Nataka kujipima mwenyewe HIV, napataje vile vipimo?

shopping

Member
May 29, 2012
20
10
Wadau naomba msaada, vile vipimo vya kujipima mwenyewe HIV naweza vipata wapi. Nimejaribu kuulizia pharmacy nyingi hawauzi.
 
Huwezi kuvipata popote zaidi ya hospitali/zahanati na kama utavipata pharmacy basi ni makosa haviuzwi.

Mtafute mfanyakazi wa hospitali itakuwa rahisi kupata.

Daktari/nurse/medical attendants n.k

UNGEKUWA KARIBU NINGEKUSAIDIA JAPO 2 Kits upime we na mwenzio.
 
Si kuna dawa unayodondshea kwenye damu?
 
Nyumbani kwako una maabara?

Una sehemu nzuri na salama ya ku-dispose vipe vifaa utakavyotumia?

Utasafisha vipi uki-contaminate mazingira ya hapo utakapojipimia kwa hiyo damu yako?

Utakuwa na moyo wa kuyahimili matokeo yakija ndivyo sivyo?

Na je unajua procedure zote mpaka upate majibu negative au positive?

Waswahili acheni ujuaji we nenda hospitali kapime saaafi uchukue majibu yako urudi kupiga kazi (in sizonje voice)
 
Nenda kapime hospital mkuu, kupima nyumbn mtihan na hasa ukiwa huna experience na hizi vitu.
 
Hivyo haviuzwi pharmacy,

Ni illegal kuviuza vitu kwa duka lolote lile wenye mamlaka ya kuviuza hivi vitu ni MSD pekee
 
Back
Top Bottom