Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,077
- 136,505
Kuna siku moja hivi nilikuwa sina hili wala lile. Nimekaa tu nyumbani naangalia dari, kuta, na sakafu za marumaru.
Basi nikampigia simu mshkaji kuona ana mpango gani kwa jioni ile.
Akasema 'Ngabu kwa nini tusiende Ramada tukajivinjari hapo?'. Nikasema poa. Nikaenda nikamkuta tayari keshafika yuko na wachuchu wawili.
Nikaagiza Pinot Grigio halafu nikajichanganya naye. Sasa nikawa nimevutiwa na yule binti mwingine, Janeth.
Nikaanza kupiga naye stori na mambo mambo. Sasa huhitaji kuwa mwanasayansi wa roketi za anga kung'amua kama nilikuwa nimemtamani. Hata yeye aliliona hilo lakini akawa anajishebedua tu.
Baadaye ndo akaniambia eti anataka nimtongoze. Nikapigwa na butwaa. Ina maana wakati wote huo nilikuwa simtongozi?
Kutongoza ndo kukoje kwani? Ni lazima useme maneno gani? Maana huenda hiyo sehemu ya mchezo mi bado sijaijua.