaonesha ana uwezo. Kumbe anaonesha kilaza sana.anaandika andika upuuzi mwingi wakati point ilikuqa fupi tu.
Hahaha maelezo ya dizaini hii angeyapeleka kule Uzi wa kula tunda kimasihara maana kule watu wanataka lugha ya picha kichwani ili wapigie puli
 
Vilaza utawajua tu yeye....alidhani anaonesha ana uwezo. Kumbe anaonesha kilaza sana.anaandika andika upuuzi mwingi wakati point ilikuqa fupi tu.
Ningeandika maneno machache usingeelewa nini nasema haya maneno meng ni kwa ajili yako
 
Mi sina muda wa kusoma upuuzi .nmeona tu unaruka ruka kama maharagwe kwenye maji ya moto nikaenda soma nyuzi za watu wenye akili.

Ningeandika maneno machache usingeelewa nini nasema haya maneno meng ni kwa ajili yako
 
Porojo tupu
Ni siku ya ijumaa alasiri naelekea kituo cha mabasi ya usafiri kwa raia ndani ya jiji la dar es salaam, hii ni ijumaa tulivu jua lishaanza mapumziko yake, rangi yake maridadi ya kahawia iliyochanganyikana na yangi ya machungwa imetanda angani, hakika ni siku tulivu ndege wanaruka na kuimba kwa shangwe, miti nayo inayumba yumba na upepo mwanana wa kutoka baharini ukipuliza taratibu.

Nikiwa nikijongea kituoni nikiongozana na wanafunzi wenye furaha wakicheza michezo yao barabarani pasipo wasi wa wasi wa bodaboda, kwa mda mfupi nikakumbuka jinsi gani nilivyokuwa na furaha utotoni mwangu kipindi kile kila kitu ni mchezo hata mauwa yalipendeza Zaidi, vyakula vilikuwa vitamu muno hasa hasa pipi, katika mawazo yangu ghafla nikashtukia SHIKAMORE kwa kukurupuka nikajibu marahaba.

Katika kujibu kwangu nikaangalia ni mtoto yupi mwenye adabu na uungwana wa kusalimia wakubwa zake, nikageuza shingo na kichwa kuelekea chini ndipo nikamwona mtoto mzuri mdomo wake mdogo unaoshindwa kufunika meno yake makubwa mapya meupe kama theluji yanamweka mweka, ngozi yake ya usoni laini ikiwa imerembwa na mistari ya vumbi kwenye mashavu kutokana na michezo aliyocheza na wenzake, macho sasa meupe hayana doa yanamatarajio makubwa sana ata kwenye gizaa yatakuwa yanangaa, hakika wanajamii wenzangu yatupasa kuwajali sana watoto hawa kwani wanastaili mengii mema sana kutoka kwetu.

Basi nikiwa nimejawa na furaha tele ghafla mtoto yule nilimsikia akisema naomba pesa ya nauli, ndipo nikajua nature yake kumbe adabu yote ni kwa sababu ya kutaka pesa, daah jamani kumbe hadi watoto ni matapeli wa hisia yaani kumbe kunisalimia kote kwa sababu anataka pesa, hii tabia yapaswa kupigwa kwa nguvu zote.

Kuwa na adabu ni jambo ambalo haliitaji kulipwa, ujumbe kwa wanaoleaa watoto kwamba kuna mambo ya msingi ambayo yanasimama yenyewe kama yenyewe kama utu, heshima, uhuru hizi ni idea ambazo zinasimama zenyewe hutakiwi kumpa mtoto pesa ili aonyeshe adabu au heshima bali mtoto aonyeshe heshima kwa sababu heshima ni kitu kilichopewa thamani na jamii na mtoto atazawadiwa kuitwa mtoto mwenye heshima na jamii full stop nothing more.

Natoa onyo kwa wale wote wanaotoa pesa kwa hawa watoto wanaoomba pesa kwa gia ya shikamore, na kwa wazazi wanaofundisha maadili kwa njia ya kuhonga MSITISHE mara moja tabia hio kwani madhara yake ni exponential katika generation za huko mbele kama huyo mtoto ambaye hajajua thamani ya kweli ya heshima, watoto wake wana asilimia kubwa ya kutokujua pia. Jamani tusingangane sana kuelekeza nguvu zetu zote katika kupata utajiri wa mali kwani kuna utajiri pia wa jamii ya watu wastarabu ambayo dhamani yake haiwezi ikalinganishwa na mkusanyo wowote wa mali za kidunia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu walikuwa wanaomba hela sana watu wasio wajua walipokuwa wadogo sasa nadhani walitoa vyao pia kwa namna moja au nyingine
Chizi Maarifa we ni muhanga
 
Back
Top Bottom