Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,116
- 8,662
Hii tabia kila siku nailaani sana hasa nikiwa nimebaki peke yangu. Pamoja na kuwa na wanawake wenye sifa lkn bado hii tabia inanisumbua sana. Hivi sasa shetani kaniongoza katika wanawake wenye rangi nyeusi. Yaani nikiwa hata out basi akipita mwanamke mwenye hii rangi basi nahisi kama nimekatwa na wembe kifuani na hujikaza tu kisabuni ili nisionekane mbele ya wandani wangu kuwa sijatulia. Situmii pombe wala kilevi chochote sasa rafiki yangu muovu huniambia hii ndo ina replace pombe hivyo nisijilaumu!!! Naongea haya kwa machungu na kama madawa ya kulevya huwa yana tabia kama hii basi ni kazi ngumu kweli kuacha.
Mbaya zaidi hata nikipata mwanamke wa rangi hii huwa sioni tofauti yeyote na hawa nilionao. (White African skin). Nimeshanusurika kukamatwa nikiwa katika harakati za kutongoza mwanamke wa rangi hii tena nikiwa ng'ambo (assume mtu amekupokea,anakulisha,anakupatia mahitaji yako ya nje na ndani ya mwili na anakulipa mshahara) lakini bado unataka kumzunguka kufanya ushetani!!! Naamini kuna wachangiaji mtaniponda na kuniona mtu wa hovyo lkn mimi naamini shetani ashaniteka na niko kwenye maombi aniachie nimpendezeshe mungu aliyeniumba kwani najua hatima yake haitakuwa njema kwangu na future ya maisha yangu.