Ni sawa kuoa MMERU, mm ni mmeru na angallia jina langu hapo halafu uwakumbuke wakurdi wa kule Iraq ambao ndio walisababisha Sadam Kunyongwa. Ishu ni kuwa kwanza wanawake wa kimeru ni Wakali, kwa hilo jiandae, pili hawataki longolongo katika maisha ni kama wachaga tu uhakikishe unatulia na kutafuta hela. Hawana uswahili. na kama ni ishu ya ni namna gani uende kwao
Tafuta mtu yoyote ambae atakuakilisha kama mshenga
Then mtaenda na kujitambulisha endapo ni siku ya kwanza/ japo siku hiyohiyo mnaweza kueleza nia yenu yaani kuoa- hapo kama una hakika mtazungumizia juu ya kuoa utapeleka KIRERENGO- Hii ni pombe kama debe 12 kwa ajili ya kueleza nia yako, kama ni walokole huwa ni soda creti kadhaa, hapo ishu ya menu upande wa mke wanaandaa.
Then mtapatana mahari kikawaida ni ngombe anayitwa SIIKYI huyu ni ngombe jike ambae hajazaa ila anakaribia kubeba mimba na huwa wanaequate kwa fedha ambapo mwaka 1996 alikuwa 60,000 so sasa hivi ni kama laki 2.Ukishatoa hiyo andaa harusi yako na kama ukafanya harusi ndugu yangu utaaga umasikini -wanajua kuzawadia hao ogopa
ila
kama unataka kuoa kienyeji chukua mzigo weka ndani then kesho yake tuma mtu akaseme fulani yuko kwako wasimtafute na mtu huyo huyo anaweza kuongea kwa kuyamaliza na wazee bila complication yyt, njia hii hutumiwa sana siku hizi na kwa wazazi wengine anakuambia sitaki mahari yako ila mkaishi vizuri. Ila sasa wameru wanapenda sana shehere za harusi
karibu unywe Loshoro bhana