Natamani Baraza la Mawaziri la Mh. JPM lingekuwa angalao na watu 10 tu mfano wa Prof. Mbarawa

M_kara

JF-Expert Member
Jan 9, 2016
385
293
Tume Yabaini Ufisadi Mkubwa Bandari....Waziri Aagiza Wahusika Waachishwe Kazi na Wafikishwe TAKUKURU

Serikali imebaini ufisadi mkubwa ndani ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kutokana na kukamilika kwa kazi ya Tume iliyoundwa mahususi ili kuchunguza utendaji wa mamlaka hiyo, na imeagiza kuchukuliwa hatua kwa watu wote wanaotajwa kuhujumu Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alisema hayo wakati akizindua Bodi mpya ya TPA inayoongozwa na Profesa Ignas Rubaratuka jijini Dar es Salaam jana.

Akiagiza hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa wahusika waliotajwa katika ufisadi na ripoti hiyo, alisema kwanza ni baadhi kufikishwa mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na wengine kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi lakini akionya kuwa ni marufuku kwa wahusika kupewa barua za onyo.

Katika kudhihirisha kukerwa na utendaji wa TPA, Profesa Mbarawa ambaye baadaye alifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Bandari ya Dar es Salaam, aligoma kukabidhi mabegi ya kuwekea nyaraka kwa wajumbe wa Bodi mpya kwa kusema kuwa yalikuwa ni ya gharama sawa na yale yanayotumika kusafiria Ulaya.

Akizungumzia kukamilika kwa kazi ya Tume, Profesa Mbarawa alisema tume hiyo iliyowajumuisha wataalamu mbalimbali imefanya kazi kubwa ya kuchunguza utendaji wa TPA na kubaini ufisadi mkubwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya mifumo ya miundombinu kama katika mita za kupima mafuta (flow meters).

Kuhusu mita za kupimia mafuta, aliitaka bodi hiyo kuwa makini katika kusimamia utendaji kazi wa mita hizo alizosema serikali imetumia Sh bilioni 12 kuzinunua ili kuhakikisha kuwa zinafanya kazi vizuri na kwamba zinapoharibika ni lazima uamuzi wa ama kununua mpya au kuzirekebisha ufanywe haraka.

Alisema ufisadi mwingine umebainika katika miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), ambako mingi imewekwa ili kuwanufaisha watu na si serikali, mgongano mkubwa wa maslahi kwa Bodi ya Zabuni uliochangia kukwama kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo, ajira za kindugu, kulindana, mtandao wa wezi, rushwa na uwezo mdogo wa kiutendaji.

Kuhusu mgongano wa maslahi kwa Bodi ya Zabuni ya TPA, ambayo aliagiza ivunjwe mara moja na kuundwa mpya, Waziri Profesa Mbarawa alisema Bodi hiyo imekuwa ikitanguliza mbele kile alichokiita ‘ten percent’ katika kila zabuni na kukiri wazi kuwa bodi hiyo ni chanzo cha matatizo mengi ya Mamlaka ya Bandari.

Alisema kutokana na udhaifu wa Bodi hiyo ya Zabuni, huduma karibu zote zinazotolewa ndani ya TPA zinatolewa na kampuni ambazo ama ni za wafanyakazi wa mamlaka hiyo, au za waume au wake zao, na kama si hivyo basi ni za ndugu, jamaa au marafiki wa wafanyakazi, jambo linalozua mgongano mkubwa wa kimaslahi.

Kuhusu ajira, alisema ripoti imebaini viongozi wa TPA wamekuwa wakiwaingiza kazini ndugu, jamaa na marafiki zao kinyume cha taratibu za utumishi serikalini na alikwenda mbali kwa kusema kuwa TPA ilipohojiwa kuhusu kasoro hizo kupitia kwa mwanasheria wake ilisema; “hakuna tatizo,” jibu alilosema lilimpa mshituko mkubwa.

Kuhusu mazingira ya rushwa, alimuonya Mwenyekiti wa Bodi hiyo mpya kuwa macho na rushwa, akisema watu wanaohujumu utendaji wa Mamlaka ya Bandari ni watu wanaotumia ushawishi wa kiwango cha juu cha rushwa na kutoa siri kwamba wamewahi kufanya jaribio la kumhonga mjini Mwanza na Dodoma bila mafanikio.

“Ripoti imebainisha kuwa wamekuwa wakihonga hata bodi, wanawapa fedha shilingi milioni tano kwa wajumbe wa bodi na hivyo wanapoteza nguvu ya kusimamia mambo. Ikitokea hivyo kwa bodi hii, wewe ni Profesa mwenzangu kwa hiyo ngoma droo lakini nitakuwajibisha. Nitamwomba Rais akuondoe mlango ulioingilia ndio utatokea na hawa wajumbe ambao wapo katika mamlaka yangu nitawafukuza papo hapo,” alionya Mbarawa
 
Asante Magufuri si jui ulijichelewa wapi maana naona ni kma utawale milele tuu
Yaani dhamira yako ya dhati na upendo wako wa dhati ndio unao nifanya nianze kujivunia kuwa mtanzania inchi imeanza kuwa na nidhamu watu wameanza kuogopa kula hela za madili
Safisha pale bandarini kuna vilaza na vihiyo wengi nao wamejificha pale nao waondoe tuu maana ndio ajira za undugu kma mtafiti alivyosema.
Mungu akutangulie ktk kibarua hiki kigumu tukichokupa
 
NO
Police+Lugumi+by+FEDE.jpg
downloadfile-17.jpeg

swissme
 
Wapo wengi wa aina ya Mbarawa. Wanafanya kimyakimya kunyoosha baada ya wabunge wa upinzani kupiga kelele juu ya utumbuaji majipu. Kurekebisha mfumo ni kazi kubwa na si lele mama
 
Tume Yabaini Ufisadi Mkubwa Bandari....Waziri Aagiza Wahusika Waachishwe Kazi na Wafikishwe TAKUKURU

K
SERIKALI imebaini ufisadi mkubwa ndani ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kutokana na kukamilika kwa kazi ya Tume iliyoundwa mahususi ili kuchunguza utendaji wa mamlaka hiyo, na imeagiza kuchukuliwa hatua kwa watu wote wanaotajwa kuhujumu Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alisema hayo wakati akizindua Bodi mpya ya TPA inayoongozwa na Profesa Ignas Rubaratuka jijini Dar es Salaam jana.

Akiagiza hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa wahusika waliotajwa katika ufisadi na ripoti hiyo, alisema kwanza ni baadhi kufikishwa mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na wengine kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi lakini akionya kuwa ni marufuku kwa wahusika kupewa barua za onyo.

Katika kudhihirisha kukerwa na utendaji wa TPA, Profesa Mbarawa ambaye baadaye alifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Bandari ya Dar es Salaam, aligoma kukabidhi mabegi ya kuwekea nyaraka kwa wajumbe wa Bodi mpya kwa kusema kuwa yalikuwa ni ya gharama sawa na yale yanayotumika kusafiria Ulaya.

Akizungumzia kukamilika kwa kazi ya Tume, Profesa Mbarawa alisema tume hiyo iliyowajumuisha wataalamu mbalimbali imefanya kazi kubwa ya kuchunguza utendaji wa TPA na kubaini ufisadi mkubwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya mifumo ya miundombinu kama katika mita za kupima mafuta (flow meters).

Kuhusu mita za kupimia mafuta, aliitaka bodi hiyo kuwa makini katika kusimamia utendaji kazi wa mita hizo alizosema serikali imetumia Sh bilioni 12 kuzinunua ili kuhakikisha kuwa zinafanya kazi vizuri na kwamba zinapoharibika ni lazima uamuzi wa ama kununua mpya au kuzirekebisha ufanywe haraka.

Alisema ufisadi mwingine umebainika katika miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), ambako mingi imewekwa ili kuwanufaisha watu na si serikali, mgongano mkubwa wa maslahi kwa Bodi ya Zabuni uliochangia kukwama kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo, ajira za kindugu, kulindana, mtandao wa wezi, rushwa na uwezo mdogo wa kiutendaji.

Kuhusu mgongano wa maslahi kwa Bodi ya Zabuni ya TPA, ambayo aliagiza ivunjwe mara moja na kuundwa mpya, Waziri Profesa Mbarawa alisema Bodi hiyo imekuwa ikitanguliza mbele kile alichokiita ‘ten percent’ katika kila zabuni na kukiri wazi kuwa bodi hiyo ni chanzo cha matatizo mengi ya Mamlaka ya Bandari.

Alisema kutokana na udhaifu wa Bodi hiyo ya Zabuni, huduma karibu zote zinazotolewa ndani ya TPA zinatolewa na kampuni ambazo ama ni za wafanyakazi wa mamlaka hiyo, au za waume au wake zao, na kama si hivyo basi ni za ndugu, jamaa au marafiki wa wafanyakazi, jambo linalozua mgongano mkubwa wa kimaslahi.

Kuhusu ajira, alisema ripoti imebaini viongozi wa TPA wamekuwa wakiwaingiza kazini ndugu, jamaa na marafiki zao kinyume cha taratibu za utumishi serikalini na alikwenda mbali kwa kusema kuwa TPA ilipohojiwa kuhusu kasoro hizo kupitia kwa mwanasheria wake ilisema; “hakuna tatizo,” jibu alilosema lilimpa mshituko mkubwa.

Kuhusu mazingira ya rushwa, alimuonya Mwenyekiti wa Bodi hiyo mpya kuwa macho na rushwa, akisema watu wanaohujumu utendaji wa Mamlaka ya Bandari ni watu wanaotumia ushawishi wa kiwango cha juu cha rushwa na kutoa siri kwamba wamewahi kufanya jaribio la kumhonga mjini Mwanza na Dodoma bila mafanikio.

“Ripoti imebainisha kuwa wamekuwa wakihonga hata bodi, wanawapa fedha shilingi milioni tano kwa wajumbe wa bodi na hivyo wanapoteza nguvu ya kusimamia mambo. Ikitokea hivyo kwa bodi hii, wewe ni Profesa mwenzangu kwa hiyo ngoma droo lakini nitakuwajibisha. Nitamwomba Rais akuondoe mlango ulioingilia ndio utatokea na hawa wajumbe ambao wapo katika mamlaka yangu nitawafukuza papo hapo,” alionya Mbarawa
nilitaraji jibu kama hilo kutoka kwa mwanasheria....mwanasheria haendeshwi kwa hisia,fununu ,Bali ushahidi

Na pia mbarawa asiingilie Kazi ya mwanasheria mkuu wa serikali,yeye ndiye huamua kumpeleka mtu mahakamani kama kuna hoja za kisheria

Sio mihemko ya
 
Mbarawa ni aina ya JPM ni mtu mwenye uelewa wa sekta nzima ya mawasiliano, halafu mchapakazi. Katika awamu hii atawasumbua sana watendaji wazembe na watafutaji wa fursa za wizi.
 
Maadili ina maana pana sio kama wengi wetu tunavyofahamu ukiwahi kufika kazini mapema ni maadili mema ukimfundisha mtoto watoto kwa moyo wako wote kwa lengo la mtoto yule afanikiwe ni maadili mema kufanya kazi kwa nguvu zote kwa lengo la kusaidia taifa lako ni maadili mema ninachotaka kusema kwa professor makame mbarawa ni kiongozi mwenye maadili mema.
 
Back
Top Bottom