Natangaza rasmi dhamira ya kugombea Ubunge 2010

Kazana bwana Mnyika jihadhari na watu kama GAME THEORY ambao wanahoji elimu yako kuwa una Zero. mtu wao Zitto kabwe ana elimu gani?
 
Rufiji,
I may be wrong lakini nahisi ni njama za CCM kupunguza makali ya viti wanavyotarajia kupoteza. Kwa mfano, kama kuna majimbo 30 ya uchaguzi na sasa yameongezeka kufikia hamsini kama walikuwa wapoteze viti 20 sasa wanadhani watakuwa bado na viti 30 ka hiyo figuratively and psychologically wataonekana kuwa hawajapoteza viti vingi.
 
Nakutakia kila la kheri katika hii safari muhimu mkuu!! Siku moja haya yote yatakwisha, na tutakuwa watu huru tena!!
 
Kijana you are good. How I wish ungegombea kwa tiketi ya CCM na siyo CHADEMA chama cha kabila lako. Hutashinda bwana mdogo.Hamia CCM. CCM and not CCJ!!Please
 
Hongera sana Mnyika kwa uamuzi uliamua kuuchukua, tunahitaji viongozi wenye Moyo na Mapenzi mema na nchi hii, viongozi wenye tija na fikira mbadala za kubadilisha maisha wa watanzania, kiongozi mwenye upeo wa kujua nini anafanya na ni outcome zake, kiongozi anayekubali kukosolewa na wala si kiongozi JINA KAMA WALIVYO WENGI.

Nchi hii inahitaji mabadiliko ya haraka sana kiutendaji kuanzia chini mpaka juu, tupo pamoja katika hili.
 
Ugumu wa Dar ni wizi wa kura sasa ni kujipanga tu vizuri.
 
Mnyika,kwanini usingejaribu mikoani?Maana Dar pagumu pale.
Ni ushauri tu mkuu

P53,

Nashukuru kwa ushauri wako lakini tayari nimeshafanya maamuzi ya kugombea ndani ya Dsm. Kwa nini unadhani pagumu?

JJ
 
Asante wote kwa shukrani na kuunga mkono dhamira husika. Nawatakieni heri.

JJ
 
i hope umejiandaa kuzuia yaliyotokea last time, we know ulishinda, nakumbuka i was still at udsm, over there almost everybody voted for you and you were leading in many polling stations ila mwishoni wakamtangaza yule mzee, nadhan walipika sana zile data ndio maana jimbo la ubungo likawa kati ya yale ya mwishomwisho kutolewa matokeo wakati dsm majimbo yote majibu yalitoka mapema! naomba ujipange zaidi kuhusu hujuma kuliko kpigiwa kura, that is your greatest enemy!
 
Mnyika Hongera sana kwa uamuzi huo Muhimu,

Utatukuta sisi wengine huko Kimara Mwisho, watu wananjaa ya Mabadiliko!
 
Hongera nakupongeza kwa hili ila naomba kukuuliza jamaa zangu waswahili wenzangu wa Mburahati na Manzese utawasaidia vipi?nadhani umelielewa swali langu kama kuna uzito nitumie kwenye PM.
 
Kaka Mnyika,
Nia unayo, uwezo unao,sababu unayo na imani yetu unayo. Tulikuwa nyuma yako 2005 na tutakuwa nyma yako tena. Wewe ni nyota ya jaa katika mazingira yetu ya leo ya upotofu wa maadili na siasa za ubinafsi.
Safari yako tunaijua, imeanzia mbali na hapana shaka kuwa itaishia mbali zaidi.
Nakutakia kila la kheri.
 
Kikubwa cha kufanya sasa hivi ni kuwahamsisha vijana wa Ubungo wajiandikishe kwa wingi.
Mi kadi yangu tayari ipo kibindoni nasubili kipyenga.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…