Nataka kuvunja uchumba, naomba ushauri

Nataka kuvunja uchumba, naomba ushauri

markbusega

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2015
Posts
826
Reaction score
850
Habari wakuu,

Mimi na mchumba wangu tulikutana secondary tukiwa darasa moja, kiumri tumepishana miaka mitatu yeye ana 27 mimi 30, katika kipindi chote cha masomo ya o level hatukuwahi kuzungumza lolote kuhusu mahusiano, mahusiano yalianza hivi siku moja nikiwa form 5 na yeye akiwa form 5 shule nyingine mkoa mwingine nilisikia simu inaita nilipopokea niliitambua sauti yake tukaongea maongezi ya kawaida tu kabla ya kukata simu aliniomba ni save namba kwamba ni yake na kwamba tutakuwa tunawasiliana, basi akawa ananipigia mara kwa mara, mimi sikuwa siriaz naye maana mziki wa PCB huko shule haukuwa wa kitoto kwangu hivyo niliamua kuwekeza juhudi zote kwenye masomo.

2009 nilimaliza kidato cha 6, nakurudi kufundisha moja ya secondary ya Kata kama partime,kumbe yeye pia alikuwa ni mmoja wa walimu part time hapo shuleni, kwa kweli alikuwa amependeza sana alinipa namba ya simu nyingine akadai ile ile ya zamani alipoteza simu nikaanza kuvutiwa naye, kwa vile wote tulikuwa tunaishi hapo shuleni, tukawa tunatembeleana, akipika chakula kizuri anashare na mimi, wakati mwingine alikuja kunisaidia kupika, nikaona ana care sana baada ya kipindi cha miezi niliamua kutangaza nia, alinicheka sana, nilijihisi mnyonge sana kwa kutokujua amelipokeaje, ukizingatia sikuwa mtu wa wanawake sana.

Baada ya kusisitiza nia yangu kwa kipindi cha miezi 3, akawa amekubali, tukawa tumekubaliana tuoane baada ya masomo sikuona shida kusubiri sote tulienda vyuo vikuu tofouti, ila nilimtembelea nilipopata nafasi ila hakutaka nijipoze hata nilipozidiwa kwa kuniomba nivumilie, nilivumilia na nilipozidiwa marachache nilijipoza kwa wengine waliotumia njia kama yake kunitrap ila yeye ndiye alikuwa moyoni mwangu, tulipomaliza elimu ya chuo kwa vile maisha kwao si haba japo si kivile aliamua kuunga masters na mimi nikaamua kukomaa kitaa nikijishughulisha na biashara ndogondogo huku nikiwinda ajira, baada ya mwaka nikawa nimeajiriwa serikalini, kwa vile mara kwa mara alisisitiza nipeleke posa kwao, nilianza kujipanga mwezi huu niende kwao nipeleke posa, mwezi wa tatu mwakani tufunge ndoa.

Katika maisha yetu ya uhusiano inaonekana yeye tu hupenda kusikilizwa na kinachonikera mpaka nishindwe kumvumilia ni hii tabia iliyozuka ya kuamua mambo tofouti na makubaliano it is vivid she is depriving my manhood mimi niki mind anaomba msamaha,hajaajiriwa kusema huenda amelewa madaraka na fedha naona ni tabia yake binafsi nahisi ananiona boya na hiki kimekuwa chanzo chamigogoro ya mara kwa mara na mchumba wangu hasa katika hiki kipindi cha mwisho cha uchumba wetu kuelekea ndoa nimeona nikatishe uchumba sijui kama niko sahihi.

Naombeni ushauri wadau.
 
Ushagonga?...au bado unasubiria tuu?....muulize kama seal bado ipo...

Anyway hata mie ningekuwa demu ningekuona boya sanaa....miaka yote unasubiria hujachapa??....pole lakini anahaki ya kukudharau kwa kutomchapa nao muda wote huo....
 
Utajua mwenyewe bana miaka yote hiyo leo ndo unamuona hizo tabia
 
Nivizuri kuaoa wanawake wakatao kua mfano mzuri kwa watoto wako,sasa kama unamuona hafai basi hujachelewa...
 
Mhh umeshaamua hivo maana hats ukishauriwa wewe ndo WA mwisho WA kutoa maamuzi amua unaloona n sahihi kwako
 
kama umeshaona madudu na kama unaona huwezi yachukulia na kuwa yako basi jua kuwa hiyo ndoa itakuwa ndoano............. kama umeshaanza kupata wakati mgumu we sepa tu
 
Mmmmmh,pole mkuu kumbe kunawanaume wavumilivu kiasi hicho hongera saaana,ila Kama unampenda mwambie ukweli Kama hata badilika muachane uone atakavo kuwa mpole
 
Umri,kiwango cha elimu na uandishi wako haviendani kabisa!
Acha uonekane boya tu!
 
Kama unaona uchumba ni tatizo, tangaza usebule kabisa. Anyway, changamoto hazikimbiwi, bali hutafutiwa ufumbuzi. Be a man, and act manish starting now.
 
Kunamakosa yacyotbika na yatibikayo chambua chuya 2pa ubak na mchele saf maana tatzo hlo ni lakulcontrol we mwenyewe mbona rahs, ukshndwa hapo je ndoa utaweza? Huo n mtihan ambao hupasw kudisco.
 
Umri,kiwango cha elimu na uandishi wako haviendani kabisa!
Acha uonekane boya tu!

Hujui uandishi wa habari ni taaluma na husomewa na si kila mtu anaweza lakini hope umeelewa na samahani kwa kukuchosha
 
Kaa chini zungumza naye wekeni roles na ujipange tena manake its like we ndo umelelea hiyo tabia, msaidie kiroho nendeni kwenye maombi mkaombewe kwani hiki kipindi cha kukaribia kutimiza huo mpango wa Mungu kuna majaribu mengi sana, kumbuka bora shetani umjuaye kuliko malaika usiye mjua utamuacha huyo ukidhani utampata mwingine mwenye afadhali kumbe uliruka mkojo ukakanyaga mavi.
 
Umri,kiwango cha elimu na uandishi wako haviendani kabisa!
Acha uonekane boya tu!

Sawa mkuu kwa vile uwezo huu ndio unanifanya niendeshe maisha yangu mpaka namshukuru Mungu. Hata hivyo hatuwez kuwa wote sawa
 
Ushagonga?...au bado unasubiria tuu?....muulize kama seal bado ipo...

Anyway hata mie ningekuwa demu ningekuona boya sanaa....miaka yote unasubiria hujachapa??....pole lakini anahaki ya kukudharau kwa kutomchapa nao muda wote huo....
Mkuu,,,,,,,long time sana. Upo....??? Sijaona comments zako muda mrefu....hahahaah.
 
Back
Top Bottom