Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Na kweli akijitokeza it may cost him or polish him.,
It has a profound effect kwenye election results, hasa hapa kwetu ni kitu kigeni.,

Asipojitokeza nayo inashusha credibility..like kwani anaogopa nini?.
Ni mtego...na fursa at once

Kwa kuwa tushaingia Uchumi wa Kati basi ingekua poa tufanye matendo ya nchi za Uchumi wa Kati!
Itakuwa aibu ya mwaka.
Hajua kujibu hoja ngumu atachomekea upupu wake, atatukana bure.
 
Nope!

Wala sijabadili.

Principles! Principles! Principles!
Na hapo ndio tatizo la watu wetu lilipo.

Hawawezi, kwa mfano, kutenganisha mtu na misingi/wazo.

Wanapata tabu sana wakiona unakosoa mtu unayekubaliana nae.

Katika fikra zao ukikubaliana na mtu unakubaliana nae hook, line and sinker.

Nope, sie wengine ni watu huru, kifikra na kivinginevyo.
 
Duh!

Mshikaji umetisha.

Maana una mawazo sawa na yangu kwa kiasi kikubwa sana!!

Halafu unajua nini, ndo maana ndani ya vyama vyetu vya kisiasa tumeona watu wakifukuzwa uanachama kutokana na kutofautiana kidogo tu kifikra.

Hakuna room for disagreement.

Tuliona akina Zitto na Kitila walivyofukuzwa CHADEMA.

Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.

Tumeona Membe alivyofukuzwa CCM.

Udikteta wa kifikra huo.
 
Malaika wa mitandaoni wameshashuka katika sura tofauti tofauti.

1.Kuna kanuni nyingi sana (subsidiary legislation) zimetungwa na TCRA na waziri wa mawasiliano zenye malengo ya kuminya watu kupata majukwaa ya mitandaoni.

Kanuni za usajili, leseni na vitu vya sampuli hiyo. Kanuni za maudhui ya mitandaoni nk... Zote zina malengo ya kuweka vigingi.

2. Upandishwaji mkubwa wa vifurushi vya data. Intaneti siku hizi ni bidhaa ya wenye pesa. Bidhaa ya watu wachache. Wale wote wanaobaki wamewekewa mazingira ya makusudi ya kushindwa kumudu bei za vifurushi.

3. Usajili wa namba za simu kwa njia ya kitambulisho cha taifa. Huu ni mpango wa makusudi wa kuwafanya watu wakose mawasiliano.

4. Matumizi mabaya ya sheria ya makosa ya mitandaoni. Mapolisi wamegeuka kuwa walinzi wa mitandaoni. Ukizungumza fyoko tu umenaswa.

Haya yote ni matokeo ya kauli ya magufuli.

Magufuli amewashusha malaika wa mitandao katika sampuli tofauti tofauti.
Very insightful!

Shukrani.

Sasa mimi niliposema nataka Magufuli ashindwe kwenye hilo, eti kuna watu mpaka leo hii hawanielewi!

Sisi sijui tuna laana gani tu??!!
 
Nope!

Wala sijabadili.

Principles! Principles! Principles!
Kama aliyeyaandika haya ya kwenye huu uzi ndiye yule yule aliyeandika ule uzi wa kumwombea fulani,basi "principles" imepata maana mpya kama ilivyo "maendeleo hayana vyama" na "msemakweli ni mpenzi wa mungu".
 
Huh? Weka vielelezo ili ueleweke!
 
Kwani sijawahi kumpinga?
Kwa nadra sana........

Wewe ushabiki wako kwa Jiwe huwa wakati mwingine umepitiliza.........

Wakati mwingine huwa unajifanya "kipofu" kwa yale ambayo sisi wengine tunayaona makosa ya wazi wazi ambayo huwa anayafanya Jiwe!
 
Unaweza nitajia mada zangu tano ninazompinga Magufuli??
 
Kwa nadra sana........

Wewe ushabiki wako kwa Jiwe huwa wakati mwingine umepitiliza.........

Wakati mwingine huwa unajifanya "kipofu" kwa yale ambayo sisi wengine tunayaona makosa ya wazi wazi ambayo huwa anayafanya Jiwe!
Naona umekula kona kwa sababu huwezi nitajia.

Na huwezi nitajia kwa sababu uliandika kwa hisia kusadiki tu.

Huna facts.

Checkmated!
 
Duh!

Mshikaji umetisha.

Maana una mawazo sawa na yangu kwa kiasi kikubwa sana!!

Halafu unajua nini, ndo maana ndani ya vyama vyetu vya kisiasa tumeona watu wakifukuzwa uanachama kutokana na kutofautiana kidogo tu kifikra.

Hakuna room for disagreement.

Tuliona akina Zitto na Kitila walivyofukuzwa CHADEMA.

Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.

Tumeona Membe alivyofukuzwa CCM.

Udikteta wa kifikra huo.
wewe na huyo unamyemjibu ni mtu mmoja, acha kutuzuga...tatizo lako wewe linalokusumbua ni JAMUKAYA!.
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Maxence kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hiyo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Ashindwe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom