Nato yasambaratisha vikundi 22 vya maharamia baharini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nato yasambaratisha vikundi 22 vya maharamia baharini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Meli ya kivita ya Uingereza, HMS Chatham, ikiwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam jana. Meli hiyo ambayo iko katika operesheni ya kulinda bahari chini ya mwamvuli wa Majeshi ya Kulinda Amani ya Nato, iliwasili juzi na itakuwapo nchini kwa siku tano kwa mazoezi mbalimbali na vikosi vya wanamaji wa Jeshi la Wananchi wa Watanzania (JWTZ).  Vikosi vya majeshi ya kujihami (Nato), vinavyoendesha operesheni ya kupambana na maharamia katika Ghuba ya Aden na Somalia, vimefanikiwa kusambaratisha vikundi 22 vya maharamia katika Bahari ya Hindi na kuzuia mashambulizi 15 yaliyopangwa kufanywa na watu hao.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kiongozi wa kikosi cha meli ya kivita ya HMS Chatham kinachofanya operesheni hiyo, Kamanda Steve Chick, alisema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa nchi mbalimbali.
  Kamanda Chick ambaye meli anayoisimamia ipo nchini kwa siku tano kuanzia juzi, alisema ziara yao hapa nchini inalenga kubadilishana uzoefu na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ili kuona namna Tanzania itakavyosaidia kupambana na uharamia.
  Alisema operesheni hiyo ambayo ilianza mwaka jana, itamalizika Desemba, mwakani na kueleza kuwa suluhisho la kudumu la maharamia ni ushirikiano wa nchi zote.
  Kwa upande wake, kapteni wa meli hiyo, Simon Huntington, alisema kikosi hicho kinajumuisha wanajeshi waliopewa mafunzo ya hali ya juu na wenye uwezo wa kutumia vifaa vya kisasa vyenye uwezo wa kufanya msako kwenye eneo kubwa.
  “Kwa hiyo tukiwa Tanzania, tutabadilishana uzoefu na kujenga mfumo wa kubadilishana taarifa pindi maharamia wanapoonekana kwenye ukanda huu,” alisema.
  Balozi wa Uingereza nchini, Diana Corner, aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kukubali kurekebisha sheria zake ili kuruhusu maharamia kushtakiwa hapa nchini.
  Alisema kitendo hicho kimedhihirisha namna Tanzania inavyoungana na Jumuiya za Kimataifa kukabiliana na tatizo la maharamia.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...