Nataka kubobea kwenye utalaam wa kutengeneza Website na Graphics

Nataka kubobea kwenye utalaam wa kutengeneza Website na Graphics

Heshima kwa wakubwa wote wa tech!

Mimi nina taaluma yangu tofauti kabisa na utaalam wa masuala ya computer!, lakini kuna jambo moja ambalo kila siku linaendelea kunivutia siku hadi siku. Nayo ni kuhusu utaalam wa masuala ya Websites na Graphics!

Nimejikuta sioni dhamani ya computer isipokuwa naona dhamani ya Websites na Graphics! (please naomba kueleweka hapa)

Naombeni mwongozo kwa wale watalaam wa hii taaluma hasa masuala ya Websites na Graphics!


Nifanye nini ili nibobee kwelikweli yaani niwe "specialist" kwenye suala la Websites na Graphics!

NB:
Siwezi kukaa darasani fulltime na kusomea digrii ya kwanza, walau nisome online ama part time ama nikipata executive ndo baridaa zaidi!

Ahsanteni sana!

Cc deejaywillzz
 
Last edited by a moderator:
Kwa kifupi i want to be a specialist in web and graphics issues!
MaishaPesa ingekuwa vizuri kama ungeelezea unataka ujifunze mwenyewe au shuleni?

Ila kinyumbani nyumbani ungeanza na Graphics (Photoshop na Illustrator) kisha ujifunze website (HTML na CSS kwa kuanzia).

Kwenye upande wa website niongezee kidogo. Website inahusisha programming, na kuna programming languages nyingi unaweza kutumia na ukatengeneza website ila HTML, CSS na JavaScript lazima zihusike
 
Last edited by a moderator:
Kwanza natumaini unajua kiingereza...then,binafsi ningekushauri kitu.

1.Usiwe na haraka,haya mambo si rahisi Kama unavyofikiri yanahitaji muda na kuwa committed

2. Mara nyingi utajikuta kuna mlolongo wa programs ambazo kila kukicha zinatengenezwa na kila mtu avutia upande wake:Read a best book first,otherwise you won't read at all

3.Anza na programs ambazo matumizi yake yataanza kukufaidisha siku ya kwanza na pia ni program mama inayotumika na watu wengi... Mfano ni Adobe Photoshop,inatumika kuanzia graphics creation,photography,architecture, games,movies e.t.c

4.Practice...ndugu,hakuna maana ya kujua kitu ambacho hukitumii.Kuna tofauti Kati ya kujua na kuwa mjuzi kwenye haya mambo ya graphics.Ukimaliza hata section moja au program moja anza kupractise otherwise utaishia kujua tu kama wengi wanaojua.

5. Be creative,tatizo la watu wengi hudhani hizi program ndio zinafanya "maajabu" kifupi ndio,ila ukweli ni creativitivy ya mtu...jifunze kuwa creative, kifupi take your time kujiendeleza kwenye program moja kwanza.Of course Kama unataka kuwa exceptional kwenye graphics

6.Soma:Adobe programs ; Photo shop, Illustrator na After Effects...hizi ni kwa kazi za kudesign logo,picha,kuweka effects...then kuna Adobe Dreamweaver kwa ajili ya website...

7. Tutorial zipo nyingi mno mtandaoni,Kama utafundishwa na mtu ni muhimu kujiendeleza mwenyewe pia.Nenda YouTube utakutana na ma-pro mwenyewe

8.Lynda .com....Hii ndio website pekee ninayoweza kukushauri uanzie kujifunza Kama utakua pekeyako...of course kuna kulipia but watu wengi wana tutorials zake,watafute.

9.Be updated always

10.Safari njema
 
Mi ntakushauri upande wa graphics

1. Kuwa na tools kuanzia software yani adobe na corel draw nk, na ukipata drawing pad itakua safi sana (mi natumia wacom lightpad)

2. Tengeneza moyo wa kujifunza na njaa ya mafanikio kwa kusoma tutorials,kujiwekea goals nk

3. Kuwa mvumilivu coz ujuzi hauji hivihivi

4. Baada ya kujifunza different techniques na styles ni muhimu i repeat muhimu ujitengenezee ur own style na ndo itakayokutofautisha na wengine

5. Kama wengine walivyosema hakikisha kuwa always upo updated

Mi nakushauri ingia tuts-plus.com upate tutorials za graphics na trust me utafika tu.
 
ushauri siwezi kupa zaidi ya uliopewa juu na jamaa, sema kuna moja kakwambia corel draw na kuwa na drawing pad kama katoa mfano ya watcom, huu ushauri usiusikilize, drawing pad ya nini kwa web designer unless unataka kufanya michoro complex you are good to go kwa kutumia mouse na keyboard vzr tu, nimefanya kazi kibao na kutengeneza illustrations nyingi sana za makampuni tofauti sijawahi tumia drawing pad, software kwa graphics msikilize aliyekwambia photoshop na illustrator, zitakumalizia kazi yote, hizi sijui corel draw unaongeza list ya vitu unnecessary mwishowe utakua na load kubwa ushindwe pa kuanzia....

Tl;dr....
English, HTML, CSS, JavaScript, ServerSide language(wengi wanapenda PHP binafsi napenda python) Photoshop na Illustrator(hii sio lazima unless unataka kufanya vector images, google ujue vector images ni nini) Determination, Curiosity pia ya kujaribujaribu vitu, hadi hapo unaweza tengeneza site yoyote unayofikiria kichwani...
 
Back
Top Bottom