Hahahha!! umenikumbusha mbali sana mwenye thread hii,huyo jamaa anaitwa Fred Saganda aka SAGANDA,alikuwa anasoma zamani kaole kule bagamoyo baadae akawa lecturer pale pale kaole,ni producer wa music na mtengeneza film,na anatengeneza pia hizi short film mfano za ukimwi zinazozaminiwa na mashirika ya nje,kwa kweli kipaji anacho,mi namjua vizuri sana mana nilisoma nae pale mlimani na hata wakati tukitengeneza nyimbo zetu enzi hizo tulikuwa tunamwita aje atoe ushauri wake alikuwa peace sana.kwa sasa anafanya maigiz kwenye stesheni ya STAR TV,kwenye kipindi cha PICKABOMB!!,kile watu wamevaa kama masnamu halafu wanaigiza rafudhi ya kichaga na kipemba, we tazama star tv utamwona tu yeye ni yule jamaa anayeigiza kwa kichaga.Jamaa kwao alikuwa mambo supa sana mana dingi alikuwa ni profesa na yeye alikulia mule ndani chuoni ndipo baba yake anapokaa,inasemekana dingi yake alikuwa hataki kabisa jamaa asomee maswala ya muziki ila jamaa muziki ulikuwa kwenye damu ikabidi dingi mwenyewe asarende.
Kwa kifupi hawa ni watoto wa kishua wa maprofesa yeye pamoja na wengine akina HASHIMU DOGO,wote hawa wamekulia ndani mule udsm watoto wa maprofesa.
Mara ya mwisho nilikutana naye mwenge kituo ch mabasi miaka mingi sana nyuma,alikuwa anatoka bagamoyo kaole nafikiri,siku zote alikuwa anatembea na gitaa lake,anaimba rap lakini ni mwimbaji mzuri wa reggae pia sema kutokana na uzushi wa ma-DJs wa bongo watu wengi wenye vipaji waliamua kusarenda akiwemo saganda kuepuka manyanyaso yao mana walikua wanajifanya miungu-watu hasa hasa CLOUDS wale jamaa ni mashetani wakubwa sana siwapendi kabisa ndio walioua mziki wa bongo.