Natamani mtoto, nisaidieni

Mpole mimi

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2014
Posts
315
Reaction score
104
Habari, Nina imani kila mwanamke anapenda kuitwa mama na mwanaume anapenda kuitwa baba kwakuwa ni jambo la kheri nina imani pia sijakosea kulileta hapa.
Jf ni mjumuiko wa watu wengi na wenye elimu na uelewa tofauti...Mimi ni mwanamke..na sasa nataman kuitwa mama..sina mtoto wala sijashika mimba bado.ila mungu akijalia ningependa iwe mwezi Huu.

Msaada hapa!
Ninaenda siku zangu siku tatu ya nne ni vitone vidogo tu...mfano kama nimeanza tarehe 05.01 namaliza tarehe 07.01...
Ni vipi hapo nitaweza kuhesabu siku zangu vizuri nikadaka mimba siku ya hatari? Na ni ipi iyo siku ya hatari?

Na pia kwa wenye ufahamu zaid juu ya watoto pacha.. Napenda na natamani sana kujaliwa hao.
Asanteni.
 
samahani una umri gani kwani?
 
nina 25 nipo kwenye Mahusiano lakini sijaolewa bado. Nisaidie hapo juu kwa uelewa wako
asante kwa jibu lako,kwani umekua katika uhusiano kwa muda gani,na umekua ukizuia mimba ama una tatizo la kushika mimba?
 
asante kwa jibu lako,kwani umekua katika uhusiano kwa muda gani,na umekua ukizuia mimba ama una tatizo la kushika mimba?

Miaka miwili sasa ..swala la mtoto limeanza mwez uliopita ndo mpaka sasa. Sina tatizo la kushika mimba
 
tatizo hujaolewa unazini!! ungekuwa umeolewa ningekusaidia.

Hapo mutant inamaana kubwa tuu, inawezekana huyo jamaa kwa kuwa ajakuoa, hivyo huna imani nae, Kwahiyo umekuwa ukitumia njia mbalimbali kuzuia usipate mimba, hivyo yawezekana hizo njia zishakusababishia athari, ebu kwanza mwambie akuoe ili uwe huru, jiachie, baadae kitanasa tu.
 

haujatwambia Cycle yako siku ngapi?

Ni siku 21,28 au 35?

Ukitupa hapo tutakupa zile siku za hatari uweze kudaka mimba vizuri...

Kuhusu swala la mapacha sio jambo dogo I see...

Mapacha mara nyingi utawapa iwapo unatumia fertility drugs kabla ya kupata ujauzito na wakati mwingine utapata watoto mapacha iwapo labda katika familia yenu kuna kitu cha hivo....vinginevyo mapacha sio cha mtoto kuwapata
 

Cycle yangu ni 28 . ni zipi fertility drugs? And yes kuna pacha kwenye familia yetu
 
Cycle yangu ni 28 . ni zipi fertility drugs? And yes kuna pacha kwenye familia yetu


Kama cycle yako ni siku 28 hesabu siku kumi na tano nyuma.

1,2,3,4,5,6,7,8,9,10,11,12,13,14,15,16,17,18,19,20,21,22,23,24,25,26,27,28

Kwa hiyo siku ya kumi na nne ndio siku yenyewe.
 
Ah basi kuna mtu alinielekeza nianze kuhesabu siku ya kwanza pale napomaliza period yaan kama nimeanza juzi basi leo kesho ndo nahesabu moja mpaka 14 ndo siku yenyewe kumbe ninaanza moja tangu siku nayoanza bleed?!.
 
Kujua cku zako za hatari, download my period calendar
 
Tangu siku ya kwanza unapoanza period hesabu moja.. ikifika 13, 14, 15.. hizi ndizo siku hatari..
Bt hasa ya kumi na nne..

Wewe Mpole mimi chukua huu ushauri ni hakika kwa asilimia 100 na ni rahisi ku count. Ongeza na hili....Mbegu za mwanaume zinaweza kukaa kwa saa 72 zikiwa hai kwa hiyo unaweza fanya tendo la ndoa siku ya 10 au 11 na ukapata ujauzito kwani zitakutana na yai katika siku ya 13 au 14.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…