Nataka kujua uhalali wa Kalynda E- commerce

Mbna nimeona insta watu wanapewa pole Kwa kutapeliwa na hii?
 
Serikali inasubiri tu mpunga ujae wauzuie... hakunaga biashara ya kirahisi hivyo.... AT LEAST ya Mr. Kuku ilikuwa inaeleweka maana bidhaa alikuwa nazo japo janja janja tu
 

Leseni huwa hazilipwi kwa pesa ya kitanzania kwa makampuni ya kimataifa so kuna wajanja pale brela washapiga watu changa la macho ukishaona mwanzo tu kuna utaperi ujue kikinuka hamna atakayekamatwa
 
.........Tufanye kazi wazee.

Pesa sio rahisi hivyo.
 
Litalia jitu...ni suala la muda tu..

DECI, Mr. Kuku..........Kalynda...

Mwanzoni huwa ni mtelezo tu....ila wakikusanya mpunga mrefu.. Kalynda itabaki story... Then vilio kama DECI na Mr. Kuku..s

Serikali inawacheki Kwa mbaaaali ikiwazomea wajinga.

ACHENI KUPENDA KITONGA.
 
Alikuja kunishawishi nilimwambia sina hela ya kujiunga akasema atanipa hela nijiunge nikipata faida nitarudisha basi ikawa hivyo leo nimemwambia tumeshapigwa kwa hiyo hela yake sina [emoji1][emoji1][emoji1]
Vipi system imecollapse[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Imecollapse kitambo toka jana then wanapiga sound kua technicians wako kazini itarudi tarehe 10. Watu wameshasepa na kijiji wako zao dubai wanakula bata kwa hela za wajinga
Mamaeeeee,Demu aliwakuwa amenishauri niweke Million niingie kundi la V.I.P,Yaan leo nilikuwa nampa pesa dadekii
 
Kalynda wanakuambia wana kwikwi ila watarudi

 
Acha maswali mengi sisi huku tumejiunga longtime kwa sh 20,000 na kila siku unapiga kamisheni ya sh 800 siku zinavyoenda mbele kamisheni inaongezeka kwa sasa napiga 6000 kwa siku.. jiunge hapa kwa link hii maisha magumu!! Kalynda
Wabongo kwa kuuzana ndio maana tuliuzana Utumwa huna huruma kabisa na Ndugu zako.😣
 
Kusajiriwa Brela haimanishi kwamba uko smart, tena kampuni zote za kutapeli kitu cha kwanza huw ani hicho.

JATU aliingiza hadi kampuni DSA ila mwisho wa siku watu wamepigwa
 
Mamaeeeee,Demu aliwakuwa amenishauri niweke Million niingie kundi la V.I.P,Yaan leo nilikuwa nampa pesa dadekii
Mimi hizi issue za mitandao siweki hela yangu anaekuja kuja kunishawishi namwambia yeye ndo anipe pesa nikipata faida kama asemavyo nitamlipa
 
Ipo hivi.. huu ni mchezo wa pesa.. hakuna biashara pesa yako inaenda kufanya.. isipo kuwa ukiweka 20K inaenda kumlipa mtu aliye kutangulia ili awahakikishie wengine kuwa inalipa.. pyramid scheme huwa zina mwisho hasa pale ambapo pesa inayo ingia kutokana na watu wapya inakuwa ndogo kuliko pesa inayotakiwa kuwalipa wale walio tangulia..
 
NCHI INA WAJINGA WENGI
ACHA TU WAUMIZWE

ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…