Nataka kuoa kati ya hawa wadada wawili

Nataka kuoa kati ya hawa wadada wawili

Mastamind

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
1,319
Reaction score
847
Nilikua na Mahusiano na binti mmoja ambaye tulikua tukifanya nae kazi me nikiwa kama boss wake, tulivyoingia kwenye mahusiano alianza kuniwekea masharti ya kutozaa coz anataka aende kujiendeleza kielimu, aling'ang'ana sana na hilo ikafika kipind hata mambo ya ndoa yakawa hayafanyiki, yakifanyika ni kwa upande mmoja tu, yaani yeye hana ushirikiano, kazini akienda anachelewa kurudi anarudi jioni ambapo anafikia kuuliza kama msosi nimepika (sikuwa na wasiwasi naye kwenye uaminifu, alikua anachelewa makusudi tu coz ya kutoelewana).

Pili maamuzi yetu mengi alikua akiingiza misimamo ya babake na kaka zake. Tuliishi hvyo me nkachoka nkapata mchepuko m1 uliokua boss wetu nae ambaye hakua anajua uhusiano wetu.

Tuligegedana na huyo boss wetu akadata akawa serious anataka ndoa. Nikawa namrusha, kutokana na kupga cm mara kwa mara alikuja kushitukiwa na kutukanwa na kutakiwa kuachana na mie. Kweli aliachana namie ila kwa masikitiko sana mpk akaugua hoi. Tulienda na binti huyu ambaye me ni bos wake ikafika wakati nikamtega akiwa kwenye siku ya fertilization akanasa. Baada ya muda alikwenda likizo kwao mkoani, akiwa likizo kaka zake walimshitukia ni mjamzito wakamshauri atoe na kumnunulia vidonge.

Aliwarubunirubuni mpk likizo ilipoisha akarudi kazin aliponiomba ushauri kuhusu kaka zake nikamwambia hilo ni juu yako wewe, ukitaka wasikilize ukitaka waache. Aliwaacha na kulea mimba ile mpaka kujifungua. Katika maisha niliishi nae nikiona nafanya majukumu yangu kwake kama kawaida. Ziku za maternity leave zilipokwisha alituma barua ya kuacha kazi akiwa bado kwao. Nilimshauri asiache ila akagoma, nikawataarifu mama yake na ndugu wa karibu na maboss wetu wakamwita na kumshauri lakini aligoma. Nikamtishia kumuacha kama ataacha kazi akawa kiburi, akaacha kweli akiwa kwao.

Baada ya miezi kadhaa akaja na mtoto kunitembelea, akagundua tumerudiana uhusiano na yule boss wetu tena, akaliamsha dude yule boss mpaka akaugua na kupelekwa kwao coz ya BP na ni emotional sana. Baada ya miezi kama miwili aliaga kurudi kwao mara moja coz babake kamuita, akarudi. Aliaga baada ya wiki anarudi but mpaka now ni mwezi wa 7 huu. Anadai hawez rudi mpaka nikamkomboe.

Swala lake ni jema ila kwangu naona km ananipelekesha sana. Nimetia mgomo namie mpaka aje kwanza kama alivyoahidi. Kipindi hiki baada ya boss wetu kupona tulirudiana coz nilimhurumia sana na ni very humble.

Ni mchaga asiye na tabia za kichaga ukiacha hela. Sasa hivi kaniteka kweli licha ya changamoto za wakubwa wenzie kumshauri aachane namie kisa ya hadhi, wanamtafutia hadi mambwana kumshawishi mahusiano but hataki.

Changamoto ya uhusiano wangu na yeye umri nimemzidi miezi 8 na tayari ana mtoto mmoja aliyezaa na Dr.mmoja aliyemtelekeza mara baada tu ya kumpa mimba miaka mi4 iliyopita

Naombeni Ushauri:
Nimuache yule binti niliyezaa nae, kiburi, jeuri ila nishafanya nae mambo kama mawili matatu hivi.

Au Nimfate huyu boss mwenye umri unaolingana ila msikivu, mnyenyekevu, adabu licha yakuwa na mtoto tayari miaka 4 now?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asa umri una tatizo gani hapo au unatafuta kisingizio tu chakuendelea kumgegeda tu bila mipango nae?....huyo uliyemzidi mbona kakushinda kama unaangalia kigezo cha umri?
 
Sema na moyowako, itafute furaha yako ilipo, inaweza kuwa kwa aliyekuwa bos wako au kwa kijakazi wako, nb. Fanya MA Uzi sahihi ambayo hutakuja kuyajutia.
 
Uyo boss wako ni vyema ukamfikiria japo sisi kwetu kijijin tunambiwa tusioe mwanamke mwenye magonjwa ya kurithi,...na B.P. kusaidia mfarakano wa familia pindi akitutangulia,...ila boss wako ana upendo wa dhati na anathamin upendo wako,
 
kabla ya kumuoa boss hakikisha unakuwa mwanaume kweli (maana inaonekana legelege sana)

maana mara 2-3 umesema mdada akamwamshia dude boss mpaka kulazwea sijaona jitihada zako za kumkinga boss (ambaye ameshikiria kazi yako, mwenye mapenzi ya kweli)

yaani nakushauri huku nasikitika maana inaonekana mdada anaweza rudi na kuamua atakalo na upo tu unang'aa sharubu. KUWA MWANAUME....KUWA NA MSIMAMO
 
kama ww umeshindwa kuamua
sisi ndo tutaweza bro pambana na haliyako tyu

sent from aifoni seveni plasi
 
Boss wa kichaga ananyenyekea ndoa baada ya kutelekezwa ukishaoa Tabia yake halisi utaiona.. Kama kweli ulimpenda dada wa watu ukamzalisha kamilisha taratibu ummiliki asiendeshwe tena NA ndugu zake!!!! Lazima aendeshwe maana anatambulika bado yupo mikononi kwa wazazi wake!!!! Note..usiruhusu damu yako kulelewa NA baba kambo....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nawe Acha uboya ya nini uhangaike na huyo uliezaa nae wakati unaona kabisa anavyokupelekesha mpige chini chukua huyo mkubwa mwenzako,but kumbuka kumhudumia mwanao na akifikisha miaka angalau mi3 kamchukue
 
Mngekuwa mnakuja kuomba ushauri kabla mambo hayajaharibika ingekuwa vizuri kweli...

Ila sasa mambo yashaharibika naona unataka tu kutumalizia wino wa 'keyboards' zetu...

Wewe mwenyewe umeweka wazi kuwa ulimtegea binti wa watu akiwa ovulation ukaweka mimba, sasa hivi kashapata mtoto unataka kumtelekeza...

Watu wengine sijui huwa mmejambwa na tembo....
 
Masingle mothers huwa wana tabu sana kwa kulazimisha ndoa hao ndio balaa, kuwa makini hapo isijekuwa anataka ndoa tu na wewe kisha anyooshe makuacha yake. Umri sioni kama ni tatizo....mwenzako mimi alinifia mwanamke aliyenizidi umri na mimi ndio nikawa dereva wake....akikupenda atakuwa msikivu tu kwako. Ceteris paribus muowe boss wako.

Sukari Yenu
 
Back
Top Bottom