Natamani sana Siku moja Rais Samia Suluhu nae azisikie hizi nyimbo za Singeli na 'Matusi' yao kisha amalizane rasmi na BASATA

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Nimetoka Kusikiliza Nyimbo za Wasanii Wakubwa Watatu wa ' Singeli " hapa Tanzania nikajuta hata kwanini nilifungulia hiyo Redio ambayo TCRA nao wana Wajibu wa Kuisimamia.

Maudhui ya Kimatusi ya Msanii
A

"Umo Umo akipanua tu Wewe ingiza Chuma cheusi Moto uwake "

Maudhui ya Kimatusi ya Msanii B

"Oyayaaa Ndizi Tamu ikikatikia ndani ya Mdomo mpana na Mlaini "

Maudhui ya Kimatusi ya Msanii C

"Raha ya Flashi ichomekwe vizuri katika tobo na ikatikie kwa ndani "

BASATA sioni sababu ya Kuwafungia Wasanii Wakweli kama Dudu Baya au kuwaonya Wawazi akina Afande Sele huku hawa wa hizi Nyimbo za ' Singeli ' mkiwaacha, mkiwachekea na mkiwadekeza pia.

Na sijui TCRA mpo wapi hadi mnaviachia hivi Vyombo vya Habari ( hasa Redio ) Maarufu hapa Mkoani Dar es Salaam zinapiga ( tena wazi wazi ) kabisa hizi Nyimbo ambazo zote zimejaa Tafsiri ya Matusi tupu yenye Athari Kubwa kwa Watoto wetu na Vizazi vijavyo.

Natamani sana Siku Moja tu Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan nae kwa bahati mbaya tu akiwa Kwake Ikulu azisikie hizi Nyimbo za Matusi za hawa Wasanii wenu wa ' Singeli ' kisha aweze Kuwazingua kama nyie aliowapa dhamana ya Udhibiti mlivyomzingua labda mtaelewa.
 
Mjifunze kuishi kwa nyakati. Tupo mwaka 2021 lkn unataka kuishi maisha ya 1960.
Nitajie maneno ya matusi hapo? Km akili yako inafanya kazi?
Kumbuka tupo katika ulimwengu wa chaguzi. Unachagua kitu gani kinakufaa. Sasa ww unataka usikilize kila nyimbo?
Sikiliza nyimbo za dini zitakufaa zaidi
Tafuta video ya Anaconda by Nick Minaji na Press ya Card B, uone.
 
Unajua maneno ya matusi? Ngoja nikupe mfano ya nyimbo ya Zuchu
Baba chanja x3 ehhh
Jibusti na karanga kisha shushia na kitumbua.
Hapo unafikiri unaweza kuifungia nyimbo yake kwa kuimba matusi? Na Sheria gani utaitumia?
Zamani wakoloni walikuwa wanafungia sana kazi za wasanii zenye lengo la kumkomboa Mwafrika kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni kwasababu walikuwa wanatoa maana ya moja kwa moja. Baada ya kuona hilo wakawa wanatumia maneno yaliyojaa ubunifu wa kisanii yenye tafsida na kutengeneza maneno mapya yenye maana mpya. Vitabu kama Kusadikika, Nagona, Mzingile, Kasri ya Mwinyi Fuadi na Mashairi ya chekacheka.
Karanga ni tusi?
Kitumbua ni tusi?
Hao wasanii wa singeli utawafungia kwa ubabe na siyo kwa sheria. Hapo hata ungekuwa ni kiongozi wa BASATA utababaika tu.
Interpretation yako wewe ni ipi?
 
Nimetoka Kusikiliza Nyimbo za Wasanii Wakubwa Watatu wa ' Singeli " hapa Tanzania nikajuta hata kwanini nilifungulia hiyo Redio ambayo TCRA nao wana Wajibu wa Kuisimamia.

Maudhui ya Kimatusi ya Msanii
A

"Umo Umo akipanua tu Wewe ingiza Chuma cheusi Moto uwake "

Maudhui ya Kimatusi ya Msanii B

"Oyayaaa Ndizi Tamu ikikatikia ndani ya Mdomo mpana na Mlaini "

Maudhui ya Kimatusi ya Msanii C

"Raha ya Flashi ichomekwe vizuri katika tobo na ikatikie kwa ndani "

BASATA sioni sababu ya Kuwafungia Wasanii Wakweli kama Dudu Baya au kuwaonya Wawazi akina Afande Sele huku hawa wa hizi Nyimbo za ' Singeli ' mkiwaacha, mkiwachekea na mkiwadekeza pia.

Na sijui TCRA mpo wapi hadi mnaviachia hivi Vyombo vya Habari ( hasa Redio ) Maarufu hapa Mkoani Dar es Salaam zinapiga ( tena wazi wazi ) kabisa hizi Nyimbo ambazo zote zimejaa Tafsiri ya Matusi tupu yenye Athari Kubwa kwa Watoto wetu na Vizazi vijavyo.

Natamani sana Siku Moja tu Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan nae kwa bahati mbaya tu akiwa Kwake Ikulu azisikie hizi Nyimbo za Matusi za hawa Wasanii wenu wa ' Singeli ' kisha aweze Kuwazingua kama nyie aliowapa dhamana ya Udhibiti mlivyomzingua labda mtaelewa.
Kama huzipendi unafuata nini kule zinakopigwa. Kila mtu alee watoto wake, kama unashindwa kuwakataza watoto wako, siyop kazi ya serkali kukulelea. Siku hizi mziki ukitoka tayari uko Youtube, na ukiishaingia huko hakuna njia atatumiaSSH kuondoa.
 
Back
Top Bottom