House of Commons
JF-Expert Member
- Oct 1, 2013
- 2,189
- 2,211
- Thread starter
-
- #81
badiebey il ufanikiwe ni lazima uchague moja, na Kuchoma Meli moto kuna maanisha huna paln B wala C bali una plan A tu, Wagiriki walichoma Meli zao moto ili wabakie na plan A tu ya kushinda Vita, Hivyo katika safari ya Ujasirimali ni lazima uwe na only one plan, namanisha, Plan A iwe ni ujasirimali, Plan B iwe ni ujasirimali pia na hivyo hivyo plan C, Ila plan A ikiwa ujasiriamali na plan B ikawa ni kazi ya kuajiriwa hutaweza kufanikiwa.
Unacho takiwa kufanya ni just kusonga mbele na unacho kifanya, usiingie kwenye ujasirimali ukiwa na roho ya kusita sita, no wewe ingia na pambana bila kumuonea yoyote aibu,
Tafuta kwanza vitabu vifuatavyo vya uvisome kwa makini: "Rich Dad Poor Dad", "Be Rich & Happy" na "How to quit from your job" vyote vya Robert Kiyosaki. Vinaweza kukupa ushauri mzuri zaidi. All the best.
Tehe tehe, Mkuu ndo maana nikakwambia unatakiwa kufanya maamuzi magumu sana na katika kuchukua maamuzi inaweza some time hadi kuvunja ndoa yako, unaweza kosana na ndugu Ila ni lazima kuchagua moja.
Kuacha kazi na kuingia kwenye ujasirimali si kazi ndogo ni kazi ngumu sana so ni lazima uwe na spirit ya kipekee kabisa
Wasalam wapendwa
Si kwamba nimechanganyikiwa, hapana. Naona kama nachelewa kutimiza malengo yangu na kazi niliyo nayo ni ya kuajiriwa na ofisi zake ni vijijini. Kwa miaka 10 nimekekuwa nikisafiri kutoka ninakoishi (naishi moja ya jiji hapa nchini) kwenda ofisini. Zifuatazo ni hasara na changamoto ninazoziona kwenye ajira hii
1 Nina shughuli zangu mbadala (miradi) huko jijini, kila wiki 1 au 2 lazima nione maendeleo yake, hii hunigharimu sana kifedha kiasi cha Tshs 80,000 hadi 100,000 kwa mwezi.
2 kipato changu kinachotokana na ajira si kikubwa sana ukilinganisha na shughuli binafsi nilizonazo
3. Shugughuli za ofisi zina nature ya kumlazimisha mwajiriwa kufanya kazi mchana, usiku hadi weekend (sometimes) bila overtime au incentives in turn
4 Sipendi kuhamishia familia huko kazini kwangu maana nitaongeza gharama za maisha na kupoteza dira na malengo yangu
5 Sioni kama ajira rasmi itanipa kipato thabiti kabla ya umri wangu wa uzeeni
6 Nataka kutumia Elimu yangu ya " shahada ya udhamili ya usimamizi wa miradi" kuendeleza miradi yangu binafsi
7 Naona kama utumwa fulani kuwa mwajiriwa, hii inanifanya au niwe mtoro kazini au ku Underform kazini kwangu
Kwa sasa bado naendelea, ila miradi yangu itakapokuwa na thamani ya 300mil nita resign with good will, na hili nitalifanya ndani ya miezi 18 ijayo kuanzia leo.
Just to share with you friends, you can advise otherwise, maana haya maisha nayo hubadirika, nipe uzoefu na mawazo yako tafadhari...
Mawazo mazuri japokuwa uzi ni wa siku nyingi, kiukweli inabidi tutoke utumwani maana hata mie huwa hili ninalifikiria na ndio maana katika kipindi changu cha kufanya kazi nimekuwa nikifanya kazi kwenye taasisi binafsi kwa mkataba kama strategy ya kutoka utumwani na serikalini sikuwahi kuomba kwa kuogopa kuizoea kazi hasa ukizingatia ajira za serikalini zenye mafao bora nyingi huwa zina wenyewe except kwa zile profession ambazo ni maalum ambazo kwa unyeti wake huwezi kufanya ufisadiNdugu yangu hongera kwanza kwa kufikiria hilo mm nilishaquit zamani nilifanya 4.5yrs na sasa niko pazuri sana. Ushauri wangu ni huu ulipotarget kupata mil300 ni mbali sana na unaweza usifike kirahisi. Ila mm nilitumia formula hii; km naweza zalisha pesa sawa na mshahara net nikiwa bado utumwani basi inanitosha sana kuondoka nikaemploy nguvu zangu zote. So inawezekana tu kaza buti. Halafu ukijiajiri utajua kuwa economy kwani ulichopata leo hutakitumia ovyo kwani hujui kesho kutakuwaje. Walioajiriwa huwa hata wanaoverspend kwani wanajua mshahara unakuja tar zile ishirini naaa... So kaza buti!
Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums