Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,595
- 65,036
Wakuu mambo vipi,
Mwaka 2006/7 nilikuwa na mahusiano na dada mmoja ambaye nilimfahamu kutokana na mizunguko yangu. Kipindi hicho huyo dada alikuwa akisoma Udsm mwaka wa pili nami nikiwa mwaka huo huo chuo kimoja hapo Moshi. Mahusiano yalidumu kwa kiasi fulani, tukawa tunatembeleana huko anakosoma na wakati mwingine akawa anakuja kunifuata Moshi.
Mwaka 2007 mwanzoni niliamua kusitisha uhusiano baada ya kupatikana mpinzani, kwa bahati mbaya nilimuachia ujauzito bila mimi kujua. Baada ya kuvunja mawasiliano, kwa upande wake alikuwa bado ananitafuta lakini nikawa sijali kutokana na nguvu ya ujana.
Mwezi wa 12 mwaka 2007 alijifungua huku akiendelea na shule na mwaka 2008 alihitimu na mwaka huo huo aliweza kupata ajira mkoani Mwanza.Kutokana na michakato ya kimaisha nami nilihitimu nikawa nazunguka baadhi ya mikoa kutafuta ajira, bila kujua kama niliacha mbegu kwa muhusika.
Mwezi wa kumi na mbili mwaka 2008 mdada huyo alirudi likizo kwao na baadaye akatembelea kwetu akiwa na mtoto huku akiniulizia kwa wadogo zangu napatikana wapi, akiwaambia kama bado sijapata ajira niende nikaishi naye huko aliko...lakini hakuwaambia kama yule mtoto ni wakwangu.
Ndugu zangu walinijulisha lakini sikupenda kufuatilia kwa sababu nilikuwa bize na kusaka shilingi.
Sasa katika pita pita zangu FB wiki iliyopita, nikasema ngoja nimtafute huyo mdada...kufungua akaunti yake wakuu naona picha ya mtoto ameshakuwa binti mkubwa sura ya baba yake. Nilimtamani sana mtoto wangu.
Sasa hapa nipo njia panda, namuhitaji mtoto angalau ajue baba yake yupo ingawa nina familia yangu kwa sasa ila cha muhimu tu nataka mtoto aweze kujua baba yako halali ni Equation x. Nifanyeje wakuu....