Natamani niwe na miradi yangu binafsi

Natamani niwe na miradi yangu binafsi

Bill of Quantity

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
1,233
Reaction score
407
Habari zenu wana JF?

Mimi ni mwanachuo, nategemea kuhitimu masomo yangu mwezi July mwaka huu.

Binafsi nimekuwa na ndoto za muda mrefu za kuja kumiliki miradi yangu binafsi ambayo angalau iniingizie 'net profit' kuanzia angalau USD 6000 kwa mwezi.

wadau, umri wangu sasa ni miaka 24, nawategemea sana ninyi kama ndugu zangu, kaka zangu wa karibu, mama na baba zangu, mnipe japo ABC's za kuingilia uraiani ili nitimize ndoto zangu.

Najua kuingia huko kwenye private employment kunahitaji starting capital, hapa nilipo sina pesa za kutosha! niseme ukweli.

Nahitimu masomo nikiwa na passion ya biashara hasa hasa katika field za logistics and transportation.

Mdau mmoja kanishauri nitafute ajira kwanza kwenye field hii kabla sijajiari, bado nawaza na kuwazua.

Wadau nipeni maoni yenu na ushauri.

Shukrani sana.
 
Habari zenu wana JF?
Mimi ni mwanachuo, nategemea kuhitimu masomo yangu mwezi July mwaka huu.
Binafsi nimekuwa na ndoto za muda mrefu za kuja kumiliki miradi yangu binafsi ambayo angalau iniingizie 'net profit' kuanzia angalau USD 6000 kwa mwezi.
wadau, umri wangu sasa ni miaka 24, nawategemea sana ninyi kama ndugu zangu, kaka zangu wa karibu, mama na baba zangu, mnipe japo ABC's za kuingilia uraiani ili nitimize ndoto zangu.
Najua kuingia huko kwenye private employment kunahitaji starting capital, hapa nilipo sina pesa za kutosha! niseme ukweli...
Nahitimu masomo nikiwa na passion ya biashara hasa hasa katika field za logistics and transportation.
Mdau mmoja kanishauri nitafute ajira kwanza kwenye field hii kabla sijajiari, bado nawaza na kuwazua.
Wadau nipeni maoni yenu na ushauri.
shukrani sana..

Ni muhimu kuwa na ndoto si jambo baya,lakini angalia hivyo vitu unavyovitsks je ni "realistic".Angalia red highlighted hapo juu,aliyekushauri walau kufanya akzi kwa muda katika field unayotaka kuwekeza amekushauri jambo jema.Ni muhimu uijue biashara unayotaka kuifanya na si kuingia kwa "theory" tu ambazo hazina changamoto zaidi ya mabadiliko ya mawazo yako.
Unataka Usd 6000 kwa mwezi i.e 6000x2000=Tsh12,000,000 hii kuwa net profit si kitu kidogo unakazi kubwa ya kufanya.Sijajua famil;lia yeni ikoje au unategemenea vipi kupata hiyo "starting" capital.Kama umekuwa na hii ndotio kaa chini uchanganue utaifikia vipi.Hapa na sisi tuna ndoto zetu na wakati unaota hatukuwepo sasa usitutegemee sana tukufumbulie kila kitu,wewe binafsi unakazi kubwa ya kufanya.Ushauri wangu tafuta mtu amabaye tayari yuko katika hiyo business pata ushauri kutoka kwake ni bora zaidi kuliko ushauri kutoka kwa mtu yeyote tena mwingine hata hajui changamoto za hiyo biashara.
 
kaka yani unaomba ushauri uraiani kwa watu wasio na elimu tena?.,wewe elimu yako imekusaidiaje?...wasomi wa siku hzi bhana
 
kaka yani unaomba ushauri uraiani kwa watu wasio na elimu tena?.,wewe elimu yako imekusaidiaje?...wasomi wa siku hzi bhana

Mkuu ...kwani mtu asiyesoma lakini ana biashara zake za siku nyingi na yuko kwenye the same field hawezi toa ushauri....??? Au unazani ushauri lazima utoke kwa msomi tu!??
 
Ni muhimu kuanza kujifunza kazi kwanza kabla ya kujiajiri mwenyewe.…tafuta sehemh upige kibarau kama ulivoshauriwa ila wakati unapiga kazi anza kufungua miradi yako kidogokidogo, leo unanunua mikokoteni unaanza kukodishia watu, kesho unanunua pikipiki unamwajiri mtu, kesho kutwa taxi, kesho yake daladala…mpaka mwisho wa siku unajikuta na mascania kibao. It takes time and is not simple as u think. Jiandae mapema kukutana na changamoto zozote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom