Nataka Kusoma kwajili ya kazi

Lawkeys

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
1,118
287
Waungwana, naomba niulize swali la kiungwana tuweze kushare uzoefu. Ninataka kusoma kozi yenye tija kwa kulingana na soko la ajiri Tanzania kwa sasa na baadaye. Sasa naomba ushauri wenu wa kiungwana nisome course ipi kati ya hizi na kwanini. Ni level ya Diploma wakuu.

1. Sociology
2. Social work
3. Human Resource
4. Business Administratio; na


Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Kutokana na utafiti nilioufanya Business Administration inalipa sana
Ili ku-prove hili nilisemalo uwe unasoma magazeti mbalimbali utaona nafasi nyingi za kazi zinataka watu wenye MBA
 
Wsh wud say something, ila kwa kozi hizo watu wapo wengi sana.,
ushauri wangu, kama unaweza jaribu kozi za science hasa IT., hii wengi wanasoma hata waliosoma Art..!
 
Tayari umepata jibu lisilo na shaka apo juu. Si kwamba tunadharau profession tajwa apo juu,ila kama unategemea soko la ajira pigana na BBA. Sikuwai kusoma iyo kozi,ila najua iko wide. Next time fikiria na Law, Accountancy,Taxation na banking. Ni vinara ktk soko la ajira. Ni mawazo yangu tu. Note: kama unataka diploma,waweza kusoma kozi yoyote ila ukisogelea digrii au advanced diploma ndo uwaze kozi muruwa kwa kuwa watu professional uanzia apo na si diploma wala cheti. All the best.
 
Waungwana, naomba niulize swali la kiungwana tuweze kushare uzoefu. Ninataka kusoma kozi yenye tija kwa kulingana na soko la ajiri Tanzania kwa sasa na baadaye. Sasa naomba ushauri wenu wa kiungwana nisome course ipi kati ya hizi na kwanini. Ni level ya Diploma wakuu.

1. Sociology
2. Social work
3. Human Resource
4. Business Administratio; na


Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Mkuu Lawkeys; nakuomba ubadili mtazamo wako kwamba unataka kusoma kwa ajili ya kuajiriwa.....?????. Tunasoma ili tupate maarifa ambayo yatatusaidia kutatua changamoto zinazotukabili kwa hiyo siyo lazima kuajiriwa, unaweza kujiajiri mwenyewe vilevile. Unatakiwa kusoma kile ambacho unaamini unapenda na siyo kutazama soko la ajira, soko la ajira hubadilika kutokana na wakati na uhitaji, unaweza kuanza kusoma leo IT lakini baada ya kumaliza soko la ajira likawa halina uhitaji wa aina yako. Vile vile kumbuka waajiri hawaajiri watu kutokana na kile walichosoma bali kutokana na kile wanachoweza kufanya kutokana na ufahamu walionao. "EMPLOYER employee people for WHAT THEY DO WITH THAT WHICH THEY KNOW."
 
Back
Top Bottom