Natafuta vitabu vya Mohammed Said Abdulla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta vitabu vya Mohammed Said Abdulla

Discussion in 'Matangazo madogo' started by mdau wetu, May 1, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF naomba msaada wenu kwa Dar es Salaam naweza kupata wapi vitabu vya siku nyingi vya mwandishi mashuhuri Mohammed Said Abdulla. Nimetembea katika baadhi ya maduka ya vitabu bado sijafanikiwa kupata. Vitabu kama
  1.Duniani kuna watu
  2.Kisima cha Giningi
  3.Mke Mmoja Watume Watatu
  4.Siri ya sifuri
  5.Mzimu wa watu wa kale
  6.Kosa la bwana msa
  Kwa waleo waliobahatika kusoma vitabu hivi bila shaka watakubaliana nami kwamba, vitabu hivi vilikuwa vya kipekee katika taaluma ya uandishi. Naombeni msaada wenu
   
 2. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  masahihisho: 3. mke mmoja waume watatu au mke mmoja wanaume watatu
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,598
  Trophy Points: 280
  mdau wetu, ni kweli kabisa, mwandishi Mohamed Said Abdullah, Mzee MSA, ni mwandishi wa kipekee. Nadhani vitabu hivi havikuwahi kufanyiwa reprint, nilibahatika kuviona vichache used pale Masomo Bookshop Soko Kuu la Zanzibar.

  Last week nilisikia mtu akizungumzia Kisima Cha Giningi kimetolewa upya.

  Sehemu ambapo nakala za mwanzo zimehifadhiwa ni Maktaba Kuu ya Taifa ile sehemu ya reserve.

  Ni mwandishi huyu aliyenisaidia sana kupanua vocabulary yangu ya Kiswahili kwa maneno kama 'maliwatoni'.

  Pasco
   
 4. Hercule Poirot

  Hercule Poirot JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,195
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Mi ninavyo viwili DUNIANI KUNA WATU NA MZIMU WA WATU WA KALE viko ktk hali poa ni pm tuongee biashara
   
 5. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nipe nambari yako ya simu au Email nitakuwa Dar kuanzia mei 22 nikutafute, kwa sasa nipo nje ya nchi
   
 6. M

  Mwanangu Member

  #6
  May 1, 2011
  Joined: Nov 18, 2007
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kingine ni: Mwana wa Yungi Hulewa
   
 7. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 407
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mimi nimetokea Zanzibar karibuni, vipo badhi ya vitabu pale Masomo Bookshop, wasiliana nao, wapo karibu kabisa na marikiti kuu:israel::israel::israel::israel:
   
 8. G

  GHANI JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 685
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ni pm ninavyo hivyo vitabu.
   
 9. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,136
  Likes Received: 7,389
  Trophy Points: 280
  Kuna mdau anajua napoweza kupata kitabu cha ''SIKUNYONGWA''? Wahusika:
  MZEE HEGAL KAARL UROOSE,
  KABWE MAKANIKA,
  BI. HALIMA,
  PETER n.k.
   
Loading...