Natafuta wateja wa zabibu

Natafuta wateja wa zabibu

ba nso

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
668
Reaction score
225
Anayehitaji tufanye biashara ya zabibu ninamkaribisha.

Ni zabibu nyekundu, zipo na hali nzuri na mikungu mikubwa.

Bei maelewano kutokana na wingi wa mzigo na ninaweza kukujumlishia shamba zima la heka moja, nipo dodoma.

Karibuni sana.
 
Mkuu si uwasiliane na watu wa Tanzania Distilleries ltd? Hawa ni watengenezaji wa wine aina ya OVEMEER na DODOMA.
Nadhani wanahitaji sana hii kitu kama malighafi yao kuu. Kwa kuanzia naku - pm namba ya jamaa mmoja namfahamu anafanya kazi kwenye hiyo kampuni.
 
Anayehitaji tufanye biashara ya zabibu ninamkaribisha.

Ni zabibu nyekundu, zipo na hali nzuri na mikungu mikubwa.

Bei maelewano kutokana na wingi wa mzigo na ninaweza kukujumlishia shamba zima la heka moja, nipo dodoma.

Karibuni sana.

Ingekuwa ni ile nyeupe usingetangaza mkuu, jaribu kuongeza kwa kulima zabibu nyeupe, au udongo wako unagoma?
 
Mkuu mbona zabibu ni dili sana how comes umekosa soko? ukiwa na zabibu nyekundu unaweza wauzia jamaa wa wine hapo dodoma ukiwa na zabibu nyeupe ndo kabisaa wakenya wanazitafuta sana kwa ajili ya kuexport ulaya hasa spain
 
nyeupe inakubali sana tu lakini bado haipo nyingi nategemea mavuno yajaoyo ndipo itakua nyingi.
Ingekuwa ni ile nyeupe usingetangaza mkuu, jaribu kuongeza kwa kulima zabibu nyeupe, au udongo wako unagoma?
 
yes ni dili sana ila wanunuzi wa hapa wanapata mzigo mwingi na kusababisha kujipangia bei, wakati mwingine wanachukua kwa mkopo, kwa mfano hadi sasa tunadai madeni ya tangu msimu uliopita hata senti hatujapata.
Mkuu mbona zabibu ni dili sana how comes umekosa soko? ukiwa na zabibu nyekundu unaweza wauzia jamaa wa wine hapo dodoma ukiwa na zabibu nyeupe ndo kabisaa wakenya wanazitafuta sana kwa ajili ya kuexport ulaya hasa spain
 
yes ni dili sana ila wanunuzi wa hapa wanapata mzigo mwingi na kusababisha kujipangia bei, wakati mwingine wanachukua kwa mkopo, kwa mfano hadi sasa tunadai madeni ya tangu msimu uliopita hata senti hatujapata.

Kama nyeupe inamea hapo shambani kwako, basi ongeza ukubwa wa shamba mkuu ili uuze nje. Zabibu tangu kuoteshwa mpaka kuvunwa ni muda gani?
 
Nadhani huwa ni miezi tisa lakini huwa wanashauri uziache mpaka two yrs ndo uanze kuvuna
 
Mbona ni simple tu
Why not ADD BALUE TO YOUR PRODUCT, I.e
1.make your own simple wine nd sell kwa wateja wa hapo karibu nawe
2. Use solar dryer and sell them u can pack in small quantity nd im sure u will fetch quite more money than u do now

Huo ndo ushauli wangu kwako na wajasilimali wote
 
Back
Top Bottom