Natafuta WebDesign Software | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta WebDesign Software

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mwazange, Dec 16, 2008.

 1. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wazee nimerambazarambaza sana nikitafuta webdesign software lakini naona kizungumkuti tu, hujui ipi ni ipi. Naombeni ushauri ipi bomba iliyopo kwenye market today ....Nataka ambayo itakuwa na vikorombwezo vya kila aina.
  haya napokea ushauri.....moja...mbili.....tatu....anza.
   
 2. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwazange,
  Ungekuwa specific sana kuhusu aina ya tovuti unayotaka kuitengeneza, kama ni ya kibiashara, ni ya kifamilia, ni ya mambo yako binafsi n.k., ili tujue ni software gani itakufaa kwa kazi hiyo. Kwa namna ulivyoweka maelezo yako, mimi binafsi nashindwa kuelewa "Vikorombwezo" unavyotaka. Vikorombwezo ndivyo hasa vinavyoamua aina ya software utakayotakiwa kutumia ili kufikia lengo lako la kuwa na tovuti unayotaka. Kwa mfano iwapo unataka tovuti yako iwe na 'animations', lazima utumie softwares zenye uwezo huo, kama vile 'adobe dreamweaver', Flash, n.k. Na kama hutaki makorokoro mengi zaidi, basi zipo nyingine kibao sana ikiwemo MS Front Page, webpage-maker, Java DK n.k, ushindwe wewe tu.
  Nadhani tupo pamoja!
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Dec 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Habari zako

  hujasema kama wewe ni mwanafunzi unataka kujifunza au ni mtumiaji unataka updates kutoka kwa wenzako kama ni mtumiaji huwa unatumia aina gani au tu ni kazi ya ofc badala ya kupeleka kwa wataalamu umeona ufanye mwenyewe tu kwa kutumia software fulani fulani kwa sababu umesikia ni rahisi kutoka kwa washauri wako yote hii hujasema

  Hata hivyo siku hizi kuna kitu kinaitwa cms content management system kuna tovuti nyingi zenye kutoa huduma ya tovuti yenye huduma hiyo kwahiyo ukinunua hiyo unachotakiwa ni kusema tu tovuti yako inahusu nini kama ni shule basi utapewa cms maalumu kwa ajili ya shule kama ni kuuza basi utapewa inayofanana na wewe kazi yako wewe itakuwa ni kutoa na kuweka vitu tu update zitafanywa na yule mtu aliyekupa cms kutokana na mkataba wenu

  unaona maisha yalivyomarahisi ?

  kwahiyo wewe kama sio mtaalamu au hujui mambo ya tovuti nakushauri ufanyie bidii zaidi fani yako uliyonayo halafu mambo ya tovuti tafuta watu waliosomea fani hii wanaoijua na wanaoifanyia kazi siku zote kwao utapata mambo mengi zaidi kwa sababu sio kazi zao

  wewe endelea na uhasibu tu au uhandisi tu
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Dizaidi f'lani unaonekana una roho korosho.
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Dec 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hapana watu wanatafuta ajira na kutafuta kazi kwahiyo awape kazi hiyo inayowahusu tusitake kufogr vitu halafu fani nzima ya ict isiheshimike
   
 6. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkulu Idimi shukrani sana, samahani kama sikuwa muwazi zaidi, nataka ya tovuti za kibiashara....animations ni muhimu zaidi...Au kama unaona unaweza ukanisaidia zaidi kwa kitu specific ninong'oneze tu(PM) maana naona tushaanza kuulizana ajira zetu hapa.
   
 7. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Halafu muheshimiwa kuna kitu umesahau wanaita DIY.....Mbona ni mambo ya kawaida tu haya, usiyatunishie misuli sana. Nilikuwa naomba software ya kufanya haya mambo, sasa kabla sijapata msaada inabidi nijieleze kama mimi ni mwanafunzi au mwalimu, nina umri gani, ni mtoto wa ngapi kuzaliwa, nimelelewa katika ukoo gani ili ndo utoe msaada wako...Duh! kazi ipo......Take it easy dude..!
   
Loading...