Habarini wana JF wapendwa, mimi naitwa Telesia Mdumula. Nina mume na watoto 5. Tunaishi Magomeni Dar. Mtoto wa 1 amemaliza la 7 mwaka huu na kupata `B` tunatarajia atachaguliwa kidato cha 1 mwakani. Wawili wanaingia la pili mwakani na wawili waliobaki bado wadogo sana. Mume wangu ni mlemavu wa kusikia na kwa miaka yote huko nyuma alikuwa akifanya kazi kwenye NGO moja kwa mkataba wa muda mfupi mfupi kutegemeana na uwepo wa pesa kwenye miradi aliyokuwemo.
Malipo yake hayakuwa makubwa ila ilisaidia kulipia kodi ya vyumba tulivyopanga kwa wakati, chakula, shule kwa watoto na kidogo nilimsaidia kuzungushia kwenye genge nililouza kuongezea pato.
Mwezi Juni mwaka huu wafadhili wa mradi aliokuwa akifanyakazi mme wangu walisitisha ghafla kutokana na sababu za kiuchumi. Ilibidi wafanyakazi wote waliokuwa kwenye mradi huo waondoke na kutafuta namna nyingine. Mme wangu hadi sasa anahangaikia vibarua ambavyo hata hivyo havipatikani kirahisi na vikipatikana malipo ni kidogo sana.
Baada ya hali kuwa ngumu sana ilibidi tutafute vyumba vya kodi nafuu bondeni tulipata viwili vya elfu 40@,tuliweza kulipa miezi 3 ila mwezi wa 9 kodi ilipoisha tukawa tumekwama kabisa.
Hadi sasa mwenye nyumba anataka tuondoke maana tumeshindwa kulipa kodi yake na nyumba yake ni ya biashara ili apate pesa ya kusomesha wanae shule za kulipia. Hapa tunapoishi bado si salama kwa mafuriko na wakati wowote tunaweza kubomolewa ila hatuna namna nyingine kabisa.
Maisha yamekuwa ya kubahatisha sana tukitegemea genge ambalo nalo halina mtaji na kodi yake ya miezi 6 sh. 180,000 imeisha mwezi uliopita na hatujui tutaipataje.
Tumekuwa tukiishi kwa mlo mmoja tu kwa siku na mara nyingi tumekuwa tukishinda na kulala njaa na watoto. Tumejaribu kutafuta mkopo ila tumekwama kwa kukosa vitu vinavyokubalika kwenye dhamana. Hata vitu vyetu vidogo vya ndani tumejaribu kuuza tupate hela kidogo ya kula na kununua vitu vya kuuza gengeni ila hatupati watu wa kununua. Sasa hivi tumeamua tuuze kitanda cha watoto lakini hatuoni mteja hata mmoja.
Mateso tunayopitia na watoto ni makubwa sana japo hatujakata tamaa. Ninaomba sana wasamalia wema humu JF watusaidie niweze kupata na kulipia kodi ya vyumba 2@40,000 sh. 480,000, kodi ya genge kwa miezi 6@30,000 sh. 180,000 na mtaji wa genge sh. 150,000. Yeyote anayetaka kuona na kuhakikisha mazingira ninayoishi na wanangu anakaribishwa sana.
Namuomba sana Mungu awabariki wote watakaoguswa na tatizo linalonikabili na wanangu pia Mungu awabariki zaidi watakaonisaidia. Shukrani kwenu wote. Namba yangu ya simu ni 0715597591.