So, huko ntakakokwenda itabidi nijisalimishe kwenye matawi yao au ntakua napeleka cash dirishani?CRDB wataendelea kukukata kwa maana lazima tu mwezi ukipita wakutafute, ila bodi ya mikopo sina uhakika maana mpaka waanze tena mchakato wa kukutafuta.
sheria ya mifuko ya jamii inakataa,huwezi ukazuia mafa ya mtu kwa kuwa ana mkopo ktk taasisi ya fedhaHuo mkopo umeufanyia nini mpk hutaki kulipa, pia nani kakuambia ukija private hutakatwa malipo ya HESLB, pia kumbuka unaakiba mfuko wa jamii ambayo itazuiwa.
Ushauri kama unataka kuja private basi makosa uliyofanya ya huko usiyarudie (mkopo usio na tija), pia ukumbuke huku contract term niya mda mchache so inabd uwe mjanja ukikopa unafanya cha maana ili siku ikibuma basi unaendeleza maisha.
mikopo ina ribaLipa deni kwanza, mwajiri wako hatokubali uache kazi (kama utafuata utaratibu wa kuacha) wakti una deni ambalo alikudhamini, pia itakupotezea uaminifu iwapo utahitaji kukopa tena.
Mie niko kwenye hatua za kuachana na ajira ili nisimamie vizuri mishe zangu,
lakini nasubiria kamkopo kaishe (ambako nilikachukua kukazia mishe zangu) pamoja na sababu nyinginezo
Pia usijerogwa ukaacha kazi bila ya kuwa na uhakika na kibarua kingine
Unahitaji Kukombolewa maisha ni zaidi ya kula na kunywa.Hakuna kitu kizuri kama ajira ya kudumu inayokupa uhakika wa kula na kunywa maisha yako yote!