nyamakonge
JF-Expert Member
- May 28, 2013
- 363
- 130
Dr. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria
Saturday, 14 December 2013 ·
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.
"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.
Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.
Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.
Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.
"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.
wakuu nachukua fursa hii,kutangaza rasmi kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo.NIA yangu hii ya dhati inafuatia utafiti mkubwa nilofanya kwa vyama mbalimbali vya siasa hapa nchini.MUNGU NISAIDIE KATIKA HARAKATI HIZI.nyamakonge o nyamakonge.
tatizo unaandika ukiwa na msukumo wa kimahaba zaidi pasipo kufanya utafit, jirani zetu wa uganda pombe aina ya gongo (kwao wanaiita waraji) ni halali kabisa,huku kwetu bukoba /karagwe waraji japo serikali inaiita haramu polis,viongozi wa vijiji,kata,madiwan wabunge na wananchi kwa ujumla ndo kinywaji chetu cha kawaida.na inatengenezwa kwa uwazi mchana kweupe na viongoz wa vijiji na kata kama kawaUtawala wa chadema na itakavyokuwa tanzania. God forbid.
WanaJF,
Ikitokea watanzania tumechagua chama cha CHADEMA kutuongoza katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo mwaka 2015, haya ndio yatakayo tokea ama hakika:
1. Serikali ya CHADEMA ndio itakuwa serikali pekee duniani kote kuruhusu kinywaji haramu aina ya GONGO kutumiwa na watu wake kwa kisingizio cha mapato ya serikali yataongezeka.
2. Seikali ya CHADEMA itafanya TANZANIA kuonekana nchi ya magoigoi, wazembe na vilaza hiyo ni kutokana na aina ya viongozi tutakao kuwa nao. Mfano ni: Lema, Sugu, Msigwa na Mbowe.
3. Kutokana na kukosa ubunifu wa vyanzo vya mapato vya serikali itakayokuwa madarakani (CDM), Watanzania tutarajie nchi yetu kuwa na madanguro (chanzo cha mapato ya serikali ya CHADEMA) na mambo mengineyo ya aina hiyo.
4. Kutokana na uhusiano mzuri kati ya CHADEMA na vyama vinavyo tetea ushoga duniani. Watanzania tutarajie nchi yetu kuwa na sheria ma sera za kutetea na kupigania mashoga.
5. Kutokana na kukosekana kwa uvumilivu na ustahimilivu wa kisiasa kati ya viongozi wa CHADEMA, Watanzania tutarajie mapigano makali kati yetu na nchi za jirani.
wakuu nachukua fursa hii,kutangaza rasmi kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo.NIA yangu hii ya dhati inafuatia utafiti mkubwa nilofanya kwa vyama mbalimbali vya siasa hapa nchini.MUNGU NISAIDIE KATIKA HARAKATI HIZI.nyamakonge o nyamakonge.
Mwigulu nchemba amlipua mbowe bungeni mda huu, ni kuhusu kumkataza joyce mukya kufanya kazi za kibunge alizopokea posho badala yake aende dubai "kwa kazi maalumu"
kwamba habari zilizotawala vichwa vya habari leo vimelichafua bunge isivyo halali badala yake mbowe ashughulikiwe kama mbunge binafsi.
Tazama video hapa chini.