Natishia kutengwa kisa mke wa Sumbawanga

Akademician

Senior Member
May 20, 2015
143
36
Habarini ndugu wanajukwaa.
Kuna rafiki zangu wapatao watatu ambao tumekuwa tukishirikiana kwa mambo mengi na kusaidiana hata kiuchumi na maarifa,
Tumekuwa tukiishi kindugu kabisa.

Wawili wana wana ndoa zao na watoto,
Mmoja ana mchumba tu.
Mimi nimekuwa singo kwa muda fulani tangu nifarakane na aliyekuwa mchumba wangu.

Sasa nimekutana na binti mmoja wa huko Sumbawanga,
Ila kwa sasa anaishi hapa Dar.
Katika urafiki wa takribani miezi 6 tumeafikiana kufunga ndoa.

Sasa nimewashirikisha hawa rafiki zangu wameanza kuweka ngumu,
Wanasema hapa Kuna tunguli za kifipa kutoka Sumbawanga zimetumika kunivuta kuoa,
Haiwezekani iwe haraka kiasi hicho.
Na wanadai nisipoangalia vema limbwata litazidi zaidi baada ya ndoa.
Wamepinga vikali na wameweka msimamo wa kujitenga nami Kabisa Kwenye hilo na hakuna Hata Mmoja anayeniunga mkono.

Ushauri wakuu.
 
Katika ndoa, mwanaume kula mizizi utegemee, lisipotokea sema asante!
Silaha kubwa ya mwanaume ni KUJIAMINI... Tunguli zipo kila mahali.
 
uchaw upo kila mahali sio kwa sumbawanga tu, na kuwa mzaliwa wa sumbawanga haimaanishi kuwa yeyote tu ni mchawi, hapana kama unapenda kweli sioni sababu kutokuoa. hao rafik zako watakataa but mwisho wa cku watakubali matokeo tu! kama unampenda muoe plz
 
Mkuu achana nao mbona mimi mwenyewe nimeolea Sumbawanga na maisha tunayasongesha fresh,tena Wafipa wana nidhamu sana wala hakuna cha limbwata.Kuhusu Limbwata hata ukioa mtu wa kabila lako km ni wa kuwekewa utawekewa tu.Achana nao kwani wao ni akina nani eeboo.
 
Kisemacho kipo,kama hakipo,kinajongea.Fanya utafiti kuhusu wasemacho marafiki zako,ndio ufanye uamuzi binafsi.
 
Unajua mtu kukupa ushauri ni kitu kimoja, na wewe kuamua kuufanyia kazi au kutoufanyia kazi huo ushauri ni kitu kingine kabisa, tatizo linakuja pale mtu anapokushauri na kukulazimisha kuufanyia kazi ushauri wake tena huku anakuwekea masharti.

Personally I think such people should grow up and learn to respect each others freedom of choice. Do you.
 
Mimi nimezaliwa sumbawanga hakuna mambo hayo zaidi ya magezitini tu by the way uchawi upo kila sehemu
 
Yaan miezi 6 unataka ndoa???????? ok we kafunge baada ya hapo uje na mirejesho km ya #monica.
 
Yaan miezi 6 unataka ndoa???????? ok we kafunge baada ya hapo uje na mirejesho km ya #monica.
 
Yaan miezi 6 unataka ndoa???????? ok we kafunge baada ya hapo uje na mirejesho km ya #monica.
 
hata mwez mngeoana tu,mengine tabia ya mtu.Waulize waliochunguzana kuanzia mwaka Afu wakafunga ndoa kama wote ndoa ni tulivu au kwann wameachana.oa tu baba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom