Natamani ningekuwa Mbunge mwanamke na Mjumbe wa NEC

Fiber Organ

New Member
Jan 24, 2020
4
3
Natamani ningekuwa mbunge wa kike na Mjumbe wa NEC ya CCM ningemshawishi kwanza Spika wa Bunge amwite Mwenyekiti wetu kwenye kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM tuzungumze naye na kumshauri kwamba suala la mtoto aliyepata ujauzito akiwa shule kuendelea na masomo ni sera ya chama chetu na tuliiweka kwenye ilani ya chama chetu ya Mwaka 2015 na kuinadi kila ilipowezekana.

Aidha, katika kikao chetu cha Mwanza cha NEC, pamoja na kumpongeza Mwenyekiti wetu kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, kwa heshima na taadhima ningemkumbusha suala la shule kwa watoto waliopata ujauzito kwamba hili sio tu halijatekelezwa bali, umelizuia kabisa, kitu ambacho Mimi kama mwakilishi wao kwenye Bunge na NEC naona kama ni usalitii kwao.

Ningejisikia vibaya watu kama Zitto ati kuwa mtetezi wa haki ya wasichana kupata elimu. Ningeona aibu ati Benki ya Dunia wanazuia msaada kwa nchi nami bado niko bungeni, kisa, elimu kwa wasichana bila ubaguzi.

Ningemwambia Mwenyekiti, sababu kubwa ya kuomba kuongezewa nafasi ya uwakilishi kwa wanawake Bungeni na kwenye Chama ni kuongeza sauti za utetezi wa wanawake ndani ya vyombo hivi adhimu na si vinginevyo.

Ningemwambia kama akina Zitto wanaweza kuwa watetezi wa wanawake kupata elimu hakuna haja, basi ya sisi wanawake kujazana Bungeni na kwenye NEC ilhali akina Zitto wanatosha. Tungefanya kampeni ya kuwa na akina Zitto wengi zaidi Bungeni na kwenye NEC.

Nadhani Mwenyekiti wangu angenielewa kwa sababu kwanza si sera ya chama chetu.
 
Anza kazi ya kumsifia mwenyekiti wetu ,this year ni election you never know utapata tuu
 
Back
Top Bottom