Nataka niwashtaki Halotel

Rais mstaafu alisema hao Halotel Viettel watatoa smartphone bure
nakumbuka hiyo kauli, pia kwa msisitizo mzee wa wapigwe tuu alisema smart phone zap zitauzwa kwa elfu sitini....
 
naunga mkono hoja...washtakiwe tu,maana hakuna namna nyingine
 
Hawa jamaa wezi kweli, halafu hizo 800MB hazifiki. ukidownload 200MB tu wanasema umefika kikomo. TCRA sijui wanafanya kazi gani??
 
Mimi mtandao ninaoutumia kudownload ni hallotel hawa jamaa ki ukweli wapo vizuri hayo mnayosema mimi hayajawai kunitokea
 
Mleta mada, kwanza tofautisha speed na data (MB/GB), MB wamesema kabisa n 800mb, speed kwel haina kikomo, tatu ni kuwa baada ya mb800 kuisha ntaendelea kutumia net ila kwa speed ndogo, hata voda na tigo ni hivyo hivyo, haya makampuni ni wezi kwel lakini uzuri wanaibia wajinga wagumu kuelewa
 
Yani halotel wanaimba kweli
 
Umekurupuka nikwamba spidi kali mpaka mb 800 baada ya hapo ni spid yakawaida
 
Ni speed bila kikomo sio data bila kikomo...kawashitaki halafu uwalipe kwa usumbufu...
 
Lakini inategemea na applications hizo mbili zilikuwa na ukubwa gani, kama zilikuwa na 800mb, basi ni sawa kwamba ulimaliza bundle yako na hivyo hutakuwa connected. Na ukiwa hujaunganishwa speed bila kikomo haiwezekani.
 
Halotel niwezi kweli kabisa nilisajili laini yao SBB ya hizo bado kuniibia nimesha ivunjavunja laini hats namba siikumbuki tens,nilijiunga na Kifurushi cha bila kikomo nikawa naangalia mieleka yenye crop za DKK 5 kama NNE hivi wakanitumia msg kuwa Kifurushi changu kimeisha,nikaunga kingine napo wakanipiga ndipo nilipo amua kuvunja laini,hamia Airtel 1000 unapewa jb 1 tenaunatumia na inaisha kwa halali kabisa kama ulivyo tumia
 
wamekwambia ni unlimited speed sio unlimited data
Mtoa Uzi Alivyojiunga na hicho kifurushi hakujua maana ya Unlimited Speed na Unlimited data na wala hakusoma Vigezo na masharti
 
Halotel wako vizuri sijajuta kununua laini ya Halotel. Huwa naacha salio hata wiki nalikuta ingekuwa airtel thubutu uone. Airtel yangu ..06 nimeitupa kisa kula salio langu kila siku/wiki
 
Bundle ya 800 unaenda kufungua kesi ? Baadae mwenyewe utaifuta hiyo kesi
 
Hiyo line naitafuta. Ntaipataje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…