Nataka niende Singida kwa mara ya kwanza

davetz28

JF-Expert Member
Dec 17, 2017
543
617
Wadau, naomba msaada wenu kwa wenye uzoefu wa kwenda Singida. Sijawahi kusafiri kwenda mkoa huo na ninataka kusafiri mwanzoni mwa mwezi wa Machi mwaka huu.

Ninaomba kuelekezwa mambo yafuatayo ili niweze kupanga bajeti yangu vizuri.

1. Nauli kutoka Dar hadi Singida Igunga

2. Gharama za malazi guest shilingi ngapi na zinapatikana karibu na stand?

3. Nitafika saa ngapi nikitoka Dar saa kumi na mbili au saa moja asubuhi

Nitashukuru sana kwa msaada walau na mimi nifanye ziara ya siku mbili katika mikoa hiyo maana napasikia tu na sina uzoefu wa kusafiri safari ndefu, kwa hiyo itakuwa safari yangu ya kwanza.

Asante kwa muda wako na msaada wako

Mdau wa JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nauli Ni Tsh 35,000/- hadi Singida/Igunga, Guest house/Lodge/hotels zipo za kumwaga Ila nzuri Ni mbali kidogo na stand kuanzia 10,000/- hadi 500,000/- uwezo wako tu, chakula utakula unachotaka, vinywaji Kama kawa!!!!
Karibu sana mgeni mtarajiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu hiyo igunga inapatikana singida maeneo yapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nauli Ni Tsh 35,000/- hadi Singida/Igunga, Guest house/Lodge/hotels zipo za kumwaga Ila nzuri Ni mbali kidogo na stand kuanzia 10,000/- hadi 500,000/- uwezo wako tu, chakula utakula unachotaka, vinywaji Kama kawa!!!!
Karibu sana mgeni mtarajiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa maelezo ya kina, umbali upi? Kama km ngapi kwa sababu nataka nifikie guest mzuri ambayo haiko mbali sana na stand.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gari gani hilo?

Nauli ya Dar - Singida ni TSH 33,000/= kwa Gari la ABC Upper Class na JMC Express.

Hizi ndio gari nzuri na zinazoaminika kwa usafir salama.

Muda wa kufika ni saa 12 jioni.
Asante sana mkuu, nategemea msaada wenu unajua ugeni nap ili nisiwe mshamba sana kwenye mji wa watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sio mbali unachukua bajaji sh 2000 tu inakuzungusha hadi unapata utakapopenda, wenyewe wanazijua Lodge/ hotels za maana, saa 12jioni unafika Sgd na saa 2 kasoro unafika Igunga Kama utashukia huko
Asante kwa maelezo ya kina, umbali upi? Kama km ngapi kwa sababu nataka nifikie guest mzuri ambayo haiko mbali sana na stand.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau, naomba msaada wenu kwa wenye uzoefu wa kwenda Singida. Sijawahi kusafiri kwenda mkoa huo na ninataka kusafiri mwanzoni mwa mwezi wa Marchi mwaka huu.

Ninaomba kuelekezwa mambo yafuatayo ili niweze kupanga bajeti yangu vizuri.

1. Nauli kutoka Dar Hadi Singida igunga,

2Gharama za malazi guest shilingi ngazi na zinapatikana karibu na stand?

3Nitafika saa ngapi nikitoka Dar saa kumi na mbili au saa moja asubuhi

Nitashukuru Sana kwa msaada walau na mimi nifanye ziara ya siku mbili katika mikoa hiyo maana napasikia tu na sina uzoefu wa kusafiri safari ndefu, kwa hiyo itakuwa safari yangu ya kwanza.

Asante kwa muda wako na msaada wako

Mdau wa jamii forum

Sent using Jamii Forums mobile app
Tafuta hela bwana acha kusumbua watu .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom