Nataka niwashtaki Halotel

el nino

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
4,712
5,051
Kwa kuwa hii tabia ya makampuni ya simu kutuibia kwa kufanya ulaghai imezidi huku mamlaka husika zikiwa kimya kama hazina kazi (TCRA ni jipu watumbuliwe tuu maana hakuna namna ) sasa naamini ni muda muafaka wa kampuni moja kuonyeshwa mfano..

Nianze na hawa halotel ambao wanasifika kwa mtandao mzuri na kweli wana net ya ukweli, wana bundle lao ambalo wanaliita la spidi bila kikomo(800mb kwa buku), nadhani watu wote tunaelewa maana ya neno bila kikomo..

Nimenunua hili Bundle nikadownload kama application 2 wakantumia message kwamba nimefika kiwango cha mwisho cha spidi hivyo .. yaani application 2 tu... nikaanza kujiuliza maana ya neno spidi bila kikomo ni nini? Na kwanini walisema ni spidi bila kikomo? Najaribu kufikiria wakifanyia watu 100,000 kila siku kama hivyo wanapata bei gani kwa ulaghai huu?

Hapo sijataja wizi wa vocha umeweka unakuta imekatwa wamekuunga wenyewe na huduma wanazo jua wao (kama Tigo ndo maexpert wa hii kitu).

Nimekuja kupata hitimisho kuwa haya makampuni yote ya simu yapo kifaida zaidi kiasi kwamba hawajali kabisa huduma wanazotoa.

Hakuna wa afadhali ila ntaanza na nyie Halotel maana mmekuja juzijuzi tuu mshaanza kujifunza umafia , mkifikisha miaka 10 si mtaua watu.
 
Kuna sehemu tu nilijua hawa wa Vietnam watakuja kutushika masikio.. Anza nao mkuu,Ukitoka huko turudi Tigo maana wameshaota mapembe na mkia kbsaa.
 
Kwanini mnakurupuka na makampuni mapya? Au walikuwa wanagawa lunch na dinner bure? Hata miez miwili hauna tayari mtu ashatimkia huko....hahah isomeni tu namba, tunalipa madeni ya uchaguzi
 
hili tulishalijua mapema, wapo wengi wanalizwa ila wanakosa pakusemea..

Kibaya zaidi hata TCRA wanalijua hilo, lakini wanalifumbia macho.
 
Kwanini mnakurupuka na makampuni mapya? Au walikuwa wanagawa lunch na dinner bure? Hata miez miwili hauna tayari mtu ashatimkia huko....hahah isomeni tu namba, tunalipa madeni ya uchaguzi
Udhaifu wa hayo ya zamani ndo umefanya tukimbilie mapya... hasahasa ujambazi wa Tigo na voda
 
Na Airtel pia wameanza ujambazi aw SMS na Bundle. Utakuta mtu umejiunga na yatosha ya wiki au Mwezi unatuma sms kama ishirini ndani ya siku mbili ukituma sms au kutumia bundle unakuta zero kote sasa unajiuliza zile sms na bundle la data zimeenda wapi.
 
Mi niko Zangu Airtel tangu enzo hizo inaitwa Celtel (Making life better) wala sitaki kujaribu wengine.
 
Unlimited speed & unlimited data downloading / uploading ni tofauti:
Lakini nikubali kuwa Kampuni kadhaa za simu zinaibia watu fedha kwa kuwachomekea huduma pasipo maelezo ya kinagaubaga! Consumerism ni somo linalotakiwa ili walaji tujue haki zetu tukatae 'matangazo majipu'.
Hata yale ya masomo yanayoshawishi watu kusoma Vyuo fulani na kwamba baada ya hapo 'Kuajiriwa ni lazima!!' Hata wangesema kuwa stadi za maisha ni lazima tunawaelewa. Voda wanaweza ongoza katika kutokuwa wazi katika huduma zao mf. Voda RED; Cheka ; Mpango Mzima; Ofa maalumu n.k
Kama katika Elimu na hata Mafuta tuna msamiati wa bei elekezi kwa nini hawa wa simu na vingámuzi kama AZAM, DSTV n.k , nao wasiwekewe?
 
Kwa kuwa hii tabia ya makampuni ya simu kutuibia kwa kufanya ulaghai imezidi huku mamlaka husika zikiwa kimya kama hazina kazi (TCRA ni jipu watumbuliwe tuu maana hakuna namna ) sasa naamini ni muda muafaka wa kampuni moja kuonyeshwa mfano..

Nianze na hawa halotel ambao wanasifika kwa mtandao mzuri na kweli wana net ya ukweli, wana bundle lao ambalo wanaliita la spidi bila kikomo(800mb kwa buku), nadhani watu wote tunaelewa maana ya neno bila kikomo..

Nimenunua hili Bundle nikadownload kama application 2 wakantumia message kuwa kwamba nimefika kiwango cha mwisho cha spidi hivyo .. yaani application 2 tu... nikaanza kujiuliza maana ya neno spidi bila kikomo ni nini na kwanini walisema ni spidi bila kikomo. najaribu kufikiria wakifanyia watu 100000 kila siku kama hivyo wanapata bei gani kwa ulaghai huu..

Hapo sijataja wizi wa vocha umeweka unakuta imekatwa wamekuunga wenyewe na huduma wanazo jua wao (kama Tigo ndo maexpert wa hii kitu)...

Nimekuja kupata hitimisho kuwa haya makampuni yote ya simu yapo kifaida zaidi kiasi kwamba hawajali kabisa huduma wanazotoa..

Hakuna wa afadhali ila ntaanza na nyie halotel maana mmekuja juzijuzi tuu mshaanza kujifunza umafia , mkifikisha miaka 10 si mtaua watu.
Kuna tofauti kati ya spidi bila kikomo na internet bila kikomo, wewe umepewa spidi kubwa zaidi isiyokata kata Ina maana uki download application zenye ukubwa wa mb hizo kwisho habari yako.

Na Internet bila kikomo ni wanakupa internet access kwa makubaliano ya siku, wiki au mwezi bila kukata hapo kidogo nadhani umeelewa na nakushauri watafute wanasheria wakutafsrie hiyo kauli kabla ya kuwashtaki maana usije ukawa walipa
 
Actually holatel pamoja na kupunguza speed hiyo bado naona kwa sasa wapo vizuri kuliko mitandao mingine. Wanapaswa wafafanue tu wanposema speed bila kikomo wanamaanisha nini maana kweli hata ukinunua cha mwezi speed mwanzoni inakuwa kubwa halafu baadae inapungua.
 
Kuna tofauti kati ya spidi bila kikomo na internet bila kikomo, wewe umepewa spidi kubwa zaidi isiyokata kata Ina maana uki download application zenye ukubwa wa mb hizo kwisho habari yako.

Na Internet bila kikomo ni wanakupa internet access kwa makubaliano ya siku, wiki au mwezi bila kukata hapo kidogo nadhani umeelewa na nakushauri watafute wanasheria wakutafsrie hiyo kauli kabla ya kuwashtaki maana usije ukawa walipa
Boss nafahamu tofauti ya unlimited speed na unlimited data..

Nacholalamikia mimi ni Bundle kuitwa la unlimited speed wakati mi nilidownload App zenye ukubwa wa mb 60 out of mb 800 walizonipa wakanitumia message wanapunguza speed yangu wakati wenyewe wamesema ni unlimited speed
 
At least ndo mtandao bora kwa Internet kwa sasa.... Ila ukiweza kuwanyoosha itakuwa sio mbaya
 
Ipo hivi sijawahi kuliona hilo tatizo la application mbili bando liishe mimi ni muathirika wa seasoni na huwa natumia halotel kudownload na huwa wakituma msg nitaendelea mpaka kesho muda nilio jiunga speed tu inapungua ambapo tofauti yake ni mpaka uwe mtaalamu sana ndiyo ujue speed imepungua.....ila na kushauri chukua halotel line ya chuo 9999 7GB mwezi mzima
 
hili tulishalijua mapema, wapo wengi wanalizwa ila wanakosa pakusemea..

Kibaya zaidi hata TCRA wanalijua hilo, lakini wanalifumbia macho.
ndugu yangu hao tcra wakisikia fulani kamtukana kiongozi an kumsimanga watafanya chini juu wakukamate, kwa hili utangoja sana
 
Back
Top Bottom