Preta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 24,323
- 18,793
Preta utaweza hii kazi kweli?
nipe # ya cm nikupe acapela
Preta utaweza hii kazi kweli?
nipe # ya cm nikupe acapela
Nina kuhahakikishia utabarikiwa wewe na Kizazi chako chote! Maana kanisa likiwa na band basi ujue neno litaingia waumini na kondoo wengi hawatapotea
Mimi vegetarian sili nyama ya kondoo
Kwa maana hiyo hata chumvini wewe huzami?
Vegs hatuzuiwi kula chumvi...labda kama una bladipresha
Teh Teh Teh Teh! Aaaaahhhhh! Hehehehe, mnanichekesha sana. Mbinguni choir vs dhambidhambi Band. Nani zaidi hapo? Wenye macho hawaambiwi tazama. Mkiulizwa nani anataka kwenda mbinguni mwasema "Mimiiii, Mimiii" hakuna asemaye anataka kwenda motoni. Sijui inakuwaje watu wanafika motoni na hawapataki?????
Wakuu,
Nilipokuwa likizo nilifurahia sana burdani ya muziki wa bendi. Sasa nafikiria kuanzisha yangu kama uwekezaji fulani.Nkaraibisha maoni yenu kama hii bizinesi ni ya ukweli au la.Pia naomba ushauri wa kitaalamu kuhusu vyombo,ufundi na usimamizi wake.
Shukran Awal....
wa kiduku utakulipa sana kaka! si unajua hadi huko juu ya mauongozi ya tanzania wanaifagilia?
Safari naomba tuwasiliane mimi nimefanya kazi katika mazingira ya biashara unayotaka kuifanya siri nyingi za biashara hiyo nazijua. Nilikuwa Mhasibu wa Safari Sound Orchestra enzi za kina Ndala Kasheba za Dukuduku naujua muziki (ninauweza na nina kipaji cha kuimba kwa kujifurahisha siyo kwa kuajiriwa) ninafahamiana na wanamuziki wengi tu wa kikongo na wabongo. Ushauri wangu ni kwamba jee Unapenda Muziki? Kama unapenda muziki OK. Kama unataka kuanzisha bendi kwa sababu ya pesa tafuta shughuli ingine kwani utasononeka mambo yakiwa magumu. Jee vyombo unavyo au una mtaji wa kiasi gani kwa ajili ya kununua vyombo? Utapiga mziki wa aina gani? Rhumba, Bongo fleva au Jazz. Unategemea wateja gani watakuwa wanakuja kwenye muziki wako? Mwisho nipigie kwa ushauri zaidi. simu 0755394701