Salama Ndugu wana JF,
NI muda sasa hatujawekana sawa juu ya uozo, Madudu yanayofanywa na viongozi wa juu wa Chadema hasa Dr.slaa, Licha ya uzuri alionao kwenye siasa za nje ya chama(kwenye majukwaa) lakini huyu ni mtawala hatari sana ndani ya chama, Na kama sekretarieti ya chama na Kamati kuu ya chama itaendelea kumfumbia macho nadhani huyu mzee si muda mrefu tutasikia pale makao makuu damu imemwagika au viongozi muhimu wameachia ngazi na hawataki tena kufanya kazi na Dr.slaa.
Naomba kuwaletea baadhi tu ya upuuzi wa Dr.slaa ambao hadi nakwenda mtandaoni hana pakuweka sura yake baada ya kutoka Kwenye kikao cha kamati kuu kilichomalizika usiku wa manane pale Mbezi garden.
1.Huwezi kuamini kama kweli huyu ndiye Dr.slaa amefanya tukio hili..Ni tukio linalo husiana na Uchaguzi wa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa uliofanyika mwaka jana ambapo Mbunge wa viti maalumu CHIKU ABWAO alishinda nafasi ile ya uchaguzi na kutambulika kama mwenyekiti wa chama mkoa wa iringa.
Lakini unajua ilikuwaje hadi limefika mezani mwa kikao cha kamati kuu?
Wakati wa uchaguzi ule wa mwenyekiti wa mkoa wa Iringa ambao Msingwa alikuwa ndiye mwenyekiti hapo awali, Chadema kupitia katibu mkuu wa chama Dr.slaa walimkopa Tsh.Million tano ndugu CHIKU ABWAO(ndivyo ilivyo wala usidout, inakuwaje chama kikope million 5 wakati kinaruzuku na misaada kibao?) kwaajili ya kusafirisha wajumbe kufika kwenye uchaguzi ule pale iringa makao makuu ya chama...
Baada ya kokopa fedha hizo kwa CHIKU ABWAO, Dr.slaa akamteua CHIKU ABWAO kuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi ule pale iringa(mwenyekiti Taifa alikuwa hajui hilo)....Wakati huohuo tena Dr.slaa akamshawishi CHIKU ABWAO kuvuta fomu ya kugombea nafasi hiyo ya uenyekiti pale iringa(kwa maana hiyo,msimamizi mkuu wa uchaguzi ule naye alikuwa mgombea wa nafasi tajwa,Unategemea nini hapo?)..Kimsingi huu ni ukiukwaji wa Demokrasia na nimambo ya kitoto ambayo Dr.slaa nayafanya na wabunge wake wa viti maalumu(sijajua kilichonyuma ya pazia)...
Mshindi wa uchaguzi ule alikuwa ni CHIKU ABWAO ambaye alikuwa ni msimamizi mkuu wa uchaguzi ule.Na Dr.slaa bila aibu akamtambua Chiku kama mwenyekiti wa mkoa wa iringa.Hii kiti imewagawa kabisa wabunge wawili wa chama kimoja(msingwa na Chiku) Msigwa analalamika imekuwaje lafu kama hii ifanywe kwa msaada wa katibu mkuu tena anayejiita Mtu makini?...
Kusema kweli kamati kuu ulishikwa na Butwaaaaa kusikia mchezo huo, Huku chiku Abwao akitumbuka macho kwa aibu ndani ya kikao kile.
Nauliza umakini wa Dr.slaa upo wapi? Anaendesha chama kihunikihuni hivi kama anaendesha kampuni yake!!!!!
2.Jambo la pili lililo onesha ni namna gani Dr,slaa hafai hata kuwa karani wa hospitali,Ni ule ugomvi wake na watendaji flani wa pale makao makuu ambapo anataka Mchumba wake Josephine apate nafasi ya kazi pale makao makuu..Hakika Dr.slaa anaugomvi mkubwa sana Na Miwgamba pamoja na Anton komu(anashughulika na mambo ya fedha pale makao makuu) amemjengea chuki,kisilani na anamuundia zengwe la kila aina ili tu Mwigamba atoke pale makao makuu.
Ndani ya kikao cha kamti kuu,Dr.slaa alitoa kali ya mwaka baada ya kusimama na kusema simtaki mwigamba na nimeshamwambia anikabidhi ripoti ya Arumeru kisha aondoke zake,Na nukuu"ndugu wajumbe unaweza kuishi na mtu miaka mitatu usijue fani yake..kumbe Mchumba wangu Josephine ni mzuri sana kwenye mambo ya IT anaweza kutusaidia kufanya kazi za kukagua fedha hapa makao makuu baada ya mwigamba kuondoka" wajumbe wakamati kuu walilipuka kwa mshangao huku wakiuliza inakuwaje Mwigamba aliyeajiriwa kwa taratibu leo anafukuzwa bila utaratibu?
Kwani wewe Dr.slaa ninani hapa? mwigamba endelea na kazi,hatutaki makahaba ndani ya chama chetu,Huyo kimada wako aishie hukohuko nyumbani kwako...walisikika wajumbe baadhi.
Kusema kweli Dr.slaa anafanya kila namana kumuingiza Mchumba wake pale makao makuu,Anajaribu kila njia,Alijaribu kumfukuza ANton komu akakwama kwa sababu ya Gazeti la mwanahalisi pili kwa sababu Mwenyekiti na Anton Komu ni maswahiba.
Mwigamba kusema kweli amekuwa msaada sana wa kuzuia upotevu wa pesa katika chaguzi mbalimbali kiasi kwamba kwenye kikao cha Sekretarieti wajumbe wote walimpongeza kwa ripoti safi ya Arumeru.
Nauliza Dr.slaa anataka kuleta mdudu gani ndani ya chama<mbona mke wa mbowe hajihusishi na mambo ya chama? Mbona Obama hamleti mke wake kwenye chama? Josephine amekupa dawa gani Dr.slaa unataka kuuua chama?
3.Kama ulikuwa hujui Dr,slaa,anaye wahi kupeleka ripoti au kesi yoyote ndiye aliyeshinda kesi kwa mijibu wa akili yake..Huwa hawezi kusikiliza pande zote mbili,yeye anahukumu bila kisikiliza..Ameshafukuza madiwani wengi kwa sababu hana utashi wa kusikiliza,Ameshafukuza Viongozi wa serikali za mitaa wengi wa chadema bila kusikiliza maoni yao.yeye anasema anaye wahi kuleta kesi ndiye mshindi.(nitawataja viongozi aliowatimua kanda ya ziwa,na sehemu mbalimbali bila kuwasikiliza..na nitawataja wale aliotunishiana nao misuli akawashindwa)nasubiri anijibu.
Mwisho naomba kuhoji UWEPO WA GODFREY LEMA kwenye kikao cha KAMATI KUU kilichomalizika jana,kimsingi ameshapoteza sifa ya kuwa mjumbe wa kamti kuu tangu alipotenguliwa ubunge..Lakini Dr.slaa ulimwita kuhudhuria kikao kama nani?
Naomba kwa leo niishie hapa,japo nina mengi sana ila "Miruzi mingi humpoteza mbwa mwelekeo" naomba tujadili haya kwanza then mengine ya ndani zaidi yatakuja.
Dr.slaa popote ulipo naomba uje ujibu hapa,kanusha madudu yako hapa!!!majibu yako yawe ya wazi na yanayoeleweka sio nusu nusu kama tulivyo kuzoea.
Mnakaribishwa mtukane,mtumie lugha mbaya...lakini mwelevu atajua ukweli wa mambo haya na atakosoa mwenendo huu wa Dr.slaa iliajirekebishe tujenge chama chetu.
By Tuntemeke...Mwakipande(mkinga halisi).