kui Iko siku utanielewa tu, mimi kwa kweli huwa sipendezwi na nchi yenu kuwa nyuma, kila nikija Bongo huwa naziona fursa nyingi sana ambazo nyie mumeziacha wazi na kulalamikia serikali kila siku. Wakenya wengi huwa tukija tunazichangamkia na kusepa. Nchi yenu imebarikiwa pakubwa na kila kitu, ila kwa utendaji mpo nyuma sana.
Unakuta Mtanzania analalamika eti rais Kikwete kawadanganya kuhusu maisha bora kwa kila Mtanzania ambayo hayapo, ila Mkenya akija huwa anaona hiyo fursa ya maisha bora kwa kila mtu na anaichangamkia. Serikali haiwezi kukuwekea chakula mezani, ni jukumu lako wewe kujipikia na kujipakulia. Kwetu Kenya tunafunzwa jinsi ya kuwa mgomvi (aggressive) tangu utotoni, tungelegea kama nyie yaani tungekufa zamani maana nchi yetu asilimia 80% ni kame tupu na hailimiki.
Wabongo mmezoea nyimbo na vijisababu vya uswahilini, mara eti IDD Amin, Kegara war iliwafanya mlegee, Tanzania potential, Wazungu waliwasaidia Wakenya n.k. Ngonjera na utepetevu mwingi tu, kama ni ufisadi hata sisi tunao, kama ni uongozi mbaya hata kwetu ndio usipime.