Natia nia ya kugombea uongozi kwenye chama cha ACT-Wazalendo

Kifwimbo

New Member
Aug 7, 2019
3
1
🖐NAMI NATIA NIA🖐.
Nianze kwa kuwapa pole ndugu zetu wa mikoa ya Lindi,tabora,Dodoma na maeneo mengine ya nchi kwa maafa ya mvua zilizopita kiwango na kusababisha maafa pole sana Ndugu zangu mwenyezi Mungu awatie nguvu na kuwapa subra katika kipindi hiki kigumu.

Najitokeza hadhari mbele ya umma wanachama na wapenzi wa chama chetu ACT WAZALENDO.

kama tunavyojua sote mchakato wa uchaguzi wa chama Taifa umefunguliwa rasmi.

Nami kama mwanachama kindakindaki wa Act wazalendo nakusudia kutia nia kuomba ridhaa kwa wanachama wenzangu ili tuendeleee kuijenga act wazalendo imara.

Nimetafakari kwa kina nimeona ninatosha pasipo shaka kutia nia ya kuingoza act wazalendo katika nafasi adhimu na ya JUU kabisa ya KIONGOZI WA CHAMA (party leader) inayoshikiliwa na mbunge wetu mahili na shupavu Zitto Z. Kabwe.

Ndugu wanachama wa act wazalendo natambua
Katika kufikia malengo yoyote lazima tuwe na mpango na mpango ni mkakati fanikishi wa malengo husika.

Kwa msingi huo nitahakikisha Ngome zote (idara) zinakua na mpango kazi wa mwaka kulingana na mwelekeo wa chama kwa mwaka husika.

Aidha Pamoja na viongozi wenzangu kupitia ofisi ya katibu mkuu tutaweka utaratibu wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango ya ngome zote (idara) kila baada ya miezi3 ili kuongeza ufanisi kiutendaji katika mipango ya ngome zetu kuanzia taifa mpaka matawi.

Natambua VIJANA ndiyo Nguvu kazi ya chama katka uongozi wangu tutahakikisha tunaibua vijana viongozi wapya kwa kuwajengea uwezo wa kiongozi, kuwapa nafasi kusimama na kuzungumza Mbele ya Umma wakiwa jasiri na wenye hoja nzito katika kuibua maswala mbalimbali yenye tija kwa Taifa na umma wa Watanzania.

Aidha katika ujenzi wa chama kwa kushirikiana na viongozi na wanachama wote tutakipeleka chama ardhini. kwa watanzania wazijue na wazielewe sera za chama chetu nguvu kubwa ilyopo kwenye mitandao ya kijamii sasa tutaileta mpaka ardhini chama kijulikane kwa watanzania wote.

Ndugu wanachama wenzangu nitumie nafasi hii kuwaomba mniunge mkono ili tuweze kuifikisha ACT wazalendo mbali.
Wenu...
Y.M.Masinde.
 
Back
Top Bottom