National Sovereignty on Natural Resources in Africa

and 998 others

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
27,921
Reaction score
39,116
Wakuu mm sijasoma Sana, Nina BSc. Civil Engineering tu. Ila nimekutana na hii kitu huko kwenye majarida ya kisomi. Naomba mliosoma mnisaidie;

1. Kama hii kitu (NATIONAL SOVEREIGNTY ON NATURAL RESOURCES) ipo nchi yoyote Afrika? Mule Geita tuna chetu? Gesi Mtwara je? Tanzanite? Almasi Mwadui?

2. Vyama vya upinzani vinajua wajibu wao au nao ni wale wale?

3. Hapa Zanzibar tunapambana na Mwani tu utalii wanafaidi wachache.

NB: Narudia, Mimi Ni Ngumbaru Mwerevu.

Kusoma andiko nililotumia Sovereignty over natural resources – A normative reinterpretation | Global Constitutionalism | Cambridge Core
 
Attachments

Tatizo hatuna mitaji wala utaalamu unategemea sovereignty tuitoe wapi? Mfano tu Gesi inahitaji uwekezaji wa zaidi ya Trillion 60 unadhani utampata mwekezaji Gani atoe pesa yote hiyo alafu mgawane pasu kwa pasu?? Okay pesa shida Bado wataalam wenye uwezo wa kuchimba na kugundua wapo wachache so hakuna namna zaidi ya kuwaachia tu wachote ila walipe Kodi stahiki n.k

2. Wapinzani wanajua kazi Yao ila tatizo katiba yetu hairuhusu mtu yoyote kumchallenge Rais. Mfano wapinzani walitumia bunge sana kupinga mikataba na Sheria kadhaa lakini wakikataa mfano bajeti ya Samia technically bunge linavunjwa!! Wakisema waje nje ya bunge wakitoa takwimu tu za wizi kwenye madini wanakutana na panga la Sheria ya takwimu na cybercrime!! N.k
 
Arabuni walifanyaje? Mbona wao wamefanikiwa?
 
Miscellaneous amendments zilipelekwa bungeni 2017 kurekebisha Sheria ya Madini ikiwemo hiyo Sheria inayohusiana na hiyo mada. Sheria hii imetuwezesha kama nchi UMMA kumiliki kisheria maliasili zetu zikiwemo Madini. Moja ya faida ya Sheria hii ni Sisi kupata 16% Free Carried Interest FCI ktk uwekezaji mkubwa wowote ktk Madini. Pia kuwa na uwezo wa kununua Hisa zingine. Ishu ya muhimu sana nyingine ni kugawana faida 50/50. Kutokana na Sheria hii imezaliwa kanuni ya Local content ambayo inawataka wawekezaji kununua huduma Kutoka Kwa local supplier.
Kiufupi Sheria hii ipo na imesaidia sana ktk kuongeza mchango wa sekta ya Madini ktk Pato la taifa kutoka 3.5% wakati inaanzishwa Hadi 7.9 Leo.
Nadhani Kwa uelewa wangu wa darasa la chekechekea nimejaribu.
Inaitwa Natural Wealth and Resources permanent Sovereignty Act 2017
 
Wakuu mm sijasoma Sana, Nina BSc. Civil Engineering tu. Ila nimekutana na hii kitu huko kwenye majarida ya kisomi. Naomba mliosoma mnisaidie;

1. Kama hii kitu (NATIONAL SOVEREIGNTY ON NATURAL RESOURCES) ipo nchi yoyote Afrika? Mule Geita tuna chetu? Gesi Mtwara je? Tanzanite? Almasi Mwadui?

2. Vyama vya upinzani vinajua wajibu wao au nao ni wale wale?

3. Hapa Zanzibar tunapambana na Mwani tu utalii wanafaidi wachache.

NB: Narudia, Mimi Ni Ngumbaru Mwerevu.
BSc Civil Engineering hujasoma? MMMMMMM
 
Miscellaneous amendments zilipelekwa bungeni 2017 kurekebisha Sheria ya Madini ikiwemo hiyo Sheria inayohusiana na hiyo mada. Sheria hii imetuwezesha kama nchi UMMA kumiliki kisheria maliasili zetu zikiwemo Madini. Moja ya faida ya Sheria hii ni Sisi kupata 16% Free Carried Interest FCI ktk uwekezaji mkubwa wowote ktk Madini. Pia kuwa na uwezo wa kununua Hisa zingine. Ishu ya muhimu sana nyingine ni kugawana faida 50/50. Kutokana na Sheria hii imezaliwa kanuni ya Local content ambayo inawataka wawekezaji kununua huduma Kutoka Kwa local supplier.
Kiufupi Sheria hii ipo na imesaidia sana ktk kuongeza mchango wa sekta ya Madini ktk Pato la taifa kutoka 3.5% wakati inaanzishwa Hadi 7.9 Leo.
Nadhani Kwa uelewa wangu wa darasa la chekechekea nimejaribu.
Inaitwa Natural Wealth and Resources permanent Sovereignty Act 2017
kwa uelewa wangu Nafikiri suala la umiliki wa Rasimali zetu upo katika sheria za kimataifa ,Nafikiri watawala wanatakiwa ku implement hii sheria kwa kuingiza serikali yetu katika makubaliano maalum na hizi foreign powers tunahitaji 50/50 stake na siyo 16% .Hii 16% haina impact kubwa kwenye uchumi wetu,,bahati nzuri haya makampuni makubwa yanauza hisa zao kupitia London stock exchange ......
 
Arabuni walifanyaje? Mbona wao wamefanikiwa?
Mkuu hata huko mabeberu ndio wanaochimba na kuuza mafuta tofauti ni mgao tu unakua mzuri kupitia hizo production-sharing agreements. Sasa nchi kma zile Zina mafuta na gesi so hata wakipata 30% ya faida inatosha kuwafanya kuwa mabilionea ndani ya muda mfupi.

So sisi tunakwama hapo kwenye mikataba.... No wonder Sheria ya TEITI inataka mikataba ya rasilimali ipelekwe bungeni ila JPM hakuwahi sio tu kupeleka mikataba bungeni Bali hata kukubali ripoti za ukaguzi za TEITI kusomwa bungeni (Nimesema JPM coz ndio wakati hiyo Sheria ilianza tumika)

Mpaka tutakapokuwa serious hatutofaidika.
 
Asante. Ndo kusema GOOD GOVERNANCE Ni kipengele hapa kwetu?
 
Mkuu hata huko mabeberu ndio wanaochimba na kuuza mafuta tofauti ni mgao tu unakua mzuri kupitia hizo production-sharing agreements. Sasa nchi kma zile Zina mafuta na gesi so hata wakipata 30% ya faida inatosha kuwafanya kuwa mabilionea ndani ya muda mfupi.

So sisi tunakwama hapo kwenye mikataba.... No wonder Sheria ya TEITI inataka mikataba ya rasilimali ipelekwe bungeni ila JPM hakuwahi sio tu kupeleka mikataba bungeni Bali hata kukubali ripoti za ukaguzi za TEITI kusomwa bungeni (Nimesema JPM coz ndio wakati hiyo Sheria ilianza tumika)

Mpaka tutakapokuwa serious hatutofaidika.
Unacho sema sio kweli kaka hao WARAAB wanamiliki kila kitu kwenye sector ya energy hakuna Beberu wa nani na ndio maana wanajeuri hata kwa AMERICA na kupa mfano mmoja tu ARAMCO co ndio the richest company in the world ambayo inamilikiwa 99% Saudi Government hii ni Energy company mifano ipo mingi tu ila huu mmoja tu.
 
Vyama vya upinzani vinajua wajibu wao au nao ni wale wale?
Ni aibu sana kwa taifa kama mleta mada unasema una shahada halafu ndiyo unajenga hoja za kijinga kiasi hiki??

Huko chuo utakuwa umetoka na magonjwa ya zinaa tu na karatasi ngumu (unayoita cheti) inayokutambuulisha kuwa ulikuwa unahudhuria masomo ngazi ya shahada lkn umetoka mtupu kichwani.

Jukumu la kupigania rasilimali na haki ktk taifa siyo ya vyama vya upinzani pekee, ni ya kila raia.

Nilitegemea uandike kuwa umefanya nn na hicho kishahada chako uchwara ili kupambania rasilimali za nchi yako badala ya kuketa pumba za kulaumu vyama vya upinzani.
 
Unacho sema sio kweli kaka hao WARAAB wanamiliki kila kitu kwenye sector ya energy hakuna Beberu wa nani na ndio maana wanajeuri hata kwa AMERICA na kupa mfano mmoja tu ARAMCO co ndio the richest company in the world ambayo inamilikiwa 99% Saudi Government hii ni Energy company mifano ipo mingi tu ila huu mmoja tu.
Lakini ARAMCO haikua fully owned na serikali tokea siku ya kwanza, ilianza na hisa below 25% kama tu ambavyo Tanzania na sisi tuna shares za 16% kwenye Twiga minerals etc sema with time ndio wakawa wananunua hisa Hadi wakaimiliki yote. Ila point ni kwamba walianza wakiwa zero ila kupitia mikataba mizuri ndio wakaweza kupata uwezo wa kujinasua.

Ila nchi kama Qatar unakuta mikataba ni ya ubia kati ya serikali na makampuni ya uvumbuzi wa gesi kama Exxon Mobil, Total n.k ila mwisho wa siku mgawanyo unakua fair na hicho ndio Cha msingi.

Nchi kama Tz hatuwezi kuwa kama Qatar au Saudia kwa ghafla tu kwamba tumiliki mfano Mapato ya gesi kwa 100% lazima tuanze mahali na ndio maana nikasema mikataba mizuri itatufikisha huko.
 
kwa uelewa wangu Nafikiri suala la umiliki wa Rasimali zetu upo katika sheria za kimataifa ,Nafikiri watawala wanatakiwa ku implement hii sheria kwa kuingiza serikali yetu katika makubaliano maalum na hizi foreign powers tunahitaji 50/50 stake na siyo 16% .Hii 16% haina impact kubwa kwenye uchumi wetu,,bahati nzuri haya makampuni makubwa yanauza hisa zao kupitia London stock exchange ......
Hizo Hisa unazozisema ndio zinazoleta mitaji mzee. Ukisema shares ziwe 50/50 halafu hizo za serikali ziwe za Bure basi huo mradi sijui kama utafanikiwa. Kinachotakiwa ni serikali kuingia kwenye management ya project hiyo yaani kuanzia manunuzi na usimamizi. 16% FCI ni Hisa za bure ambazo zinaruhusu kama nchi kuingia kwenye management.
 
Ninachosema ni kwamba siyo hisa za bure , tununue hizo hisa mpaka tumiliki 50%stake .kupitia hayo masoko ya hisa ...
 
Dah! Siku kibao sipo JF, na hapa nimekuja kunusa tu!

Anyway, ingawaje hii mada ni pana sana lakini👇👇👇
Tatizo hatuna mitaji wala utaalamu unategemea sovereignty tuitoe wapi? Mfano tu Gesi inahitaji uwekezaji wa zaidi ya Trillion 60 unadhani utampata mwekezaji Gani atoe pesa yote hiyo alafu mgawane pasu kwa pasu?? Okay pesa shida Bado wataalam wenye uwezo wa kuchimba na kugundua wapo wachache so hakuna namna zaidi ya kuwaachia tu wachote ila walipe Kodi stahiki n.k
Hapo juu umemaliza kila kitu. Labda nitoe changamoto kwa Juma1967 na wengineo kusoma "misahafu" ifuatayo:-

1. Sheria ya Mafuta ya 2015,
2. Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi ya 2015, na
3. Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania ya mwaka 2015.

Ili upate picha kubwa zaidi, ongeza na Sera ya Nishati ya Taifa ya 2015 bila kusahau Model Production Sharing Agreement ya 2013.

Binafsi nimesoma zote hizo, lakini kwa sasa sitafanya reference yoyote kwavile nimekuja kuchungulia tu. Ukisoma sheria tajwa hapo juu, pamoja na hizo supplement ndipo mtu moja kwa moja atakuja kwenye hoja yako yapo juu.

Waswahili wanasema Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni. Pamoja na madudu yote ya Serikali ya JK, kwangu mimi sheria hizo hapo juu ndio sheria bora kabisa kuwahi kutungwa nchi hii!

Zaidi ya miaka 5 iliyopita nilipoisoma hiyo Model Production Sharing Agreement ya 2013, hapo hapo nikajua lazima Wawekezaji WAIGOMEE.

Niliamini lazima waigomee kwa sababu, Serikali ingekuwa inachukua percent kubwa sana... from 50% and above kutegemeana na umri wa project.

Na ninaposema 50% and above sio including Tax bali model inapendekeza huo ndo mgawanyo wa mapato ya mafuta na gesi kati ya serikali na mwekezaji AFTER TAX.

TIP: Mwishoni mwa mwaka jana kuliripotiwa taarifa za Serikali kuingia mkataba wa utafutaji na uchimbaji gas na kampuni fulani kule Ruvuma. January Makamba akataja percent ambayo serikali itapata lakini hapa JF watu wakabisha sana kwa sababu ni kama haingii akilini!

Anyway, ni kweli ni kama haingii akilini lakini hivyo ndivyo inavyosema Model Production Sharing Agreement! Na ni kutokana na mashaka hayo ndo maana nikaamini LAZIMA Wawekezaji wataogomea.

What happened next? June 25, 2022 The Citizen wakaja na habari titled:

Tanzania in a new initiative to attract oil, gas investors

Na sehemu ya habari hiyo inasema:-
The government of Tanzania is readying to amend the Model Production Sharing Agreements (MPSAs) of 2013 to loosen conditions in the oil and gas sector after Tanzania failed to sell any exploration block during the past nine years.
Yaani kama ambavyo nilivyoshuku hapo kabla kwamba Investors lazima wataogomea MPSA, na kweli bado wanatia ngumu! The Citizen wanaendelea:-
The changes will take into consideration the global trends in trade, fuel prices over the past decade and estimates for the next decade, the institutional changes in Tanzania and current legal system, including the Petroleum Act of 2015, which is said to be unfavourable to investors.
Na kwa nyongeza tu, National Energy Policy inatamka wazi kwamba Raslimali ya Mafuta na Gesi ni Mali ya WATANZANIA.

Ni kutokana na hilo, ndo maana Sheria ya Mafuta ya 2015 nayo inatamka wazi kwamba MMILIKI WA LESENI za Vitalu vya Mafuta na Gesi ni National Oil Company.

National Oil Company ni Kampuni inayotakiwa kuanzishwa kwa mujibu wa sheria hiyo hapo juu, na NOC ndiyo ita-takeover shughuli za TPDC.

So, according to sheria hiyo hiyo, Kampuni YOYOTE inayotaka kuendesha shughuli za uchimbaji mafuta na gesi ni LAZIMA iingie UBIA na mmiliki wa vitalu hivyo, yaani NOC!

Aidha, sheria inaendelea kusema kwamba NOC wanatakiwa KUMILIKI ANGALAU 25% of Production Interest na kampuni yoyote inayotaka kuchimba mafuta na gesi, unless...

Sasa ukisoma maelezo hayo hapo juu ndipo tunarudi kwenye hoja yako ambayo nimesema umemaliza kila kitu!

Kwenye Gas and Oil Industry, 25% ni KUBWA SANA... je, NOC/TPDC wana ubavu wa kufanya cost sharing itakayowawezesha kumiliki 25% ya hisa ya vitalu?!

Ukweli ni kwamba NOC hawana pesa hiyo na ndo maana sheria imeweka loophole just in case NOC wanashindwa kumiliki AT LEAST 25%.

Na labda nikurekebishe kidogo, huenda umekosea tu uliposema
Gesi inahitaji uwekezaji wa zaidi ya Trillion 60
Actually, huo sio uwekezaji kwenye gesi bali uwekezaji kwenye Gas Processing Plant ONLY ambao ni zaidi ya TZS 70 TRILLION. Hizo ni fixed costs kwa ajili ya miundombinu!!

Sasa ukiangalia such massive investment inayohitajika kwenye gas industry, makarabrasha yetu yanaweza kusema wazi kwamba GAS NI MALI YA WATANZANIA but practically, lack of capital and technology hilo suala la Mali ya Watanzania litabaki kuwa theory tu!

Na kama The Citizens linavyosema, kuna kila dalili SSH ameanza kutepeta, na ukweli mchungu ni kwamba, HANA CHOICE unless, ama tuwe na mtaji wa kutosha na teknolojia sisi wenyewe au turudi kwenye kauli za enzi za Mwalimu kwamba "Gesi HAIOZI"!!!
 
Back
Top Bottom