Natamani Rais Magufuli atoe tamko hili

fite fite

Senior Member
Feb 27, 2017
113
225
Leo ngoja niseme kitu kinachoniumiza sana hata nikinyakuliwa niwe nimetoa langu la moyoni, ambacho natamani Sana MH. Rais JP Magufuli alitoe Kama tamko na bungeni sheria itungwe kabisa ili kusimamia kisawa sawa.

Watoto wa viongozi wa serikali tusome nao shule zetu za serikali (kata).

Najua wengi mtanielewa vibaya haswa pale nitakapo kugusa lakini ukweli ndio huo ili kuweza kuweka usawa.

Mfano:
mtoto wa waziri wa tamisemi asome shule ya msingi Gongo la Mboto.

Mtoto wa Waziri wa Fedha asome shule ya msingi Buhigwe

Tuone Kama kutakuwa na uhaba wa walimu, Nyumba za watumishi, madawati na vitabu vya kiada mashuleni

Maana tuliowapati dhamana ya kusimamia kwa niaba yetu wao watoto wao wanasoma shule zinazojitosheleza hata tukilalamika kero zetu haziwaumizi wao kwa kuwa watoto wao hawapo shule zenye kero rukuki.

Faida za tamko Hilo au sheria

1. Tabaka la walioshika mpini na walioshika mkali litapungua sana.

2. Miundo mbinu ya shule za kata itaboreshwa kwa kiwango kizuri.

3. Viongozi wa serikali watakuwa na uchungu na shule hizi watajali, watawasikiliza walimu na kutatua keep zao.

4. Usalama utaimarishwa sana maeneo ya shule zote serikali

5. Ufaulu utaongezeka Sana maana viongozi hawatakubali watoto wao wasome shule ambayo Ina uhaba wa walimu, madawati, matundu ya vyoo, vitabu.

6. Wanafunzi hawataonewa kwa kufutiwa mitihani yao wakati kosa sio la kwao.

7. Usawa utakuwepo.


Faida nyingine mtaongezea wadau. Ila tamani Sana itokee hivyo natamani Sana yaani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom