Natamani kufanya kazi Ikulu

Natamani kufanya kazi Ikulu

mkuu ninajaribu kupakua hiki kitabu lakini ninapata jibu hili 'You do not have permission to view this page or perform this action'. shida yaweza kua nini?

Uzi utakuwa umefutwa mkuu
 
mkuu ninajaribu kupakua hiki kitabu lakini ninapata jibu hili 'You do not have permission to view this page or perform this action'. shida yaweza kua nini?
Nipm email yako nikutumie km hutojali
 
Waafrika hasa sisi watanganyika hatuna utaratibu wa kuandika wala kusoma.

Viongozi wenyewe hawasomi chochote, wengi hata ukiwasikiliza tu unajua kichwani hamna kitu, wapate muda wa kuandika sangapi

Viongozi wachache amabao wanajipambanua kama wasomaji hata wakiongea unaweza kuwasikiliza, aghalabu wanaweza kujenga hoja, Prof. Mwandosya, ZZK, J. Makamba ni wasomaji na waandishi wazuri

Kuna mambo mengi tungejifunza kama tungekua na utaratibu wa kuandika vitabu na mengi tunapoteza kwa kutoandika vitabu.

Sijasoma Fire and Fury japo nimekutana nacho mara kadhaa labda sababu sivutiwi na siasa sana hasa za Marekani.
 
Ikulu huwezi enda kufanya kazi kwa kusoma vitabu vya hadthi za maisha ya watu huo umbeya.

Hivyo vitabu ulivyosoma havilingani na mazingira ya Tanzania ya siasa

Mleta mada huijui Tanzania inavyoandaa maraisi.CCM system yake huandaa maraisi kwa siri na kuwaficha.Huwezi wajua mpaka kule Dodoma ila wenyewe hujijua na hutakiwa kuficha hiyo siri ili wanga wasije wawangia mapema.Ndivyo mwinyi alivyopatikana,Mkapa alivyopatikana,na Kikwete ndivyo alivyopatikana wakati kipindi chake Mrema ndie alikuwa maarufu watu wakajua mrema atashika ikapigwa chenga ya nguvu kikwete akapewa.Kipindi cha Magufuli Lowasa alikuwa maarufu lakini alijiandaa kuwa raisi hakuandaliwa kuwa Raisi ndio kosa lake kubwa.Kukaa kote CCM alidhani uraisi mtu unajiandaa mwenyewe kumbe unaandaliwa.Magufuli hakuwa na makeke alitulia tuli sababu toka siku nyingi aliandaliwa ghafla kaibuka huyo kawabwaga wote waliokuwa wamejiandaa kuwa maraisi badala ya kuandaliwa.Mgombea uraisi baada ya Magufuli kuondoka ni siri kubwa huwezi mjua hata ni nani tofauti na CHADEMA ambako raisi hujiandaa mwenyewe tunajua ni Lowasa na Zanzibar ni Seif sharrif hamad.Kwa zanzibar CCM imeficha shein akimaliza huwezi hata kisia nani atakuwa raisi.Hiyo ndio CCM
 
Bujibuji nafarijika kuona una maneno mazuri ya biblia bila shaka ww ni mwinjilisti au mchungaji.
Mimi ni chumvi ya ulimwengu, mimi ni taa, mimi ni jiwe walilolikataa waashi, mimi ni mwamba , mimi ni chapa yake KRISTO
Wagalatia : Mlango 6

17 Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.

 
Natamani kufanya kazi Ikulu!

Jana nimeanza kusoma kitabu cha "FIRE AND FURY", pamoja na kwamba sijamaliza kusoma, kimenivutia sana. Mwaka juzi nilisoma kitabu cha AN ACCIDENTAL PRIME MINISTER (MANMOHAN SINGH), na baadaye nikasoma kitabu cha NARENDA MODI:THE MAN OF THE MOMENT.

Katika vitabu hivi unapata mambo ya ndani kabisa ya viongozi wa juu ambayo huwezi kuyapata katika hali ya kawaida (kwenye tv, radio, social media, newspapers), kiasi kwamba wananchi wananyimwa haki ya kujua mambo ya msingi. Mfano! JPM hakuwa mtu aliyetegemewa kushika madaraka ya juu. Hata yeye amepata kusema mara nyingi. Lakini mwisho wa siku akashinda.

Mtu angeweza kujiuliza: Nini ilikuwa sababu ya Magufuli kushinda uteuzi wa kugombea urais ndani ya chama? Baada ya hapo ,kujua team yake ya kampeni. Walijipangaje?Mikakati yao ilikuwaje?Walifanikiwa sehem gani?Wapi walishindwa?bChangamoto zipi walikutana nazo? Nini kilitokea baada JPM kushinda?

Kwanini JPM alichelewa sana kutangaza baraza la mawaziri? Je, yale ambayo alikuwa anayaamini kwamba atafanya kabla hajawa Rais, ni haya ambayo anayafanya?
Mtazamo wake kuhusu nchi na utawala kabla ya kuwa Rais bado haujabadilika? Ni changamoto zipi anazopitia katika kutimiza maono yake? Vipi wasaidizi wake wanafanya kazi sawa na anavyotaka? Anawaamini? Maswali yapo mengi sana.

Majibu yake yanaweza kutusaidia kufahamu changamoto halisi ambazo viongozi wanapitia na hivyo kuwa funzo kwa viongozi wajao. Hili jambo la kila kiongozi kufa na siri zake ni tatizo. Viongozi wajifunze kuandika. Hata kama hawawezi kuandika ,kuna watu wengi wanaweza kuandika.

Hata wasaidizi wa viongozi wanaweza kuweka kumbukumbu kwa kuandika vitabu.
Nimemfikiria Salva Rweyemamu. Nimemfikiria Gerson Msigwa. Ni mambo mangapi anayajua ambayo anaweza kuandika, sisi wengine tukajifunza. Pengine wanaogopa, kwamba wakiandika mambo "negative" watakutana na mkono wa dora.

Lakini kuna mambo mengi yanaweza kuandikwa bila kuathiri personality ya mwandishi na anayeandikwa. Ipo siku tutajaribu kuondoa mawingu.
1595710961927.png
 
Thread nzuri..fikirishi...bahati mbaya comments kicheleee.....

Aaagh ndio mwendelezo wa kutopenda kusumbua AKILI ZETU na kusoma na kuandika Kama alivyosema mtoa post na wadau wengine?!!!!

Aya bnaaaa watu wako BUSY celebrity forum...
 
Back
Top Bottom