Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Unajua watu wengi tumepigwa bumbuazi kutoka na msimamo wako wa sasa,umekuwa mtetezi wa kila kitu juu ya serikali yaani huoni huambiwi,unalizungumziaje hilo?
 
Unajua watu wengi tumepigwa bumbuazi kutoka na msimamo wako wa sasa,umekuwa mtetezi wa kila kitu juu ya serikali yaani huoni huambiwi,unalizungumziaje hilo?

Mimi nimekuwa mtetezi wa kila kitu juu ya hii serikali?

Nyie watu mnachekesha sana.

Nimekuwaje mtetezi wa kila kitu ilhali juzi tu hapa nimewapinga na msimamo wao wa kukataza wanafunzi wa kike wapatao mimba kurudi shuleni?

Hilo nimelipinga juzi tu hapa na hata mwezi haujapita.

Hata hizi kampeni za sijui Magufuli atawale kwa zaidi ya miaka 10 nimezipinga na nitazipinga daima.

Huwa mko wapi nikiwa nampinga?

Hivi, kwani mnadhani ni lazima watu wote tuwe ni washabiki wa vyama?

Sio lazima wote tuwe CCM au CHADEMA.

Wengine hatuna vyama na huko kutokuwa na vyama kunatuweka huru zaidi.

Kwa vile kuna mambo namuunga mkono Magufuli hiyo haina maana namuunga mkono kwenye kila kitu. Mengine nampinga. Kwa hiyo wala sijabadilika. Akipatia sehemu nitamuunga mkono. Nikiona kakosea nitampinga.

Hata kwa vyama vya upinzani ni vivyo hivyo. Wakipatia jambo nitawaunga mkono. Wakikosea nitawachana.

Lililo gumu kueleweka hapo ni lipi?
 
Ukinyonga wako
 
Magufuli ni jembe ni sharp kama kisu cha bucha, mtasubiri ashindwe ila ndo anaongeza kasi. In short he is the best president in africa kwa sasa. Nakuona wewe ni mpumbav na mshenzi mkubwa maana hauwezi kutoboa mtumbwi ambao wewe mwenyewe umeupanda. Sikutofautishi na lissu ama katibu mkuu wa cuf malimu. Unataka magufuli ashindwe, then what next akishindwa yeye unadhani wewe utabaki salama, ni sawa na mbumbumbu wenzako wanaofundisha wazungu kutuwekea vikwazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msimamo wako wa awali ulikuwa kwamba JPM hata sifa ya kuwa Rais hana. Sasa kama hata sifa hana inakuwaje udai kuna mambo unakubaliana naye na mengine hukubaliani naye?
 
Msimamo wako wa awali ulikuwa kwamba JPM hata sifa ya kuwa Rais hana. Sasa kama hata sifa hana inakuwaje udai kuna mambo unakubaliana naye na mengine hukubaliani naye?

Hata kama kwa maoni yangu naona kuwa hana sifa ya kuwa rais, lakini uhalisia wa mambo ni kwamba yeye ndiye rais.

Kwa hiyo, maoni yangu juu ya uwezo wake wa kuwa rais hayazuii uhalisia wa kwamba yeye ndiye rais.

Mimi kukubaliana naye kwenye baadhi ya mambo na kupingana naye kwenye baadhi ni kwa kuzingatia uhalisia uliopo.

Umenielewa?
 
Namuunga mkono Magufuli kwenye mambo mengi kasoro la kutowapa shahiki watumishi
 
Hili ndilo bandiko la mwisho huyu jamaa kumkosoa Rais, mengineyo tunayashuhudia wote humu mtandaoni, ni sifa kwa kwenda mbele. Sasa yeye na wanaonunuliwa sijui kuna tofauti gani. Kumbe alikuwa na price tag?!!!
 
Ngoja aje umuulize, unataka ashindwe Rais? Majibu utayapata
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…