Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Nawaona raia wengi wakifurahi na kushangilia maisha waishiyo kwenye nchi ya peponi na mimi natamani niishi mahali hapo lakini nikiwauliza walifikaje hapo wanasema tulikufa ndo nakata tamaa maana siko tayari kufa japo naipenda pepo.
Kiongozi wa nchi ya peponi anakurupuka sana kama tumbo la kuhara hataki kufuata sheria, ni katili kama nyoka anayengata na kumuua mtu wakati hawana uwezo wa kumla. Kuwanyanyasa wengine kwake ni sifa kuu ya kuongoza.
Hii nchi ya peponi imegeuka na kuwa nchi ya ardhi au kama ile ya msituni ambapo simba na chui wamejipa uhalali wa kuwatoa roho digidigi utadhani ndo sheria za mbuga. Hii ni hatari, matendo yao haramu wanataka tuyashangilie.
Nimelikumbuka hili, ni juzi juzi tu nilinunua tofali zangu 2500 nikatumia 1000, zikabaki 1500 ambazo sijui matumizi yake. Mtu mmoja anasema eti tofali zimeibiwa mimi nasema tofali zangu zipo japo hazionekani.
Enyi askari wa nchi ya peponi muishiyo Wilaya ya kushoto kamateni raia wote waishiyo Wilaya ya kulia maana naona wananichafulia serikali yangu ya nchi ya peponi kwani wanahojihoji zilipo tofali zangu 1500 hii haiwezi kukubalika na huo ni uchochezi.
Siku hizi hawa raia wanapingana na ukweli wakati imeandikwa tena kwenye ukurasa fulani kuwa tofali hizi hazionekani na mimi nasema hakuna aliyeziiba maana nimeambiwa kuwa nchi ya peponi haina wezi. Sasa najiuliza hii tabia inatoka wapi ya kusema giza ni giza badala ya kusema giza ni nuru na nuru ni giza?? Mimi sikubali lazima hawa raia niwakamate kwa uchochezi wao.
Ninao watoto watu wanasoma shule ya msingi Juu. Watoto 2 Kati ya hao 3 mmoja ni WANASABA na wawili nawalea tu. Wote walipewa Mitihani wakafanya na matokeo yalipotoka wote walipata ziro baada ya kupata matokeo nikaamua kuchukua hatua. Niliwaachisha shule wale wawili lakini huyu mmoja nimemuacha kwani nilikumbuka kuwa ni mtoto wanasaba na pia mkumbuke "damu ni nzito kuliko maji".
Sasa navitaka vyombo vya dola hili ikiwemo UHAMIAJI kuwahoji wale wote wanaohoji zilipo tofali 1500 maana nahisi hao watakuwa sio raia wa nchi ya peponi kwa jinsi wanavyohojihoji.