Nataka KULIMA ALZETI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka KULIMA ALZETI

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by FUSO, Aug 15, 2011.

 1. F

  FUSO JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,855
  Likes Received: 2,331
  Trophy Points: 280
  Wakuu wa JF hasa MR. MLILA

  Nataka kuanzisha kilimo kikubwa cha alizeti, kutokana na soko lake kuwa la juu sana hapa nchini nimeona ni muda muafaka nijikite huko na sitakuwa hapa mjini kwa muda kuanzia November mwaka huu.

  Nina maswali machache tu ambayo inabidi niyatafutie majibu yake kabla ya kuaza zoezi hili.

  1. Ni mkoa upi unafaa kwa kilimo cha Alzeti
  2. Je kuna mbegu aina ngapi za Alzeti na ipi itanifaa katika mkoa tanjwa?
  3. Nina uhakika na masoko ya ndani, je kuna mtu anafahamu masoko ya nje maana nitalima si chini ya hekari 100 kwa kuanzia.
  4. Wazo langu linaendana na kupata mashine ya kukamulia Alzeti hiyo na Packing - je kuna mtu ana fununu za mashine hizi na bei zake hasa za India na china?

  Kilimo ni kwa vitendo si maneno: Natoa hoja.
   
 2. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  kama unaomba ushauri usitaje mtu direct kama unamtaka MALILA unge-MP sasa hapa wengine kukushauri wataona wanajipendekeza wakati unamtaka zaidi malila na ndio utakayemuamini.
   
 3. F

  FUSO JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,855
  Likes Received: 2,331
  Trophy Points: 280
  mkuu nimeandika wana JF then nikasema hasa mlila lakini sikumaanisha kwamba wengine sintapokea mawazo yao anyway naomba niifute kauli yangu na nawaomba radhi wana JF kwa usumbufu uliojitokeza.

  Napenda kupata ushauri / Mawazo kutoka kwa mwana JF yoyote kuhusu hiki kilimo cha alzeti.
   
 4. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  1. Ni mkoa upi unafaa kwa kilimo cha Alzeti ----- Singida na Manyara.. nilijaribu Bagamoyo nikatoka kapa. ninaposema kapa namaanisha nimepoteza si chini ya milioni moja (nilijaribu ekari 10). maeneo ya babati na kiteto kuna kampuni inafanya contract farming ila wakati mwingine inaumiza kwenye bei. kampuni hii inaitwa FAIDA MALI unaweza kuigoogle utaipata.
  2. Je kuna mbegu aina ngapi za Alzeti na ipi itanifaa katika mkoa tanjwa?--- mimi niliagiza Morogoro, sijajua jamaa alizichukua wapi ila naweza kukuulizia. ila hata arusha mjini zinapatikana.
  3. Nina uhakika na masoko ya ndani, je kuna mtu anafahamu masoko ya nje maana nitalima si chini ya hekari 100 kwa kuanzia--- anza na soko la Tanzania, ukiweza kamua mwenyewe na utapata faida zaidi. ukenkiitaka kujifunza kwa vitendo nenda Tegeta kibaoni. ukifika kibaoni karibu na LUKU na jengo la benki ulizia jamaa wanaokamua mafuata ya alizeti utaelekezwa. watakupa zaidi ABC ya nini wanafanya. maana jamaa anakamua na kufanya packing. KAMA ukiweza usianze na ekari zote 100 otherwise uwe umefanya soil analysis na kupata mtalaamu.anza kidogo utest kama zinakubali au la.
  4. Wazo langu linaendana na kupata mashine ya kukamulia Alzeti hiyo na Packing - je kuna mtu ana fununu za mashine hizi na bei zake hasa za India na china? SIDO wanategeneza mashine hizo na ni nzuri. sijajua bei yao. wapigie watakupa details ila kipindi fulani zilikuwa kwenye 3-5ml kutegemea na capacity na accessories zake.

  kwa maelezo zaidi hebu soma thread hii iliwahi kujadiliwa hapa JF siku za nyuma https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/53704-tujadili-alizeti-kama-zao-la-kibiashara.html
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,855
  Likes Received: 2,331
  Trophy Points: 280
  kweli haya ndiyo manufaa ya JF. majibu mazuri pia nitaenda kwenye hiyo topic nipitie discussions mbali mbali - Asante mkuu - nitaanza utafiti katika maeneo uliyopendekeza, Yes ni kweli kwa kuanza ni vyema nitajaribu hekari 10 hivi kwa season one. Sina uhakika kama wizara ya kilimo na ufugaji wana soil anaysisi map ya nchi yetu kunisaidia kwamba wapi nilime zao gani nitajariu kuwaona vile vile.
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Dr wa Ukweli kachanganya majina kati ya Malila na Mlila, aliyeombwa kuchangia mada zaidi ni Mlila.
  Mimi Malila kama mjumbe nichangie kama ifuatavyo. Alizeti inalimwa sehemu kubwa ya nchi yetu, napenda kukupa majina ya maeneo yafuatayo yanayolima sana alizeti na sababu zake.
  Idodi Iringa/Mtinko singida/Mby Vijijini/Morogoro/Kibakwe Dom/Chunya,Wanda Singida, huko alizeti inalimwa sana na biashara imeanza huko siku nyingi, usafiri upo, manpower ipo na wanunuzi wa jumla wapo.Haya ni maeneo ambayo unaweza kupata ardhi kubwa sehemu moja kwa bei nzuri sana. Maeneo ya kanda ya kaskazini kama Babati/Hydom/Kilu six huko au Arusha na Moshi, kupata ardhi kubwa huko ni suala gumu kidogo,maeneo kama Handeni/Kilindi kuna ardhi kubwa,bei pia imesimama juu kidogo,vitapeli uchwara vipo. Kiteto ardhi ipo mbugani,lakini mvua zake ni za mashaka sana.

  Songea kuko vizuri, lakini kupata eka 100 ni mziki kidogo. Maeneo niliyopendekeza yana mashine nyingi za kukamulia alizeti zinazofanya kazi sasa na hivyo kuongeza ushindani.

  Majibu ya Kanyagio hapo juu ni sahihi kabisa.
   
 7. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2015
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,092
  Likes Received: 11,231
  Trophy Points: 280
  Kama nikitaka kulima alizeti kama eka 500 napati wapi eneo kama hilo??
   
 8. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2015
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,353
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Project inaendeleaje?
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2015
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Njoo Iringa vijijini kuna maeneo mwafaka kwa kilimo cha alizeti.
   
 10. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2015
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,092
  Likes Received: 11,231
  Trophy Points: 280
  Umesharudi? Ile appointment yetu vipi?
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2015
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Nimesharudi, ila ratiba imebana vibaya, naomba tuwasiliane jumapili jioni tuone hali ikoje.
   
Loading...