Ni kweli lazima ujikane mwenyewe na kumfuata Yesu.
Lakini, kumbuka tu viumbe dhaifu.
Na mara nyingi tunaanguka majaribuni hata kwa wale waliosimama katika imani kwa muda mrefu.
Kwa huyu anayeanza kumbuka pombe/bar ilikuwa na mtindo wa maisha yake.
Sitegemei ani rahisi kwake kuacha kwa siku moja
anahitaji muda na anaweza akaanguka mara kadhaa
kikubwa ni kujua umenagua wapi na vipi ili uweze kusimama katika imani tena.
Mfano mzuri tunauona kwa safari ya Yesu kuelekea Calvary
haikuwa rahisi
alianguka mara tatu
lakini hakuacha kutimiza jukumu lake la ukombozi
na hata wakati mwingine
tunahitaji msaada kwa watu wanaotuzunguka kufikia malengo yetu ya kiimani
tunaona Yesu ilibidi kusaidiwa ya Simon wa kirene
kukamilisha safari yake
mtoa mada,
unajua unachokisikia moyoni mwako
sisi binadamu si lolote hata tukukatisha tamaa
Yesu akasema "kila anayetaka kunifuata ajikane mwenyewe kisha abebe msalaba wake anifuate". Kama kweli umeamua kumpokea Yesu maishani mwako amua hili "msiipende dunia na mambo yake, maana apendaye dunia kumpenda baba hakumo ndani yake". Lakini sehemu nyingine anasema "mtu hawezi kutumikia mabwana wawili maana atampenda mmoja na kumchukia mwingine. Kwa hiyo amua kutumikia pombe au Yesu, na sio kuchanganya.