Nataka kununua shamba Rufiji

PRESIDA TO BE..

JF-Expert Member
Dec 12, 2012
302
200
Ndugu.wasalaam..
Mimi ni kjana ambae natafuta maisha kupitia kilimo.
Ndugu wana JamiiForums nmekuja hapa kwenye hii forum kuulizia mwenye information ya kupata mashamba huko Rufiji na wanauzaje kwa heka. Nataka nifanye kilimo cha umwagiliaji...

Kama hutojali PM unisaidie kijana wa kitanzania anaetafuta pesa kihalali na sio vinginevyo..

Asanteni sana kwa kunielewa!
 
Ndugu.wasalaam..
Mimi ni kjana ambae natafuta maisha kupitia kilimo.
Ndugu wanajamiiforum nmekuja hapa kwenye hii forum kuulizia mwenye information ya kupata mashamba huko Rufiji na wanauzaje kwa heka. Nataka nifanye kilimo cha umwagiliaji...

Kama hutojali PM unisaidie kijana wa kitanzania anaetafuta pesa kihalali na sio vinginevyo..

Asanteni sana kwa kunielewa!
Andaa kuanzia laki 5 kwa heka ila bei yaweza kupungua kama litakuwa mbali zaidi na mji
 
Unataka kulima nini ndugu? Maximumu laki 4 na kushuka chini, mimi nalima huko na nina mashamba huko tuwasiliane kwa msaada zaidi.
Naomba utueleze hapa mkuu. Wengi tutafaidika. Tukija wote huko kwenye mawasiliano yako utapata shida kutujibu wote kila mtu kwa wakati wake. Thanx in advance!
 
Rufiji imegawanyika ndugu kuna maeneo yenye maji namaanisha sehemu zilizo karibu na mto jambo ambalo sio rahisi sana kupata itahitaji upige kambi upate wenyeji haswa usije ukapigwa, sehemu ambazo hazina maji ni kwanzia maeneo ya jaribu kuelekea kibiti mpaka rufiji yenyewe, ukitafuta maeneo hayo itakupasa uwe nguvu kubwa maana itakubidi uchimbe kisima au ulime mazao yanayotegemea mvua kama, mananasi, muhogo na passion nk, hapo ndio maana nikauliza unataka kulima nini? Pia nilimuuliza mtu mmoja aliokuambia andaa laki 5 alafu akakuambi mbali na mji inapungua, shamba tangu lini linakuwa mjini? Maeneo kwanzia jaribu kwenda kibiti mpaka rufiji kwa mashamba haiwezi kuzidi laki 4 ikizidi hiyo itakuwa kiwanja, mimi nipo maeneo ya bungu njia yakwenda nyamisati natumia maji ya kisima na mambo yanakwenda tu, ndugu yangu nivizuri kufikiria kikubwa but kwenye utekelezaji nivizuri kuanza na kidogo.

NAKUTAKIA KILA LAKHERI.
 
Uchawi upo kichwani mwako ndugu, ukiamini na kuishi kwenye hizo imani utapata tabu sana ndugu, kwani huko uliko wachawi hawapo? Na kwataharifa yako Dar es salaam ndio mkoa 3 kwa uchawi lakini kila siku watu wanakuja tu .
 
ALF najua wewe ni mtu wa rufiji,pole ila waambie wajomba zako waache,kama vipi wawaloge wasomali wasiendelee na vita
 
Ha ha ha, mimi ni msukuma ila tangu ninunue shamba huu ni mwaka wa sita sasa nipo na hao jamaa na ninaishi nao vizuri tu.
 
Ndugu.wasalaam..
Mimi ni kjana ambae natafuta maisha kupitia kilimo.
Ndugu wanajamiiforum nmekuja hapa kwenye hii forum kuulizia mwenye information ya kupata mashamba huko Rufiji na wanauzaje kwa heka. Nataka nifanye kilimo cha umwagiliaji...

Kama hutojali PM unisaidie kijana wa kitanzania anaetafuta pesa kihalali na sio vinginevyo..

Asanteni sana kwa kunielewa!
Mkuu kama walivyokwambia wanajamvi wenzangu Rufiji ni wilaya na makao makuu yake yapo Utete.
Wilaya ya Rufiji kwenye barabara kuu iendayo Mtwara imeanzia Jaribu Mpakani, Bungu, Kibiti, Ikwiriri, Nyamwage njia panda ya kwenda Utete,Muhoro Mpaka Somanga. Kama alivyokuambia Mkuu ALF bei inategemea uhitaji inaanzia laki 1 haizidi 4 kwa heka. Swali langu unahitaji heka ngapi? Angalizo mashamba yaliokuwa karibu na barabara kuu huwa bei za juu kidogo.
 
ALF kubishana na mtu mwenye imani yake utapata shida tu ila mimi nikushukuru kwa maelezo yako maziri yenyekueleweka,lakini mkuu mimi nipo Ikwiriri na kulingana na mahitaji ya mdau huo ni lazma aweke wazi kwanza anataka kulima mazao gani ili tunapokuja kumpa information tumpe zenye usahihi kulingana na matakwa yake
 
Ndugu zangu mimi nataka kilimocha vitunguu na matikiti so nahataji sehemu iliyo.karibu na maji...
 
Rufiji imegawanyika ndugu kuna maeneo yenye maji namaanisha sehemu zilizo karibu na mto jambo ambalo sio rahisi sana kupata itahitaji upige kambi upate wenyeji haswa usije ukapigwa, sehemu ambazo hazina maji ni kwanzia maeneo ya jaribu kuelekea kibiti mpaka rufiji yenyewe, ukitafuta maeneo hayo itakupasa uwe nguvu kubwa maana itakubidi uchimbe kisima au ulime mazao yanayotegemea mvua kama, mananasi, muhogo na passion nk, hapo ndio maana nikauliza unataka kulima nini? Pia nilimuuliza mtu mmoja aliokuambia andaa laki 5 alafu akakuambi mbali na mji inapungua, shamba tangu lini linakuwa mjini? Maeneo kwanzia jaribu kwenda kibiti mpaka rufiji kwa mashamba haiwezi kuzidi laki 4 ikizidi hiyo itakuwa kiwanja, mimi nipo maeneo ya bungu njia yakwenda nyamisati natumia maji ya kisima na mambo yanakwenda tu, ndugu yangu nivizuri kufikiria kikubwa but kwenye utekelezaji nivizuri kuanza na kidogo.

NAKUTAKIA KILA LAKHERI.

mkuu asnte je kukichimba hicho kisima ili cost bei gani
 
Yrsozigwa nakubaliana nawewe, cause nikauliza je yeye anataka kulima mazao gani? Akijibu mazao gani ndio wadau watamsaidia kulingana na eneo la hitaji husika.

Nimepokea simu kutoka kwa wadau mbalimbali nashukuru kwa siju zenu na kuonyesha nia katika kilimo, mimi nipo maeneo ya bungu njia yakwenda nyamisati, hivyo naweza kutoa msaada kwa watu wanaohitaji maeneo sehemu za Kimbendu, Mlanzi, Msumo, Hanga, Mahege na nyamwage na wakati fulani kuna mtu alikuwa anauza shamba eneo la Jaribu ila sijawasiliana muda kujua kama bado lipo.

Ila kwa ushauri nivizuri kama mnachukua maeneo, mkachukua maneo ya karibukaribu inakuwa faida sababu mnakuwa na mawasiliano ya taharifa, pia hata kuunganisha nguvu kwa kuweka maendeleo ya haraka.
 
Back
Top Bottom