Valencia_UPV
JF-Expert Member
- Mar 31, 2016
- 7,682
- 9,557
Unguja tunataka mgao wetu tu
Za nini zote hizo? Au urembo? Kama kutumia kimaisha PhD moja tu inatosha in a lifetimeClassmates wengi Wana PhD Zaidi ya moja
Umeeleweka mkuu, kuna haja ya kukaa chini na Wawekezaji hao kama walivyofanya Botswana wakapata 50 % stake kwenye kampunu DeBeer's ambayo inachimba almasi ....Dah! Siku kibao sipo JF, na hapa nimekuja kunusa tu!
Anyway, ingawaje hii mada ni pana sana lakini👇👇👇
Hapo juu umemaliza kila kitu. Labda nitoe changamoto kwa Juma1967 na wengineo kusoma "misahafu" ifuatayo:-
1. Sheria ya Mafuta ya 2015,
2. Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi ya 2015, na
3. Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania ya mwaka 2015.
Ili upate picha kubwa zaidi, ongeza na Sera ya Nishati ya Taifa ya 2015 bila kusahau Model Production Sharing Agreement ya 2013.
Binafsi nimesoma zote hizo, lakini kwa sasa sitafanya reference yoyote kwavile nimekuja kuchungulia tu. Ukisoma sheria tajwa hapo juu, pamoja na hizo supplement ndipo mtu moja kwa moja atakuja kwenye hoja yako yapo juu.
Waswahili wanasema Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni. Pamoja na madudu yote ya Serikali ya JK, kwangu mimi sheria hizo hapo juu ndio sheria bora kabisa kuwahi kutungwa nchi hii!
Zaidi ya miaka 5 iliyopita nilipoisoma hiyo Model Production Sharing Agreement ya 2013, hapo hapo nikajua lazima Wawekezaji WAIGOMEE.
Niliamini lazima waigomee kwa sababu, Serikali ingekuwa inachukua percent kubwa sana... from 50% and above kutegemeana na umri wa project.
Na ninaposema 50% and above sio including Tax bali model inapendekeza huo ndo mgawanyo wa mapato ya mafuta na gesi kati ya serikali na mwekezaji AFTER TAX.
TIP: Mwishoni mwa mwaka jana kuliripotiwa taarifa za Serikali kuingia mkataba wa utafutaji na uchimbaji gas na kampuni fulani kule Ruvuma. January Makamba akataja percent ambayo serikali itapata lakini hapa JF watu wakabisha sana kwa sababu ni kama haingii akilini!
Anyway, ni kweli ni kama haingii akilini lakini hivyo ndivyo inavyosema Model Production Sharing Agreement! Na ni kutokana na mashaka hayo ndo maana nikaamini LAZIMA Wawekezaji wataogomea.
What happened next? June 25, 2022 The Citizen wakaja na habari titled:
Tanzania in a new initiative to attract oil, gas investors
Na sehemu ya habari hiyo inasema:-
Yaani kama ambavyo nilivyoshuku hapo kabla kwamba Investors lazima wataogomea MPSA, na kweli bado wanatia ngumu! The Citizen wanaendelea:-
Na kwa nyongeza tu, National Energy Policy inatamka wazi kwamba Raslimali ya Mafuta na Gesi ni Mali ya WATANZANIA.
Ni kutokana na hilo, ndo maana Sheria ya Mafuta ya 2015 nayo inatamka wazi kwamba MMILIKI WA LESENI za Vitalu vya Mafuta na Gesi ni National Oil Company.
National Oil Company ni Kampuni inayotakiwa kuanzishwa kwa mujibu wa sheria hiyo hapo juu, na NOC ndiyo ita-takeover shughuli za TPDC.
So, according to sheria hiyo hiyo, Kampuni YOYOTE inayotaka kuendesha shughuli za uchimbaji mafuta na gesi ni LAZIMA iingie UBIA na mmiliki wa vitalu hivyo, yaani NOC!
Aidha, sheria inaendelea kusema kwamba NOC wanatakiwa KUMILIKI ANGALAU 25% of Production Interest na kampuni yoyote inayotaka kuchimba mafuta na gesi, unless...
Sasa ukisoma maelezo hayo hapo juu ndipo tunarudi kwenye hoja yako ambayo nimesema umemaliza kila kitu!
Kwenye Gas and Oil Industry, 25% ni KUBWA SANA... je, NOC/TPDC wana ubavu wa kufanya cost sharing itakayowawezesha kumiliki 25% ya hisa ya vitalu?!
Ukweli ni kwamba NOC hawana pesa hiyo na ndo maana sheria imeweka loophole just in case NOC wanashindwa kumiliki AT LEAST 25%.
Na labda nikurekebishe kidogo, huenda umekosea tu uliposema
Actually, huo sio uwekezaji kwenye gesi bali uwekezaji kwenye Gas Processing Plant ONLY ambao ni zaidi ya TZS 70 TRILLION. Hizo ni fixed costs kwa ajili ya miundombinu!!
Sasa ukiangalia such massive investment inayohitajika kwenye gas industry, makarabrasha yetu yanaweza kusema wazi kwamba GAS NI MALI YA WATANZANIA but practically, lack of capital and technology hilo suala la Mali ya Watanzania litabaki kuwa theory tu!
Na kama The Citizens linavyosema, kuna kila dalili SSH ameanza kutepeta, na ukweli mchungu ni kwamba, HANA CHOICE unless, ama tuwe na mtaji wa kutosha na teknolojia sisi wenyewe au turudi kwenye kauli za enzi za Mwalimu kwamba "Gesi HAIOZI"!!!
Bandari bye byeWakuu mm sijasoma Sana, Nina BSc. Civil Engineering tu. Ila nimekutana na hii kitu huko kwenye majarida ya kisomi. Naomba mliosoma mnisaidie;
1. Kama hii kitu (NATIONAL SOVEREIGNTY ON NATURAL RESOURCES) ipo nchi yoyote Afrika? Mule Geita tuna chetu? Gesi Mtwara je? Tanzanite? Almasi Mwadui?
2. Vyama vya upinzani vinajua wajibu wao au nao ni wale wale?
3. Hapa Zanzibar tunapambana na Mwani tu utalii wanafaidi wachache.
NB: Narudia, Mimi Ni Ngumbaru Mwerevu.
Kusoma andiko nililotumia Sovereignty over natural resources – A normative reinterpretation | Global Constitutionalism | Cambridge Core