Udochi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2015
- 782
- 1,056
Habarini mabibi na mabwana.
Kichwa cha mada kinahusika kabisa hapo juu.
Kutokana na kile kipato changu cha awali elfu 8 hadi 10 kwa siku,
Nilipanga chumba kimoja Uswahilini,
Ambapo nilikuwa na wapangaji wenzangu kibao,
Kila baada ya siku kadhaa mixer kuamshana alfajiri kwa ajili ya mchango wa luku,
Vilevile ukiamka asubuhi hata uwe na haraka au ubanwe na haja kiasi gani, ni lazima uwe mpole kusubiria wengine waingie chooni/bafuni (choo na bafu havijatenganishwa- ni hichohicho kimoja, na ni kwa wapangaji wote).
Asubuhi mixer kupishana kwenye korido na akina dada wamejifunga vibwebwe waenda kuosha vyombo, kufua n.k.
Muda mwingine full mwingiliano wa sauti za redio na TV kutoka vyumba vingine.
Kiukweli hali hii inanikosesha amani, sema uwezo wa kiuchumi nd'o tatizo.
Sasa kutokana na mihangaiko ya hapa mjini kwa sisi vijana tusichoka kufaiti,
Kipato kimeongezeka kufikia elfu 13 hadi 15.
Katika mizunguko yangu ya hapa na pale jana nikakutana na rafiki yangu ni fundi rangi,
Alikuwa anapaka rangi nyumba moja kali kinyama.
Nikaingia mle ndani nikakuta nyumba inavutia sana,
Ina chumba self (choo ndani), sebule, na jiko, umeme wa kujitegemea (sio wa kushea na wengibe), maji masaa 24, milango na madirisha ya grill, na yana vioo vya alminiamu,
full tiles na gipsum.
Kwa kweli niliitamani sana ile nyumba na nikaumia roho sana kwa kuwa najua kabisa hizi nyumba ni za watu wazito,
Sio masikini kama sisi.
Nikajaribu kumuulizia yule rafiki yangu fundi rangi,
"Hivi kama hii wanapangisha Sh. ngapi chumba?"
Akacheka, akanijibu: "hii haipangishwi kwa chumba mkuu,
Hii ni apartment ambayo inapangishwa yote.
Subiri mwenyewe anakuja, nitamuuliza."
Mara mwenyewe akafika,
Akamuuliza,
Akasema "Kwa hapa mjini ni laki na nusu, ila hali ilivyokuwa ngumu nikipata mtu wa laki 1,
napangisha kwa 100,000/=, inalipwa kwa miezi 6."
Kiukweli nikasema wenye nazo wanafaidi sana,
Nikamuuliza tu kwa kujaribu "kaka kama mimi nanayo ya miezi mitatu huwezi kunifikiria?"
Akasema,
"Bwa. Mdogo ingawa hali ya uchumi ni ngumu, ila fanya angalau ya miezi 4,
Tafuta laki 4 nikupe mkataba kuanzia mwezi ujao".
Nikamwomba namba ya simu yule mmiliki, nikamwambia ngoja nikachanganue tutaongea.
Nimecheki kwenye Tigopesa nina laki 5 na nusu.
Wakuu, kwa hiki kipato changu vipi,
Nijilipue ili nikajiachie kwenye apartment kali au niendelee kukaza huku Uswahilini kwenye sakafu ya simenti?
Hapa nipo ghetto naumiza ndonga, kuwaza na kuwazua.