WIZI MTUPU!!! Mkuu jamaa wameshatimiza lengo leo la kuweka kituo cha jeshi Africa na pia kuwaweka vibaraka wao madarakani. Kama sikosei pesa zote za Libya zilizokuwa katika bank accounts za nje ya nchi zilikuwa hazifiki $200 billion sasa wameshaenda kubambikwa deni la $480 Billion!!!!! Utamdai vipi mtu ikiwa hamkuwa na makubaliano naye ya awali? kwamba nitatumia pesa (sijui ni kiasi gani) halafu gharama kamili nitakuletea unilipe? hivi kule kwingine walikovamia pia walipeleka bakuli lao ili walipwe gharama zao walizoingia katika uvamizi ule!!!?
Mkuu BAK,
Wajinga ndo waliwao,na kama hakuna wajinga dunia ingekuwaje?
Waliambiwa hizo bilioni $170 zote zitakuwa unfrozen pindi Gaddafi akiuwawa.
Gaddafi kauwawa,na hadi sasa wamepewa hiyo bilioni moja tu!
Sasa badala ya kuwakopesha hao waasi pesa za kumwondoa Gaddafi,kwanini wasingewapa hizo pesa wanazodaie eti zilikuwa za Gaddafi binafsi ili ndo zitumike bila ya haja ya kuwa na madeni?
Again,wamewaambia kuwa zitatolewa kama kukishakuwa na stability,kwa maana rahisi kabisa ni kwamba hawatakaa wazipate.(naamini stability ni ndoto kwa Libya in the near future)
Na hata wakizipata,mahesabu yake yatakuwa ya kimizenguo tu.
Hao waasi ni wajinga sana,wao wanadhani kuwa NATO walipokaa kimya kuhusu wao kutumia Alkaeda ni wajinga.
Hiyo ndo sababu watakatoitumia kwa black mail na kuwageuka.
Kwa kifupi Libya anaye i own ni NATO.
Libya ni taifa la NATO na si la Walibya.
Kuna mahali Gaddafi alifanya kosa kuhusiana na fikra za young Libyans,na inawezekana ni kwenye kuwapatia elimu stahiki ya mwafrika.
Sasa kama yeye aliwaachia wakaona wataliano na wafaransa ni watu muhimu zaidi,then these are the consequences.
Same mistakes wanazofanya viongozi wetu,wanapotembeza bakuli na rais kiguu na njia kila kukicha,basi wananchi ni lazima wawaone hao wazungu wanaoombwa kuwa ni watu wa maana,na kama wakitaka kuwaondoa,wananchi watakubali kiurahisi kutokana na how viongozi acts.